GAVANA WA TAITA TAVETA ACHAGUA KUKEMEA NJE LAKINI KUNYAMAZIA UFISADI NDANI

 

Taita Taveta, Oktoba 22, 2025 —

Wananchi wa Taita Taveta wameeleza mshangao na kutoridhishwa na hatua ya Gavana H.E. Dkt. Andrew Mwadime (Wakujaa) kushiriki hadharani kulaani uongozi wa Gavana Mutahi Kahiga wa Nyeri, huku akikaidi kukemea suala nyeti la vyeti ghushi ndani ya serikali yake mwenyewe.

Hii ni baada ya madai ya kughushi vyeti dhidi ya CEC wa Ardhi, Bi. Christine Zighe Mwashighadi, kuibuliwa pamoja na ushahidi kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN) kuthibitisha kuwa shahada anayoidai si halali. Hata hivyo, licha ya uzito wa tuhuma hizo, Gavana hajachukua hatua yoyote wala kutoa tamko rasmi.

Kinyume chake, anapatikana akihutubia hafla za umma katika kaunti nyingine, akiwalaumu viongozi wengine juu ya masuala ya kimaadili — hatua inayotafsiriwa na wengi kama unafiki wa kisiasa.

Wananchi wanahoji:

  • Kwa nini Gavana hawezi kuonyesha ujasiri kama huo dhidi ya maovu ndani ya serikali yake?
  • Kwa nini tuhuma za kughushi vyeti, jambo linalodhalilisha taaluma na uadilifu wa utumishi wa umma, zinapuuzwa?

Wakati wananchi wakihitaji majibu na hatua thabiti dhidi ya maovu ndani ya serikali ya kaunti, viongozi wao wanatoa mihadhara ya maadili kwa wengine.

Mwito wetu kwa Gavana Wakujaa ni huu: 

Anza kusafisha nyumba yako kabla hujahubiri usafi kwa majirani. Wananchi wanahitaji uongozi wa ukweli, uwajibikaji wa ndani, na si siasa za maonyesho.

Taitans wanastahili uwajibikaji, si ukimya wa kisiasa.

#WanTam

#UwajibikajiKwanza

#FakeDegreesMustFall

more recommended stories