Katibu Mkuu wa Mwasima Mbuwa Welfare Society Bw. Mwaluma Mnjala
Na Mwandishi wa Kwaela News Network
Ni wazi kwamba ardhi ni moja ya rasilmali kuu za uzalishaji mahali popote duniani. Hivyo basi ilikuwa ni furaha yangu kuu asubuhi ya leo, kusikia kupitia kwa chombo kimoja cha habari ya kwamba wananchi wa Majengo Singila, eneo la Mwatate, watamiliki ekari takriban mia mbili na hamsini kutoka kwa shamba la makonge la Teita Estates Ltd. Ripoti hiyo ni sawia na semi ambazo Waziri wa Ardhi wa Kaunti ya Taita Taveta, Ndugu Mwandawiro Mghanga, alizitoa katika studio za Anguo FM yapata kama mwezi mmoja uliopita sasa. Isitoshe, Mwandawiro aliongeza kusema kwamba eneo lengine la takriban ekari mia tatu, zimetengwa kutoka kwa shamba hilo hilo lamakonge, kwa manufaa ya wananchi wa Landi.
KIU YA MASHAMBA
Umiliki wa ardhi hiyo, hasa kwa wananchi wa Singila Majengo, ni ushindi mkubwa kwao, hasa ukitilia maanani ya kwamba waliungana chini ya “SINGILA MAJENGO GROUP” kutetea ardhi hito katika kesi ambayo iliamuliwa tarehe 11 Mei mwaka wa 2011.
Kwa kuwa ongezeko la watu limeleta presha ya umiliki wa ardhi, hasa katika maeneo ya milimani, watu wengi hukimbilia mahali popote wasikiapo ya kuwa kuna ardhi inauzwa, au kugawanywa. Kiu hii ya ardhi ndio ilipelekea jamaa fulani kuungana na kuunda kikundi cha “Welfare Group” ambacho wamekuwa wakihadaa wananchi kwamba “watawagawanyia maelfu na maelfu ya ekari ambazo zilinyakuliwa na shamba la Teita Estates”. Hata ingawa “Welfare Groups” haziruhusiwi kuingilia maswala ya uwekezaji na ununuzi wa ardhi, kundi hilo lilijisajili kwa jina la MWASIMA MBUWA WELFARE SOCIETY.
Ajabu ni kwamba viongozi wa kundi hilo la Mwasima Mbuwa Welfare Society, ambalo wananchi wa Taita Taveta wamelichangia mamilioni ya pesa kwa miaka zaidi ya kumi kufikia sasa, wamegeuka kuwa mabubu, wasiseme lolote kuhusu hatima ya ardhi hii iliyotolewa kwa wananchi. Hawataki kusema ukweli ya kwamba ARDHI HIYO IMETOLEWA KWA WAKAZI WA SINGILA MAJENGO – na haitafaidi wananchi wote wale waliotapeliwa na Mwasima Mbuwa. Badala yake, kila “wanahisa” wanapopiga simu, wanazidi kuhimizwa kutoa hela zaidi “ili kupata ekari kubwa zaidi wakati wa mgao” na vile vile, kushurutishwa waongeze hela zengine “kama gharama za kumlipa wakili wetu”.
MASWALI KWA MWASIMA MBUWA
Swali la kwanza ni : kwa nini wananchi waendelee kutoa pesa kwa wakili wakati tayari koti iliamua kitambo sana (Mei 11, 2011) ya kwamba ardhi yote ya shamba la Teita Estates ipimwe na MASOROVEYA KUTOKA PANDE ZOTE HUSIKA ili ibainishwe ikiwa ni kweli shamba hilo la makonge limenyakua eneo zaidi ya ekari elfu thelathini, ambazo ndio inazomiliki kihalali. Matokeo ya usoroveya huo ulibainisha ya kwamba shamba hilo limekalia eneo ya ekari 30,284.
