Wananchi wa Kaunti ya Taita Taveta, hususan wakaazi wa Voi, wanalaani vikali na kwa masikitiko makubwa hali ya kusikitisha inayojitokeza katika Hospitali ya Rufaa ya Moi–Voi ambako kwa muda sasa kumekuwa na uhaba mkubwa wa madawa, vifaa tiba na mahitaji muhimu ya wagonjwa, ilhali wananchi wanaendelea kulipa michango yao ya huduma za afya (SHA) kama inavyotakiwa kisheria.
Ni jambo la kusikitisha na lisilokubalika kwamba:
- Wagonjwa waliolazwa wanawalazimika kununua dawa, sindano, gloves, drips na vifaa vingine kwa pesa zao binafsi.
- Wengine wanakwama kupata matibabu ya msingi kwa sababu hospitali “haina madawa.”
Hii yote inafanyika wakati serikali ya kaunti inapokea fedha za afya kutoka serikali kuu na michango ya wananchi.
TUNAKEMEA KWA NGUVU ZETU ZOTE
1. Utepetefu wa kiutendaji ndani ya idara ya afya ya kaunti.
2. Dalili za ufisadi na wizi wa rasilimali za umma, ambapo dawa na vifaa vinanunuliwa kwenye makaratasi lakini havifiki kwa wagonjwa.
3. Kutoajibika kwa uongozi wa afya wa kaunti, hasa:
- Waziri wa Afya wa Kaunti
- Kamati ya Afya ya Bunge la Kaunti
- Na uongozi mzima wa Sekta ya Afya
Uongozi huu umeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kikatiba wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya kwa heshima na usawa.
TUNATAKA UFAFANUZI WA HARAKA KUHUSU
- Fedha zote za SHA zilizopokelewa na hospitali kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
- Hatima ya bajeti ya ununuzi wa madawa na vifaa.
- Madeni ya kaunti kwa KEMSA na wasambazaji binafsi.
- Ni nani anayehusika na kuruhusu wagonjwa kununua vifaa ndani ya hospitali ya umma.
ONYO KWA SERIKALI YA KAUNTI
Afya ya wananchi si mradi wa kisiasa, si fursa ya wizi, wala si kitu cha kuchezewa. Maisha ya watu yako hatarini kila siku kutokana na uzembe huu.
Ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa mara moja:
Wananchi wako tayari kutumia njia zote halali za kikatiba kudai haki yao, ikiwemo maandamano ya amani, mashauri ya kisheria na kuhusisha taasisi za kitaifa za uchunguzi.
WITO
Tunaitaka Serikali ya Kaunti ya Taita Taveta, kupitia Wizara ya Afya na Kamati ya Afya ya Bunge la Kaunti, kutoa majibu ya wazi kwa umma ndani ya siku saba (7).
Tunazitaka pia taasisi za kitaifa za uangalizi wa fedha za umma kuchunguza matumizi ya rasilimali katika sekta ya afya ya kaunti hii.
Afya ni haki ya kikatiba. Hatuwezi kukubali tena vifo, mateso na aibu kwa sababu ya uzembe, ufisadi na tamaa ya viongozi wachache.
Imetolewa na Wananchi wa Voi – Kaunti ya Taita Taveta
Kupitia: Kwaela News Network
Tarehe: 27 Novemba, 2025
more recommended stories
SHOULD CATHOLIC PRIESTS BE ALLOWED TO MARRY?The Sandro Ferretto case has.
TAITA TAVETA INA MIRADI, LAKINI HAINA MAJIWapo wanaoamini kuwa miradi inayoendelea Taita.
OFFICIAL REBUTTAL AND CONDEMNATION OF THE APPROVAL OF MR. ALFRED MLOLWA AS COUNTY EXECUTIVE COMMITTEE MEMBER FOR HEALTH SERVICESStatement by Concerned Citizens of.
DOES TAITA TAVETA PRIORITIZE PROFESSIONAL EXPERTISE IN HEALTH LEADERSHIP?A quick comparison of leadership in.
I Was Fluent in DisappearingI was a girl who spoke Swahili and Luhya,.
GENDER-BASED VIOLENCE IN TAITA TAVETA COUNTY: A GROWING CRISISGender-based violence (GBV) in Taita Taveta.
WHERE THE CHURCH IS GETTING IT WRONG IN DEALING WITH POLITICIANSBy Pastor Cassian Ngotho Mwachanya There.
MBELE URGED TO RELEASE MASTER PLAN FOR WUNDANYI KMTCAthanas Mbele Challenged to Release Master.
OUR COMMUNITY MUST TALK: GROWING SUICIDE CASES RAISE ALARMBy Christopher Mwachia, Ward Administrator.
BURIALS IN TAITA TAVETA HAVE BEEN REDUCED TO POLITICAL SLAUGHTERHOUSES.It is both heartbreaking and infuriating.
MAJOR HEALTH BOOST PROPOSED FOR VOI, EVEN AS TRUST DEFICIT CHALLENGES LOOMThe Taita Taveta County Government, under.
DRUGS, ILLICIT BREWS, AND THE DEADLY GAMES THE STATE IS PLAYING WITH KENYAN LIVESBy Kwaela News Network | Special.
CALLS GROW FOR TRADITIONAL BURIAL RITES FOLLOWING DEATH OF CYRUS JIRONGOSections of the Luhya community have.
SUMMARY EXPOSÉ: EMERGING CONCERNS ON THE MANAGEMENT OF TAITA TAVETA COUNTY HEALTH DEPARTMENTA recent internal communication originating from.
SAFETY CONCERNS IN ONGOING RURAL ELECTRIFICATION IN TAVETA CONSTITUENCY⚠️ PUBLIC AWARENESS STATEMENT ⚠️ We.
WATER CRISIS HITS MOI COUNTY REFERRAL HOSPITAL Patients Forced to Bring Own.

Leave a Comment