Shirikisho la soka tawi la pwani FKF limetangaza kuandaa mashindano ya soka ikiwemo Chapa dimba na jamhuri Cup kaunti ya Taita Taveta kufwatia juhudi za serikali hiyo chini ya wizara ya michezo kukuza vipaji vya soka kupiku kaunti zingine 5 za pwani.
Mwenyekiti wake Gabriel Mghendi ameyasema haya wakati wa mchuano wa mechi ya fainali ya soka shindano la Governors Cup Taita Taveta kati ya timu ya Sagalla (Voi) na Mbale (wundanyi) na kuongeza kuwataja marefa wanaongoza mechi kaunti hiyo kama wanaohitaji mafunzo ya ziada ili kufikia viwango vinavyohitajika na shirikisho la soka ulimwenguni FIFA.
Katika pwani mzima kaunti hii inapeperusha bendera ya kuunga mkono sekta ya michezo kwa dhati na kwasababu vipaji vipo, tutahakikisha mwaka huu Chapa Dimba inatumika kutambua vipaji hapa Taita Taveta na kombe la Jamhuri cup awamu hii litaandaliwa kaunti hii. Tutalazimika kuleta wakufunzi wa marefa kutoka Fifa ili watoe mafunzo rasmi kwa marefa wa kaunti hii kwa sababu nimeona wangali hafifu. Mwenyekiti amesema.
Waziri wa vijana na michezo kaunti hiyo Bigvai Mwailemi amesema watandaa misururu ya michezo ikwemo vikapu, nyavu, soka miongoni mwa zingine ili kukuza vipaji vya vijana na kudokeza kuanzishwa mpango wa kutoa mafunzo maalum kwa vijana hao kuhusu uendeshaji biashara na kuwaomba wajisajili kwa makundi ili wafaidike na mipango ya serikali ikiwemo asilimia 30 ya zabuni zinazotolewa na serikali ya kaunti.
Timu ya sagalla imetwaa ubingwa wa mechi hiyo kwa kuwafunga wapinzani wake mabao 3 kwa 2. Mabao ya sagalla yakifungwa na wachezaji Musa Hussein (11), Joram Mwakichilu (18), James Kwida (85) nayo mabao ya Mbale yakifungwa na wachezaji Yawa Menza (30) kwa njia ya penalti na Wison Tayo (43) .
Kwa upande wa kina dada, timu ya Chala kutoka Taveta iliridhika na nafasi ya pili kwa kulazwa mabao 2 bila jawabu na wenzao wa Mbololo kutoka Voi mechi iliyochezwa uwanja wa Mwatunge, Mwatate.
Awali, gavana Granton Samboja alihudhuria mashindano ya mbio za Madoka Marathon awamu ya 13 na kuzindua rasmi mradi wa ujenzi kambi ya wanariadha inayotarajiwa kuongozwa na mkufunzi Daniel Kormen ambaye licha ya kustaafu kwake bado anashikilia rekodi ya mbio za masafa mafupi duniani.

“Tunataka vijana wa eneo hili mfanye mazoezi sana ili tuweze kushinda mbio za ulimwengu. Nitakua hapa mwaka ujao kuongoza kambi hiyo itakapokua tayari. Naomba mwanafunzi atakayeandikisha alama ya A kwa mtihani unaokuja wa KCSE munipatie nim tafutie ufadhili wa masomo ngambo.” Kormen amesema.
James Mwadime kutoka Taveta alishinda mbio za kilomita 10 kwa muda wa dakika 28 sekunde 42,Daniel Muindi alitumia muda wa saa limoja na dakika 6 kushinda mbio za Half marathon upande wa wanaume huku kitengo cha kina dada kikipeperushwa nae Delvin Relin aliyetumia lisaa limoja na dakika 16.
more recommended stories
LET US HONOUR OUR HISTORY: NAME THE VOI STADIUM AFTER MWANGEKA WA MALOWHA!As Taita Taveta prepares to receive.
VINDO SPORTS STADIUM NA SWALI LA MAJI TAITA TAVETAWakazi wa Kaunti ya Taita Taveta.
THE GREAT EAST AFRICAN MP SPORTS SAFARI — WHERE ATHLETICS MEETS PUBLIC FUND SQUANDERINGEast African MPs have once.
KERICHO SHOWS THE WAY: INSIDE THE KKK SUPER CUP CHANGING YOUTH LIVESWhen Aaron Cheruiyot launched the.
PRESIDENT RUTO’S TEARS STIR CONTROVERSY AMID GEN Z PAINWhile receiving Kenyan athletes from the.
YOUTH EMPOWERMENT IN TAITA-TAVETA COUNTY: A CALL TO ACTIONThe challenges facing young people.
KAYA TIWI RUN RIOT TO WIN GIRLS’ BASKETBALL CROWN AS DR. AGGREY RETAIN BASKETBALL BOYS’ TROPHY By Cedric Masindo It was a.
IT IS A BATTLE OF THE TITANS AS COAST REGIONAL GAMES ENTER DAY 2 IN MALINDITaita Taveta’s Dr. Aggrey and.
SHOWDOWN LOOMS AHEAD OF COAST REGIONAL GAMES IN MALINDIAll eyes are set on.
-
DR. AGGREY MAKES A RESOUNDING MESSAGE AS TAITA TAVETA COUNTY SCHOOL GAMES ENTER THE FINAL STAGE
By Cedric Masindo Former basket national.
TERM ONE GAMES IN TAITA AT THE DAWSON MWANYUMBA STADIUM – WUNDANYI.A great display of talent was.
TAITA TAVETA YOUTH DESERVE BETTERI find myself perplexed as.
THE SHAME OF A SEXIST COUNTY!By Tito Almasi On Sunday, Governor.
MWATATE UNITED YANG’ARA NYUMBANI BAADA YA KUINYUKA VIHIGA BULLETS MABAO 5 BILAMwatate united yang’ara nyumbani baada ya.
ON SUNDAY, I ATTENDED TTC CROSS COUNTRY CHAMPIONSHIPS AT DAWSON MWANYUMBA IN WUNDANYI.It was a terrible mistake. That.
TIMU YA TAVEVO FC INAYOSAMBAZA MAJI TAITA TAVETA YAPEPETWA 3-0 NA TIMU YA MAUNGU ALL STARS UWANJANI SGRHio Jana Wachezaji wa Timu.

Leave a Comment