TIMU YA TAVEVO FC INAYOSAMBAZA MAJI TAITA TAVETA YAPEPETWA 3-0 NA TIMU YA MAUNGU ALL STARS UWANJANI SGR

 

Hio Jana Wachezaji wa Timu ya Tavevo Fc walikua wageni wa Timu ya Maungu all stars Wakicheza Mechi ya Kirafiki Uwanjani SGR ambapo Timu Hio ya Maji iliweza Kurindimwa Mabao Matatu Kwa Ndunge na Mabingwa Wa Ndovuni.

Kizito Kuzika Wa Maungu all stars Ndie aliyefungua Mifereji Ya Mabao Huku Bazenga Wa Timu ya Maungu all stars Victor Kawa akifunga Bao la Pili Kwenye Sentahafu Alipopiga Shuti Nzito lililoshindwa Kunyakwa na Mlinda Lango wa Timu Ya Maji Hamisi Mwembe.

Akifunga Ukurasa Wa Mabao Mwalimu Kaluva Alifunga Bao La Tatu Baada ya Mabeki wa Timu ya Tavevo Kushindwa Kuhimili Kasi Ya Wachezaji Wa Timu Ya Maungu All stars Fc.

Wakishuhudia Mechi Hizo , MCA Mtarajiwa Wa Marungu Wadi Bwana Idris Mohammed na Mwenzake Seneta Mtarajiwa Bwana John Righa waliwapongeza Wachezaji Wote Kwa Kuonyesha Mchezo Mzuri wa Kukata Na Shoka Huku wakiahidi Kuinua Na Kukuza talanta Pindi Watakapochaguliwa Kuwakilisha Wananchi Kwenye bunge la Kaunti na Lile la Seneti AGOSTI Mwaka Huu wa 2022.

~ Maungu All Stars FC

more recommended stories