AFYA YETU YA KAUNTI INAUMWA …

 

 

Na Joel Mburia”Rangile”

Afya yetu inaumwa,

Sasa iko kitandani,

Yaendelea kufinywa,

Na imetiwa pembeni,

Idara nzima yaumwa,

Yelekea kaburini,

Afya yetu inaumwa,

Wagonjwa wanaumia.

 

We nenda hospitalini,

Uchunguze pole pole,

Usiseme narubuni,

Ingia huku na kule,

Dawa hamna jamani,

Msiseme ni kelele,

Afya yetu inaumwa,

Wagonjwa wanaumia.

 

Usemapo unalengwa,

Unafanyiwa adui,

Ukicheza utapigwa,

Kwao wewe ni adui,

Afya yote yalemewa,

Wafikiri hawajui?

Afya yetu inaumwa,

Wagonjwa wanaumia.

 

Mipangilio waanza,

Tarumbeta kuzipiga,

Vuvuzera zinaanza,

HUKU kule tutapiga,

Uozo tutatangaza,

Bila mtu kumpiga,

Afya yetu inaumwa,

Wagonjwa wanaumia.

 

Najikunyata pembeni,

Kheri kufanyike kitu,

Afya irudi laini,

Tunataka kila mtu,

Ajue afya i taabani,

Ndani kumejaa kutu!,

Afya yetu inaumwa,

Wagonjwa wanaumia.

Asanteni 🤣

more recommended stories