Kwa miaka na mikaka, wakaazi wa Kaunti ya #TaitaTaveta wamekuwa wakipata shida kutokana na wanyama pori. Kaunti hii imezingirwa na mbuga la wanyama la Tsavo. Takrim zinaashiria kuwa, takribani asilimia sitini na mbili ya ardhi ya Taita Taveta iko chini ya Tsavo. Hii imemewaletea wakaazi wa maeneo haya shida na hasara nyingi kupindukia.
Shida ya kwanza inasababishwa na ukosefu wa maji huko mbugani. Shirika la Kenya Wildlife Service na wizara ya Ministry of Tourism And Wildlife – Kenya wamezembea sana katika kuhakikisha kuwa kuna maji ya kuwatosha wanyama mbugani hasa wakati wa misimu ya kiangazi na ukame. Licha ya mbuga hili kuwaletea pato nono, kila mwaka, kutokana na utalii, hawajafanya juhudi mwafaka za kuhakikisha kuna maji ya kutosha, kama kuchimba visima (boreholes) vya maji huko mbugani. Sababu hiyo, inawalazimu wanyama kutoka mbugani na kuelekea maeneo ya wakaazi angaa kukata kiu, na hivyo basi kusababisha migogoro na wakaazi.
Kwa miaka nyingi, wakaazi wa Taita Taveta wamelalamika vikali kwa kuharibiwa mimea yao, mifugo kuuliwa, kuumizwa na hata kuuliwa wapendwa wao na wanyama pori. Malalamiko hayo huishia kwenye masikio yasiyosikia. Mpaka leo hii hamna suluhu mwafaka ya matatizo haya.

Shida ya pili ni ongezeko la idadi ya wanyama pori mbugani. Ni kama KWS imechukua mila na desturi za kimasai, eti kwamba wingi wa mifugo ndio utajiri!
Hawataki kupunguza idadi ya wanyama pori, hasa waliozeeka, ili wapatie wenzao nafasi. Kulingana nao, mpaka mnyama afe mwenyewe ndio ataondoka mbugani.
Isitoshe, tangu jadi, nyama za porini ,zimekuwa zimepigwa marufuku vikali. Yaani hata dikidiki 🦌 akinyongwa na nyasi mbugani kisha mkaazi amchukue na atengezee watoto wake kitoweo, akishikwa na maofisaa wa KWS anajutia siku yake ya kuzaliwa.
Maofisaa wa KWS wanajulikana kwa kuchukua sheria mikononi mwao.
Hata watoto kuwinda ndege, 🐦 na sungura 🐇 na wanyama wengine wadogo wadogo 🐿️ ni hatia.
Kutia kidonda chumvi, mapato ya TSAVO hayafikii wakaazi wa Taita Taveta. Wakaazi wanabaki wakijiuliza, faida ya TSAVO kwao ni ipi?
Hili ongezeko la idadi ya wanyama pori ndilo linasababisha migongano na wakaazi.
Hii italazimu KWS waanzishe kutumia mbinu za kisasa kuimarisha mbuga hili la wanyama. Hata raia siku hizi wanatumia mbinu za kitaalamu na za kisasa kuwachunga na kuwalisha mifuho wao, hasa ng’ombe 🐄, sababu mambo yamebadilika. Watu wameongezeka na sehemu ya ardhi ni ile ile.
KWS wao bado wako pale pale kwa miaka za mbeleni za ukoloni!
Inawapasa sasa waruhusu raia waanze kufanya uwindaji ndani ya TSAVO ili kupunguza idadi ya wanyama hao. Uwindaji huo uwe chini ya masharti na mwongozi fulani.
Kwa mfano, iruhusiwe tu kuuwa mnyama wa kiume aliyekomaa 🐏 ama aliyezeeka. Wanyama wa kike na wachanga, wachungwe. Masharti hayo yazingatiwe na yafwatiliwe kikamilifu. Wawindaji watambuliwe na wapewe vibali rasmi.
