Categories: *Featured News

TATIZO LA WANYAMA PORI TAITA TAVETA

Kwa miaka na mikaka, wakaazi wa Kaunti ya #TaitaTaveta wamekuwa wakipata shida kutokana na wanyama pori. Kaunti hii imezingirwa na mbuga la wanyama la Tsavo. Takrim zinaashiria kuwa, takribani asilimia sitini na mbili ya ardhi ya Taita Taveta iko chini ya Tsavo. Hii imemewaletea wakaazi wa maeneo haya shidaΒ  na hasara nyingi kupindukia.

Shida ya kwanza inasababishwa na ukosefu wa maji huko mbugani. Shirika la Kenya Wildlife ServiceΒ na wizara ya Ministry of Tourism And Wildlife – Kenya wamezembea sana katika kuhakikisha kuwa kuna maji ya kuwatosha wanyama mbugani hasa wakati wa misimu ya kiangazi na ukame. Licha ya mbuga hili kuwaletea pato nono, kila mwaka, kutokana na utalii, hawajafanya juhudi mwafaka za kuhakikisha kuna maji ya kutosha, kama kuchimba visima (boreholes) vya maji huko mbugani. Sababu hiyo, inawalazimu wanyama kutoka mbugani na kuelekea maeneo ya wakaazi angaa kukata kiu, na hivyo basi kusababisha migogoro na wakaazi.

Kwa miaka nyingi, wakaazi wa Taita Taveta wamelalamika vikali kwa kuharibiwa mimea yao, mifugo kuuliwa, kuumizwa na hata kuuliwa wapendwa wao na wanyama pori. Malalamiko hayo huishia kwenye masikio yasiyosikia. Mpaka leo hii hamna suluhu mwafaka ya matatizo haya.

Mimi nimeoshwa na ndovu. Fomu za kutafuta fidia kwa KWS tumekuwa tukijaza. Tunazungushwa weee tumechoka. – Mkaazi wa Taita Taveta analalamika.

Shida ya pili ni ongezeko la idadi ya wanyama pori mbugani. Ni kama KWS imechukua mila na desturi za kimasai, eti kwamba wingi wa mifugo ndio utajiri!

Hawataki kupunguza idadi ya wanyama pori, hasa waliozeeka, ili wapatie wenzao nafasi. Kulingana nao, mpaka mnyama afe mwenyewe ndio ataondoka mbugani.

Isitoshe, tangu jadi, nyama za porini ,zimekuwa zimepigwa marufuku vikali. Yaani hata dikidiki 🦌 akinyongwa na nyasi mbugani kisha mkaazi amchukue na atengezee watoto wake kitoweo, akishikwa na maofisaa wa KWS anajutia siku yake ya kuzaliwa.

Maofisaa wa KWS wanajulikana kwa kuchukua sheria mikononi mwao.

Hata watoto kuwinda ndege, 🐦 na sungura πŸ‡ na wanyama wengine wadogo wadogo 🐿️ ni hatia.

Kutia kidonda chumvi, mapato ya TSAVO hayafikii wakaazi wa Taita Taveta. Wakaazi wanabaki wakijiuliza, faida ya TSAVO kwao ni ipi?

Hili ongezeko la idadi ya wanyama pori ndilo linasababisha migongano na wakaazi.

Hii italazimu KWS waanzishe kutumia mbinu za kisasa kuimarisha mbuga hili la wanyama. Hata raia siku hizi wanatumia mbinu za kitaalamu na za kisasa kuwachunga na kuwalisha mifuho wao, hasaΒ  ng’ombe πŸ„, sababu mambo yamebadilika. Watu wameongezeka na sehemu ya ardhi ni ile ile.

KWS wao bado wako pale pale kwa miaka za mbeleni za ukoloni!

Inawapasa sasa waruhusu raia waanze kufanya uwindaji ndani ya TSAVO ili kupunguza idadi ya wanyama hao. Uwindaji huo uwe chini ya masharti na mwongozi fulani.

Kwa mfano, iruhusiwe tu kuuwa mnyama wa kiume aliyekomaa 🐏 ama aliyezeeka. Wanyama wa kike na wachanga, wachungwe. Masharti hayo yazingatiwe na yafwatiliwe kikamilifu. Wawindaji watambuliwe na wapewe vibali rasmi.

Kuwa na vifaru πŸ¦“ zaidi ya laki mbili, nyati πŸƒ zaidi ya laki, twiga πŸ¦’ laki, na kadhalika, huko mbugani, ambazo hatuwezi kuzitunza ipaswavyo, kuna faidi nani? πŸ€·πŸΎβ€β™‚οΈ

Idadai ya wanyama ikifika kiwango kifaacho, wasitishe uwindaji.

Isiwe tu ni wao wanakula nyama choma ya wanyama pori, huko mafichoni na wakaazi wa Taita Taveta, waliozingira na TSAVO wanameza mate tu na kupata hasara ya wanyama hao.

Wakaazi wa #TaitaTaveta tuamke – KWAELA ! β˜€οΈβ˜€οΈβ˜€οΈ

Mwachere Shuma

Leave a Comment
Share
Published by
Mwachere Shuma

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED β€” HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

18 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE β€” FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago