Miaka za tisini na kurudi nyuma, mtu angesimama pale Mwasange Shopping Centre, Mrughua, masaa ya asubuhi ama jioni kisha aangalie huko juu Vuria na Mwasoko, angeona vitu vyeupe vikizururazurura. Vitu hivyo vilikuwa vinakwea mawe na kushuka. Mwasange ndiko mahali serikali ya kaunti imekuwa ikijenga social hall kwa zaidi ya miaka mitano sasa. Tukiwa wadogo tulikuwa tunaambiwa ni mbuzi wa mashetani. Baadaye mbuzi hao walikuwa wanapotea bila kuaga.
Hivi karibuni kupitia kwa Google Earth, nimeona mbuzi kama hao weupe wako huko 📍 Kishushe. Wanazurura kwa kamlima fulani huko. Tofauti na wale wa Vuria na Mwasoko ni kwamba hawa wa Kishushe wana mchungaji. Asubuhi na mapema wanaonekana wakitoka kwenye boma fulani hapo chini ya mlima wakielekea mlimani. Jioni wanarudishwa nyumbani.
Wacha niachane na mambo ya hawa mbuzi, kwasababu nikiuliza ni wa nani, wangwana fulani watajitokeza kuniambia niache udaku na kimbelembele kama kina mama wa soko mjinga. Ama waninunulie dera nivae angaa nitambulike wazi kuwa nina umama ndani yangu. Wengine wataongezea kwamba kama nimekosa kazi, nichukue jembe nikalime. Bila shaka kuna wale wataniambia kuwa ninasumbuliwa na wivu.
Haidhuru, yote nitayapokea vyema, kwasababu nimewachokoza mimi mwenyewe. Nimeachana na mbuzi sasa niko kwa zizi la mbuzi.
Jengo Mbugani
Kando ya zizi hilo, kama tulivyoweka pin 📍 hapo juu, kuna mjengo unaendelea. Kulingana na picha zinazoonekana kwa Google Earth, mjengo huo, licha ya kuwa katikati ya mbuga, unaonekana wa kisasa na unaogharimu hela nyingi. Niliporudisha Google Earth nyuma kwa miezi kadhaa, inaonekana hapo kwenye jengo hilo kulikuwa na borehole drilling rig.
Wangwana walinena, udaku wahitaji muda. Niliamua kuchukua wasaa na nikatuma jamaa fulani akachunguze kinachoendelea hapo.
Jamaa kufika huko alipigwa na butwaa alipo ona jumba si jumba linajengwa huko mbugani. Kulikuwa na wajenzi kadhaa waliokuwa wanaendelea na kazi yao. Jamaa wangu alizuru hekalu hili huku shughuli zikifanywa kama kawaida. Akagundua kweli kuna kisima kimechimbwa pale. Tayari kilikuwa kinangojea kufanyiwa furnishing, na maji yawe tayari kutumika hata nyumbani.

Mali ya kaunti
Upelelezi uliofwata ulibaini kuwa kisiwa hicho kilichimbwa na drilling rig ya serikali ya kaunti ya Taita Taveta. Pia yadaiwa kuwa, jumba linajengwa kwa kutumia simiti, vyuma na vifaa vingine vingi, vilivyotoka kwa miradi ya serikali ya kaunti. Baadhi ya miradi hiyo imekwama sababu ya kukosa vifaa na hela. Kumbe miradi inakwamishwa na ubadili wa aina hii? Ambapo mtu binafsi anaamua kunyakua mali ya uma na kujifaidisha.
Hii ina maana kwamba, Bunge la Kaunti lilipopitisha sheria ya kuruhusu serikali ya kaunti ifanye biashara na drilling rig ya serikali, ilifungua mwanya wa watu binafsi kunufaika na mashine ya uma kwa malipo fulani? Cha ajabu ni kwamba kwenye orodha ya mapato ya kaunti ya mwaka 2020/2021, hakukua na mapato yoyote kutokana na drilling rig. Bila kumumunya maneno tunaweza jijazia kuwa, mjenzi huyu alipata huduma ya chombo cha serikali ya kaunti bila kulipa hata centi moja. Na hii ni kinyume na matarajio. Ni haki kweli?
