KWAELA WELFARE GROUP – KATIBA NA SHERIA. 

 

1.JINA LA CHAMA: KWAELA WELFARE GROUP.

LENGO LA CHAMA. 

a) Kuwatia moyo wataita/wataveta kujiunga kama mwanachama.

b) Kushirikiana pamoja wakati wa shida, hasa kifo kwa mmoja wetu au jamaa yake.

c) Chama kitashuhulikia kusafirisha Mwili kwa mazishi, nyumbani kadri ya kiwango cha pesa kitakacho wekwa na wanachama.

d) Ikiwa mwanachama atashuhulikiwa na muajiri wake basi chama kitatos pesa sawa ya gharama ya gari na jeneza kwa walio filiwa kulingana na kiwango chetu kilicho kubaliwa na wanachama.

2.MADHUMUNI

a) Kushughulikia na kupelekwa nyumbani maiti ya mwanachama au mtoto atakaefariki.

b) Kushughulikia miradi ya maendeleo.

c) Watoto ndugu au dada wanao mtegemea mwanachama walio zaidi ya miaka kumi na minane(18yrs)ambao wanasoma nilazima wajiandikishe chamani. Hakuna malipo yoyote yatakayo tolewa kwa mwanachama huyo akifariki chama kitachukua jukumu.

UANACHAMA

a) Kujiandikisha kuwa mwanachama ni wazi kwa kila mtaita /mtaveta, mwenye umri wa miaka kumi na minane na zaidi (18yrs and above)

b) Ada ya Kujiandikisha kuwa mwanachama ni ksh. 500.

c) Malipo ya mwezi ni ksh 250.

d) Mtu yeyote atakae jiunga na KWAELA WELFARE GROUP kuwa mwanachama baada ya usajili wake, basi mwanachama huyo atasubiri kwa muda wa miezi mitatu chini ya uangalizi(probation 3months) ndio iwapo amepatwa na msiba chama kiweze kumhudumia.

4.MAAFISA TEKELEZI.

a) Mwenyekiti.

b) Naibu mwenyekiti.

c) Mwandishi.

d)Naibu mwandishi.

e) Mweka hazina.

Maafisa hawa watakua ofisini kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe ya uchaguzi. Iwapo afisa ameshindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo, chama kina uwezo wa kumsimamisha na mwanachama mwengine kushikilia wadhfa huo hadi uchaguzi wa mwaka utakapofanywa.

SHERIA

Mwanachama atakae pitisha miezi sita(6 months) bila kulipa ada ya mwezi, basi atapoteza uanachama wake. Hata hivyo ataweza kukaribishwa tena chamani kwa Kujiandikisha upya na kulipa madeni yote ya zamani. Mwanachama huyo atakua kwa probation ya miezi mitatu (3months).

b) Mwanachama ni lazima kuhudhuria mikutano ya chama, iwapo atakosa nafasi ajieleze mapema kabla ya siku ya mkutano.

c) Mwanachama akikosa kuhudhuria mkutano atatozwa ada ya (200ksh).

d) Msiba utokeapo, chama kitatoa pesa kwa account kwa kiwango kilicho kubalika na mwanachama. Mwanachama kuendelea kuchamga ksh. 500 kila mmoja ili iregeshwe kwa account.

e) Chama kitashughulikia mwanachama, (Bibi/Bwana) watoto wake na wazazi wake.

f) Wakati wa msiba(matangani) hakuta jadiliwa mambo ya chama, maswali kutokana na madeni, yataulizwa na kujibiwa kwa mikutano.

g) Katiba na sheria za chama zinaweza kurekebishwa na theluthi moja ya idadi ya wanachama walio jiandikisha(1/3ya wanachama)

h) Chama hiki cha Welfare Group hakina uhusiano wowote na chama cha kisiasa.

i) Kila mwanachama atatoa mchango wake kuanzia mwezi ule chama kilipo anzishwa.

YALIO PITISHWA NA WANACHAMA. 

1. Pesa za kusafirisha maiti ni ksh 30,000.

2. Mtu anae jiunga upya na chama atakua chini ya uangalizi(probation) kwa miezi mitatu (3months)

3. Akipatwa na msiba akiwa chini ya uangalizi huu chama kitampa ksh. 5,000.

4.Viongozi walio maliza muhula na baada ya uchaguzi kufanywa wameregeshwa tena uongozini au wametolewa uongozini kupitia kura, chama kitawapatia wanachama hao ksh. 500 kila mmoja kama kiinua mgongo.

5. Viongozi wanao hudhuria mikutano kupewa ksh. 200 kwa kila kikao wanacho hudhuria.

6.Wanachama wawili kuhudhuria mazishi yanapotokea ili kuwakilisha chama.

7. Kila mwaka June kutakua na mchango mmoja kujazilia mfuko wa chama. Kila mwanachama kutoa mchango wa ksh. 1,000 pesa hizi zitaingia kwa miradi ya maendeleo.

8.Mwanachama akipoteza mtoto wake wa miezi sita(6 months) kurudi chini hadi siku moja chama kitampatia mwanachama huyo ksh. 10, 000 kama gharama za mazishi.

more recommended stories