Swali lengine : “Ni nini hatima ya mamilioni yote wananchi walitoa kwa kununua shamba ambalo ni wazi sasa ya kwamba ni “shamba hewa” lililoahidiwa na watapeli hawa?
MAJONZI
Inasikitisha sana kusikia vile waliotapeliwa na genge hilo wanapitia mateso makubwa kwa hasara waliyopata. Wengine waliaga dunia kwa sababu ya magonjwa kama presha na “depression”. Wengine wanalipa loni walizokopa, wengine wakauza mifugo yao…..na hadi sasa, baada ya miaka zaidi ya kumi kumi, bado wanazidi kushurutishwa waongeze pesa zaidi! Majonzi haya si kwa watu binafsi pekee : kupitia kwa bwenyenye mmoja anayefanya biashara zake Mombasa, hata makampuni mengi na vyama vingi vya ushirika viliweza kushawishiwa na kuingiza mamilioni kwenye kashfa hii ambayo imeelekea kutajirisha bwenyenye huyo na viongozi wa Mwasima Mbuwa Welfare. Isitoshe, bwenyenye huyo hakukomea hapo : alishawishi makanisa mengi “kuwekeza” rasilmali zao vile vile. Sasa waliotapeliwa wamejikuta kwenye njia panda – utaendaje kuombewa kwa hasara uliyopata ilhali kanisa hilo hilo unaenda kuombewa pia limetapeliwa?
KURUDISHIWA FIDIA
Siku za hivi majuzi, tangu Mwandawiro Mghanga kufichua ukweli wa mambo, watu wengi wamejua kuwa pesa zao zimeliwa na wajanja. Katika ofisi za Mwasima Mbuwa pamoja na Bweyenye huyo wa Mombasa, imekuwa hali ya “mwenye nguvu mpishe”. Wale walio na uwezo wa kushtaki matapeli hao ndio wanaorudishiwa pesa zao kwa njia ya siri. Maskini walala hoi – kama ilivyo kawaida – ndio wanaachwa wapambane na hali zao.
Ombi langu ni hili : Mwasima Mbuwa warudishie watu wote pesa zao BILA YA KUBAGUA. Lau sivyo waliotapeliwa wataungana na kuwashtaki wahusika wote waliowatapeli.
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
View Comments
How come no one is raising up to sue the scammers? 🤷🏾♂
Where are the TTC leaders who unleash the ru… https://t.co/dP0Sd8UEnP
Hata na sisi pia tumetapeliwa pesa nyingi
So you mean we were conned ? I am a victim !
Ikiwa Habari hizo siyo uzushi, Wananchi waliolaghai wanapaswa kujitokeza kuelezea ukweli ili wapate usaidizi kutoka kwa serikali.
Let's start a watts up group mwasimabuva,refunds group. Collect victims names and amounts paid that must be refunded and then report to CID
We are conned too we are victims
Immediately I was elected to parliament I did a thorough background check of the MWASIMA MBUWA issue, using the relevant Ministry of Lands officers led by the then District Land Surveyor Mr Kinanda.
Mr Kinanda and team compiled a report showing that the claim by Mnjala Mwaluma of Mwasima Mbuwa Welfare Association-Mwatate was a fabrication.
I went ahead and held a meeting at Shasha Camp with all my councillors where Mr Kinanda presented the report and we agreed that the councillors would in turn use all relevant forums including churches to educate the masses.
Despite all this the population chose to believe Mnjala Mwaluma instead of the councillors they had elected.
What can anyone do to help someone who has consciously chosen to be conned?
~ Hon Calist Mwatela
******
Former MP - MWATATE CONSTITUENCY
Osighilwa mlungu..
thank you Lord i almost fall a victim but i chose not pay till i see the light
Huyu jamaa ni kaaa babake atakimbia na sijulikane alipo history reapets itself mwana wa choka n choka
I happened to be a victim after dad,siz and i we paid them