Kuwa na vifaru 🦓 zaidi ya laki mbili, nyati 🐃 zaidi ya laki, twiga 🦒 laki, na kadhalika, huko mbugani, ambazo hatuwezi kuzitunza ipaswavyo, kuna faidi nani? 🤷🏾♂️
Idadai ya wanyama ikifika kiwango kifaacho, wasitishe uwindaji.
Isiwe tu ni wao wanakula nyama choma ya wanyama pori, huko mafichoni na wakaazi wa Taita Taveta, waliozingira na TSAVO wanameza mate tu na kupata hasara ya wanyama hao.
Wakaazi wa #TaitaTaveta tuamke – KWAELA ! ☀️☀️☀️
more recommended stories
TAITA TAVETA: WE CANNOT CONTINUE THIS WAY — A COUNTY GOVERNMENT IN CRISIS OF ACCOUNTABILITYKwaela News Network | Editorial Taita.
DOCUMENT REVIEW: TAITA TAVETA COUNTY CIDP III (2023–2027)A Review of Planned Development Priorities,.
COVID-19 FUNDS IN TAITA TAVETA: YEARS AFTER THE AUDIT, WHO ANSWERED THE QUESTIONS — AND WHO WAS HELD ACCOUNTABLE?As High Court reduces Rodger Ngoo’s.
RUTO’S TAITA TAVETA TOUR: DEVELOPMENT INSPECTION OR PROMISE DELIVERY MISSION?President William Ruto is expected to.
VOI THIRSTS AS LEADERS TRADE STATEMENTS, EXCUSES AND BLAMEYears of promises, unpaid.
MRUGHUA SOCIAL HALL: A DECADE OF WAITING, MILLIONS SPENT, AND STILL NO ANSWERSTen Years Later, Why Is.
SIX-YEAR DEFAMATION CASE ENDS AS COURT AWARDS COSTS TO KWAELA NEWS NETWORK, BUT QUESTIONS OVER COVID-19 FUNDS REMAINVOI, TAITA TAVETA — A six-year.
Family, Power and Public Trust: The Questions Governor Wakujaa Must AnswerThe latest appointments in Taita Taveta.
PETITIONERS FAIL TO PROVE OWNERSHIP OF 1,306 HECTARES AS COURT DISMISSES NDARA B LAND CASECase: Gadiel Mnyambo Mwaisama & Others.
NJORO KUBWA OR MZIMA PHASE II? WEIGHING TAITA TAVETA’S BIG WATER OPTIONSWater has long been one.
WHY KENYANS ARE TURNING AGAINST SAFARICOM OVER SURVEILLANCE FEARSFor years, Safaricom has enjoyed enormous.
FIRES, FEAR AND FAILURE: THE HARD QUESTIONS TAITA TAVETA SCHOOLS MUST ANSWERA disturbing pattern is emerging in.
PARIS JUU YA MACHOZI YETU: AIBU YA VIONGOZI WALIOSAHAU WATU WAOKatika wakati ambapo wananchi wa.
ISANGAIWISHI DEVELOPMENT COMMUNITY OFFICIAL STATEMENT ON LAND OWNERSHIP, HISTORICAL RECORD, AND DEVELOPMENT1. Introduction The Isangaiwishi Development Community.
AUDIT SHOCKER: HUNDREDS OF MILLIONS IN WORKERS’ DEDUCTIONS UNACCOUNTED FOR AS FINANCE SHAKE UP ROCKS TAITA TAVETABy Kwaela News Network Investigations Desk.
COURT EXPOSES ILLEGAL IMPEACHMENT: TAITA TAVETA COUNTY ASSEMBLY FAULTED FOR RUSHED, UNCONSTITUTIONAL REMOVAL OF SPEAKER MWAMBURIMombasa, Kenya — In a damning.

Leave a Comment