WAFANYI BIASHARA TAVETA WAPINGA UCHAGUZI WA LEO

Taveta Sokoni

Wafanyi biashara wengi wa Taveta wamepinga vikali uchaguzi uliofanyika leo, wakidai kuwa haukuwa halali na haukuwapa nafasi ya kushiriki kikamilifu.

Kwa mujibu wa wafanyi biashara hao, walipigiwa firimbi ya kuitwa kwenye uchaguzi jana bila kupewa muda wa kutosha kujiandaa. Wanasema hatua hii ililenga kuwapitisha viongozi waliopendekezwa na Ofisi ya Trade ya Kanjo badala ya wale wanaochaguliwa na wafanyi biashara wenyewe.

Malalamiko makubwa yanaelekezwa kwa maafisa wa Trade waliotajwa kama Moka na Aquilina, ambao wanadaiwa kuongoza mchakato huo kwa njia isiyo ya haki. Wafanyi biashara wanasema walinyimwa nafasi ya kuchagua viongozi wao, hususan nafasi ya mwenyekiti, ambapo walitaka kuchagua wao lakini badala yake majina yalipendekezwa moja kwa moja na maafisa wa Kanjo.

Hali hii imezua maswali miongoni mwa wafanyi biashara:

  • Je, kamati ya soko ni ya wafanyi biashara au ni ya Kanjo?
  • Kwa nini viongozi wanapendekezwa na maafisa badala ya kuchaguliwa na wanabiashara?
  • Je, soko la Taveta ni la wafanyi biashara wote au la kikundi maalum?

Wafanyi biashara wanasisitiza kuwa soko ni mali ya wote, na si wachache au kundi fulani kama mama mboga pekee. Wanataka haki ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa viongozi wao.

Aidha, wameonya kuwa hawatakubali matokeo ya uchaguzi huo na wameitaka serikali ya kaunti kurudia mchakato huo kwa njia ya haki na uwazi. Vinginevyo, wameashiria kuwa wako tayari kuchukua hatua zaidi, ikiwemo maandamano.

“Soko ni la wafanyi biashara wote, sio wachache. Viongozi wawekwe na wafanyi biashara, sio kwa mifuko,” walisema kwa pamoja.

more recommended stories