TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MZOZO WA BAJETI KATIKA KAUNTI YA TAITA TAVETA.

Aliyekuwa Gavana wa Kaunti yaTaita Taveta Bw John Mruttu

Sisi tulio orodheshwa hapo chini tunatoa taarifa ifuatayo ili kushindikiza msimamo wa viongozi wa dini kuhusu mzozo wa bajeti katika Kaunti ya Taita Taveta.

Kama mjuavyo Kaunti ya Taita Taveta imekumbwa na mzozo kati ya Executive na County Assembly kutokana na kutoelewana kuhusu bajeti ya matumizi ya fedha za serikali kwa  kipindi cha mwaka 2019/2020. Ili kuwezesha shughuli za serikali kuendelea ipaswavyo,  pande zote mbili zilikubaliana kupitisha vote-on-account ambayo inaruhusu matumizi ya  asilimia hamsini (50%} ya fedha kwa kulipa mishahara ya wafanya kazi na gharama  nyingine isipokuwa miradi ya maendeleo.

Kutokana na msukosuko huo, Gavana wa Kaunti alitangaza nia yake ya kutaka serikali ya kaunti ivunjwe na akaanzisha zoezi la kukusanya sahihi kutoka kwa wananchi wa Kaunti  ili kutimiza malengo hayo. Gavana ametangaza kwamba mpaka hivi sasa amekusanya  sahihi takribani elfu hamsini na mbili.



Viongozi wa kidini na vile vile viongozi wengine katika kaunti hii wamekuwa mara kwa mara wakisihi Gavana na bunge la kaunti kufanya mazungumzo ili kujaribu kutatua mzozo  huo. Mnamo tarehe 26/08/2019 viongozi hao wa dini walitoa taarifa wakisisitiza haja na  umuhimu wa mazungumzo kama njia ya kutatua mzozo huo.

Sisi kama washika dau katika maswala ya kaunti hii ya Taita Taveta tunaunga mkono haki ya kikatiba ya viongozi wa dini, au kundi lingine lolote au watu binafsi kuwa na maoni yao  na vile vile haki ya kutamka hayo maoni. Letu si kutoa hukumu kwamba ni pande gani iko  sawa na ni ipi ina makosa bali kusisitiza kwamba hapa nchini Kenya kuna uhuru wa  kuzungumzia jambo lolote kulingana na katiba.

Pia tunapinga vikali shutuma na lawama zote zinazo elekezwa kwa viongozi wa dini kama ambao hawana haki ya kutoa maoni yao. Tungependa ikumbukwe kwamba hata Taifa letu  la Kenya limefaidi pakubwa kutokana na maoni ya viongozi wa kidini wakati kumekuwa  na machafuko. Msimamo wetu ni kwamba viongozi wa dini na hata viongozi wengine  katika jamii wanastahili heshima. Kwa hivyo tunashindikiza Gavana na Bunge la Kaunti  wasikie mwito huo wa viongozi wote na waanze mazungumzo kabla kuchukuwa hatua  hiyo ya kuvunja serikali ya Kaunti hii ya Taita Taveta.

Mhe John Mtuta Mruttu

Mhe Dan Mwazo

Mhe Thomas Mwadeghu

Mhe Callistus Mwatela

Mhe Joyce Lay

Mhe Khamis Chome Abdi

more recommended stories