WITO WA UWAZI NA MAADILI: MBUNGE WA TAVETA, MHESHIMIWA JOHN OKANO BWIRE, AHOJIWE KUHUSU MGONGANO WA MASLAHI NA UTETEZI WA WATUHUMIWA WA UFISADI

Hon John Bwire - MP Taveta

 

TAREHE: 12 Novemba 2025

MAHALI: Taveta, Kaunti ya Taita Taveta  

Wakazi wa Taita Taveta na wadau wa haki za kijamii wameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu hatua ya Mbunge wao, Mheshimiwa John Okano Bwire, kuendelea kuwatetea mahakamani maafisa wa serikali wanaokabiliwa na tuhuma nzito za ufisadi, huku akiwa ni kiongozi wa kisiasa anayepaswa kusimamia na kutetea maslahi ya wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali na rekodi za mahakama, Bw. Bwire amehusishwa katika kesi zinazohusiana na ubadhirifu wa fedha za umma, zikiwemo zile za COVID-19 funds, fedha za TTC (Taita Taveta County), na kashfa nyingine kama ya Zanzibar Bonding Scandal. Aidha, taarifa zinaonesha kuwa amewahi kuwashtaki vijana waliokosoa utendakazi wa serikali ya kaunti.

Soma

VOI LAW COURTS FINES ROGERS NGOO KSH 12 MILLION AFTER A 5-YEAR WAIT

MY FIRM DIDN&#8217 IDRIS OVER GOVERNOR SAMBOJA’S POOR PERFORMANCE SAYS ADVOCATE BWIRE

Wananchi wanahoji:

  • Je, ni halali kwa Mbunge anayepaswa kusimamia rasilimali za umma, kuwatetea wale wanaoshukiwa kuzifisadi?
  • Je, huu si mgongano wa moja kwa moja wa maslahi (conflict of interest)?
  • Je, imani ya wananchi kwa uongozi wake itaendelea kuwepo huku akiwa upande wa watuhumiwa wa kuhujumu maendeleo yao?

Huu si tu mjadala wa kisheria, bali wa kimaadili na kisiasa. Iwapo kweli anajitolea kusaidia sekta mbali mbali  au kufanya maendeleo Taveta, kwa nini asimame kidete dhidi ya wale wanaodhoofisha huduma hizo?

Soma

MCAS MULTIMILLION BONDING TRIP TO ZANZIBAR 

BREAKING NEWS: ARREST OF TAITA TAVETA DEPUTY SPEAKER FOR EMBEZZLEMENT OF KSHS 17 MILLION IN A BONDING TRIP TO ZANZIBAR BY 30 OFFICIALS

THE RETURN OF THE LOOTERS: WHY IS GOVERNOR MWADIME RESURRECTING TAITA TAVETA’S DARK PAST?

Tunatoa wito kwa:

  • Bunge la Kitaifa, kuchunguza mienendo ya viongozi wanaokinzana na maadili ya uongozi.
  • EACC kufuatilia kwa kina kesi zinazomhusisha au kuhusisha watuhumiwa wanaotetewa naye.
  • Wananchi wa Taveta kuhoji na kuwajibisha viongozi wao kwa njia za kisheria na za kiraia.

Uwajibikaji ni msingi wa maendeleo. Kukaa kimya ni kuunga mkono ufisadi. 

Imetolewa na: KWAELA CIVIC FORUM

kwa niaba ya wananchi wanaotaka haki, uwazi, na maadili mema. 

 

more recommended stories