AMEKONDA KAMA MOJA!

 

Hata Akatiwa Chaja, Hajai Akawa Juba,

Amekonda Kama Teja, Hanayo Tena Haiba,

Mtaani Ni Kioja, Salama Habebi Koba,

Kazi Kashindwa Samboja, Amekonda Kama Moja

Limevuka Lake Koja, Na Maguu Tele Miba,

Aona Haya Angoja, Lau Sivyo Angeiba,

Kakonda Kama Mrija, Mana Hali Akashiba,

Kazi Kashindwa Samboja, Amekonda Kama Moja,

Mambo Huwapata Waja, Yamemkuta Ngariba,

Malimwengu Yana Fuja, Ya Fujapo Ni Msiba,

Ameshavuka Daraja, Aomba Japo Kibaba,

Kazi Kashindwa Samboja, Amekonda Kama Moja,

Mambo Huambwa N’kangaja, Ela Yazidi Dhoruba,

Naye Angoja Yakija, Ajaliwacho Sihaba,

Yalo Mawi Ayatuja, Hathubutu Kuyabeba,

Kazi Kashindwa Samboja, Amekonda Kama Moja!

Ninani Atamtaja, Akumbuke Zake Huba,

Akumbuke Siku Moja,Yeye Alimpa Tiba,

Na Leo Japo Kipaja, Ampe Njaa Kuziba,

Kazi Kashindwa Samboja, Amekonda Kama Moja.

Hapa Namaliza Hoja, Shujaa Wa Sabasaba

Wala Sihongeki Mja, Mi Simba Aliyeshiba

Jamuhuri Wanataja, Jina La Vuma Sihaba

Kazi Kashindwa Samboja, Amekonda Kama Moja!

MALENGA WA TAVETA-SULTANI JAMUHURI

*©2022*

more recommended stories