WAFANYAKAZI WA KAUNTI WALIA KWA KUTENDEWA TOFAUTI KATIKA BIMA YA AFYA

 

Kwaela News Network – Taita Taveta | Oktoba 7, 2025

Wafanyakazi wa Serikali ya Kaunti ya Taita Taveta wameeleza masikitiko yao kuhusu mfumo wa bima ya afya unaowagawa katika makundi mawili, hali wanayodai ni ya ubaguzi wa wazi kazini.

Kwa mujibu wa mfumo huo:

– Wafanyakazi wa job group A hadi J wanasimamiwa na Jubilee Insurance, inayotoa huduma za:

1. Matibabu ya kawaida na ya kitaalamu

2. Huduma ya macho (optical)

– Wafanyakazi wa job group K na kuendelea juu wanasimamiwa na AAR Insurance, inayotoa:

1. Matibabu ya kawaida na ya kitaalamu

2. Huduma ya macho (optical)

3. Huduma ya meno (dental)

Wafanyakazi hao wanasema huu ni ubaguzi ulio wazi, kwani huduma ya afya ni haki ya msingi na haipaswi kutolewa kwa upendeleo kulingana na cheo au nafasi ya mtu kazini.

“Wakati wa kampeni, gavana alituahidi usawa kazini. Lakini sasa tunaonekana kama watoto wa tumbo na wengine wa mgongoni,” alisema mfanyakazi mmoja aliyeomba jina lake libanwe.

Wanaendelea kuuliza:

– Je, haki ya matibabu bora ni kwa wachache au kwa wote?

– Je, wakati wa uchaguzi, wale waliotengwa watapiga kura nusu?

Kwaela News Network inatoa wito kwa ofisi ya gavana *Mwadime* kuangazia upya suala hili, ili kuhakikisha kila mfanyakazi anapata huduma sawa bila ubaguzi.

Kwaela News – Ola Kwalangala!

more recommended stories