Ni miaka mitatu sasa tangu aanze safari ya kuongoza Taita Taveta. Tumebakiwa na mwaka mmoja tu kabla ya kampeni kuanza rasmi. Katika kipindi hiki—kisiasa, kiuchumi na kijamii—wananchi wana haki kuuliza:
1. Je, ni lipi kubwa alilofanya katika kuinua maisha ya mwana DaTu wa kawaida?
Mwananchi wa kawaida bado anangoja majibu kuhusu mabadiliko yanayoguswa na mkono wake moja kwa moja:
- Afya bora na inayopatikana kirahisi
- Elimu iliyoimarishwa
- Ajira kwa vijana
- Miundombinu inayorahisisha uchumi wa kaya
Hadi sasa, wananchi wanahitaji kuona matokeo yanayojitokeza bila propaganda, bila takwimu za kipeperushi—matokeo yanayoonekana kwa macho.
2. Ni mradi upi maalum, uliozinduliwa na serikali yake, umefadhiliwa kikamilifu na kaunti na unaendelea ipasavyo?
Wananchi wanahoji: mbali na kutembelea, kuzindua upya au kufungua miradi ya serikali za nyuma, ni ipi aliyoianzisha yeye, kutoka msingi hadi utekelezaji?
Hili ndilo swali linaloendelea kuwasha mijadala mashinani.
3. Wizara ya Elimu: je, ameifanya vizuri zaidi ya waliomtangulia?
- Katika kaunti ambapo:
- Madarasa mengi bado yana vifaa pungufu,
- Wazazi wengi wanahangaika na karo,
- Walimu wa ECDE mara nyingi hukosa motisha na vifaa,
Wananchi wanasubiri kuona ikiwa utawala wa sasa umeleta mageuzi yoyote ya kutajika—sio tu matangazo, bali matokeo.
4. Hali ya Afya imeimarika vipi?
Mbali na Eye Center na Cancer Center—ambazo zinafadhiliwa na wafadhili—wananchi wanataka kufahamu:
- Ni hospitali ipi mpya au vituo vya afya vilivyokarabatiwa au kujengwa kwa fedha za kaunti?
- Je, vituo vya afya mashinani bado vina upungufu wa dawa?
- Je, rasilimali watu wa afya wanahudumiwa ipasavyo?
Afya ndiyo kipimo kikuu cha utawala. Wananchi wanangoja majibu.

5. Miundombinu: barabara, madaraja, na ukarabati — nini kimeanzishwa tangu aapishwe?
Wakati uchumi wa Taita Taveta unategemea sana:
- Usafirishaji wa mazao,
- Utalii,
- Na biashara ndogo ndogo,
Barabara ni uti wa mgongo. Swali bado: ni lipi jipya lililoanzishwa chini ya uongozi wake?
6. Je, alikamilisha miradi iliyokwama kama alivyoahidi wakati wa kampeni?
Ahadi yake kuu ilikuwa:
▶️ “Kwanza nitamalizia miradi iliyokwama kabla sijazindua mipya.”
Wananchi wanahoji:
- Ni miradi ipi imekamilishwa?
- Iliisha lini?
- Na kwa kiwango gani imekuwa na manufaa kwa wananchi?
7. Vita dhidi ya Ufisadi: kuna hatua ya kweli iliyopigwa?
Katika kaunti yenye historia ya ufujaji wa fedha, wananchi wanatarajia hatua halisi kama:
- Ukaguzi wa matumizi ya fedha,
- Kuchukuliwa hatua kwa maafisa wafisadi na waliogushi vyeti kupata ajira.
- Uwajibikaji wa wazi katika zabuni na tenda,
- Ripoti za matumizi zinazosomwa hadharani.
Hadi sasa, wananchi wanajiuliza: kuna mabadiliko ya kweli au ni maneno matamu tu?
Je, Taita Taveta inajivunia kuwa na #Wakujaa kama Gavana — AU inavumilia kuwa na #Wakutoa?
Kwa mwaka mmoja uliosalia kabla ya kampeni kuanza, maswali haya si ya kisiasa—ni madai ya uwajibikaji kutoka kwa wananchi wanaohitaji uongozi wa matendo, sio wa kauli tu.
more recommended stories
TAITA TAVETA: WE CANNOT CONTINUE THIS WAY — A COUNTY GOVERNMENT IN CRISIS OF ACCOUNTABILITYKwaela News Network | Editorial Taita.
DOCUMENT REVIEW: TAITA TAVETA COUNTY CIDP III (2023–2027)A Review of Planned Development Priorities,.
COVID-19 FUNDS IN TAITA TAVETA: YEARS AFTER THE AUDIT, WHO ANSWERED THE QUESTIONS — AND WHO WAS HELD ACCOUNTABLE?As High Court reduces Rodger Ngoo’s.
RUTO’S TAITA TAVETA TOUR: DEVELOPMENT INSPECTION OR PROMISE DELIVERY MISSION?President William Ruto is expected to.
VOI THIRSTS AS LEADERS TRADE STATEMENTS, EXCUSES AND BLAMEYears of promises, unpaid.
MRUGHUA SOCIAL HALL: A DECADE OF WAITING, MILLIONS SPENT, AND STILL NO ANSWERSTen Years Later, Why Is.
SIX-YEAR DEFAMATION CASE ENDS AS COURT AWARDS COSTS TO KWAELA NEWS NETWORK, BUT QUESTIONS OVER COVID-19 FUNDS REMAINVOI, TAITA TAVETA — A six-year.
Family, Power and Public Trust: The Questions Governor Wakujaa Must AnswerThe latest appointments in Taita Taveta.
PETITIONERS FAIL TO PROVE OWNERSHIP OF 1,306 HECTARES AS COURT DISMISSES NDARA B LAND CASECase: Gadiel Mnyambo Mwaisama & Others.
NJORO KUBWA OR MZIMA PHASE II? WEIGHING TAITA TAVETA’S BIG WATER OPTIONSWater has long been one.
WHY KENYANS ARE TURNING AGAINST SAFARICOM OVER SURVEILLANCE FEARSFor years, Safaricom has enjoyed enormous.
FIRES, FEAR AND FAILURE: THE HARD QUESTIONS TAITA TAVETA SCHOOLS MUST ANSWERA disturbing pattern is emerging in.
PARIS JUU YA MACHOZI YETU: AIBU YA VIONGOZI WALIOSAHAU WATU WAOKatika wakati ambapo wananchi wa.
ISANGAIWISHI DEVELOPMENT COMMUNITY OFFICIAL STATEMENT ON LAND OWNERSHIP, HISTORICAL RECORD, AND DEVELOPMENT1. Introduction The Isangaiwishi Development Community.
AUDIT SHOCKER: HUNDREDS OF MILLIONS IN WORKERS’ DEDUCTIONS UNACCOUNTED FOR AS FINANCE SHAKE UP ROCKS TAITA TAVETABy Kwaela News Network Investigations Desk.
COURT EXPOSES ILLEGAL IMPEACHMENT: TAITA TAVETA COUNTY ASSEMBLY FAULTED FOR RUSHED, UNCONSTITUTIONAL REMOVAL OF SPEAKER MWAMBURIMombasa, Kenya — In a damning.

1 Comment on this post
Leave a Comment