Wafanyi biashara wengi wa Taveta wamepinga vikali uchaguzi uliofanyika leo, wakidai kuwa haukuwa halali na haukuwapa nafasi ya kushiriki kikamilifu.
Kwa mujibu wa wafanyi biashara hao, walipigiwa firimbi ya kuitwa kwenye uchaguzi jana bila kupewa muda wa kutosha kujiandaa. Wanasema hatua hii ililenga kuwapitisha viongozi waliopendekezwa na Ofisi ya Trade ya Kanjo badala ya wale wanaochaguliwa na wafanyi biashara wenyewe.
Malalamiko makubwa yanaelekezwa kwa maafisa wa Trade waliotajwa kama Moka na Aquilina, ambao wanadaiwa kuongoza mchakato huo kwa njia isiyo ya haki. Wafanyi biashara wanasema walinyimwa nafasi ya kuchagua viongozi wao, hususan nafasi ya mwenyekiti, ambapo walitaka kuchagua wao lakini badala yake majina yalipendekezwa moja kwa moja na maafisa wa Kanjo.
Hali hii imezua maswali miongoni mwa wafanyi biashara:
- Je, kamati ya soko ni ya wafanyi biashara au ni ya Kanjo?
- Kwa nini viongozi wanapendekezwa na maafisa badala ya kuchaguliwa na wanabiashara?
- Je, soko la Taveta ni la wafanyi biashara wote au la kikundi maalum?
Wafanyi biashara wanasisitiza kuwa soko ni mali ya wote, na si wachache au kundi fulani kama mama mboga pekee. Wanataka haki ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa viongozi wao.
Aidha, wameonya kuwa hawatakubali matokeo ya uchaguzi huo na wameitaka serikali ya kaunti kurudia mchakato huo kwa njia ya haki na uwazi. Vinginevyo, wameashiria kuwa wako tayari kuchukua hatua zaidi, ikiwemo maandamano.
“Soko ni la wafanyi biashara wote, sio wachache. Viongozi wawekwe na wafanyi biashara, sio kwa mifuko,” walisema kwa pamoja.
more recommended stories
TAITA TAVETA RANCHERS MUST THINK BEYOND GRAZING FEES AND BUILD WEALTH FOR FUTURE GENERATIONSAcross Taita Taveta County, a.
Relief for Guarantors as Qwetu DT SACCO Intensifies Recovery of Long-Standing Loan DefaultsThere is growing relief among.
TAITA TAVETA COUNTY GOVERNMENT, PLEASE PAY MY DUESHello Kwaela, My name is.
Kishushe Ranching Cooperative Society Limited at the Center of Kenya’s Mineral FutureKenya is steadily positioning itself.
INSIDE THE NAIROBI HOSPITAL CRISIS: BILLIONS MISSING, COURT ORDERS DEFIED, AND A 70-YEAR LEGACY ON THE BRINKNairobi | March 19, 2026 For.
THE INJUSTICES & ECONOMIC CONSEQUENCES IMPOSED ON VOI RESIDENTS BY SUBSEQUENT COUNTY ADMINISTRATIONSVoi Constituency is not a recent.
AFFORDABLE HOUSING OR STATE-BACKED REAL ESTATE? KENYANS DEMAND STRAIGHT ANSWERSAcross Kenya, the government’s Affordable Housing.
Quail Farming: A Quiet Agribusiness Opportunity Emerging in Taita TavetaBy Kwaela News Network – Taita.
PUBLIC DEMAND FOR TRANSPARENCY: TAVEVO, HOW DO YOU CALCULATE WATER BILLS?Residents across Taita Taveta County.
KENYA STRIKES GOLD: Will Kenyans Truly Benefit or Be Left Behind Again?KAKAMEGA, KENYA – A major gold.
ATHANAS MBELE AWASILISHA PETISHENI BUNGENI DHIDI YA KAMPUNI ZA MIKOPO ZINAZOWANYANYASA WAKAZI WA TAITA TAVETATaita Taveta, Kenya — Kiongozi.
STOP MISUSING POLYTECHNICS AS CONDUITS FOR FAKE BURSARIES BY ROGUE MCASThe Taita Taveta County Education.
FOUR LAW ENFORCEMENT OFFICERS ARRESTED OVER ILLEGAL ARMS TRADEDetectives from the Operations Support Unit.
RESIDENTS ALARMED AS TAITA TAVETA WATER BILLS OUTSOURCED TO ROGUE DEBT COLLECTORSThe Taita Taveta County Government, through.
TAITA TAVETA COUNTY REVENUE – WAKUJAA’S TURNAROUND STORYBy Geoffrey KIMONGE (GK) Critics.
RAFIKI IMARA HOLDINGS LIMITED TUNAOMBA HAKI YETUTulikuwa wateja wa kampuni.

Leave a Comment