Maswali Yanayoibuka
Kuna wale wanasema eti hawa wangwana wanajenga kwa kutumia mikopo. Tunawauliza maswali:
1. Ni benki lipi linaweza patia mtu mkopo wa kiwango cha pesa ambacho hakiendi sawa na mapato yake?
2. Na kama kweli wanatumia mikopo kujenga majumba ya kifahari namna hii, basi wajitokeze hadharani, waseme hivyo. Pia Ikiwa wataulizwa kuonyesha stakabadhi za mikopo wawe tayari kuziweka bayana.
Tunaweza bahatisha kuwa Bunge la Kaunti likisukumwa kufanya uchunguzi, mwishowe litabana ukweli. Huenda ikawa litatoa ripoti kuwa, mapato hayo ya drilling rig yataonekana kwenye ripoti ya hesabu ya mwaka wa 2021/2022 na wala si vile tunavyotarajia.
Baada ya kupata taarifa hii niljiuliza maswali kadhaa.
1. Ni nani anajenga nyumba ya kifahari kama hii porini?
2. Je, mwenye jengo hili, anatoa pesa wapi, ilhali majirani wake wote wanakisiwa kuwa ni maskini?
3. Ni muujiza gani amefanya akapata hela za kufanya mradi wa aina ile msituni?
4. Jee analipa ushuru kutokana na huo muujiza wake unaomletea hela zote hizo?
Bado sijapata majibu ya maswali haya yote.
Hata hivyo tunandaa ripoti ya tuliyoyaona pale 📍 Birikani – Voi.
Mwandishi ni mwanaharakati sugu wa kaunti ya Taita Taveta
Mhariri ni Maria Nene
more recommended stories
TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSUREThe growing controversy surrounding the.
NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULINGAffected families in Mlambenyi, Golani and.
TAITA TAVETA: WILL DEBORAH WAKESHO SUCCEED THE LATE MARGARET KAWUKI, OR WILL POLITICAL CARTELS INTERFERE?Questions emerge over Jubilee Party’s.
CHRISTOPHER MWAMBINGU: EACC INVESTIGATES ALLEGED FORGED DEGREE USED TO SECURE DIRECTOR OF ADMINISTRATION POSITIONA third case raises further.
MWATATE MP RACE: RICHARD LUKINDO’S AMBITIONS AND THE UNANSWERED DEGREE QUESTIONThe political stakes surrounding former.
TAITA TAVETA: PRISONS OFFICER, NINE OTHERS ARRESTED IN MOTORCYCLE THEFT SYNDICATE PROBESerious questions emerge over alleged security.
ALLEGATIONS OF HARASSMENT RETURN ALONG VOI-CALTEX ROAD CORRIDORResidents, motorists, and public transport operators.
CHURU CHURU PROJECTS HAZIJENGI TAIFAKuna tofauti kubwa kati ya.
BWIRE: ACCESS TO POWER IS NOT A POLITICAL MANDATEHon. John Bwire’s declaration that.
RESIDENTS RAISE CONCERNS OVER ALLEGED MOTORIST HARASSMENT ALONG VOI-MOMBASA ROADResidents and motorists in Voi.
THE TAITA TAVETA COUNTY ASSEMBLY’S VETTING PROCESS MUST UPHOLD THE CONSTITUTION AND PUBLIC TRUSTWe, the concerned citizens of Taita.
THE STRUCTURED POVERTY IN TAITA TAVETAResidents demand answers after thousands.
Taita Taveta Workers Demand Immediate Payment of Salaries and AllowancesFrustration is mounting among employees in.
Nepotism Concerns Intensify as Family Links Dominate Senior Appointments in Taita Taveta CountyCalls for transparency and fairness in.
UNGA, POLITICS AND 2027: PS MWAMODO’S JORA VISIT SPARKS DEBATEA food distribution exercise led by.
Taita Taveta Residents Increasingly Question Leaders’ Priorities Amid Unresolved ChallengesWhat was billed as a development.

Thanks for sharing this.like any other complains these beautiful and useful words tend to fall in deaf ears from the so called superior elders and the locals who thinks their voices can not be heard or even put them behind bars.unless people unite and open their eyes things may remain the same decade after decade.