WITO WA UWAZI KUHUSU MATUMIZI YA KSH 78 MILIONI KATIKA WODI ZA TAITA TAVETA

 

Taita Taveta, 29 Septemba 2025 — Wito umetolewa kwa Waziri wa Ujenzi, Arch. Martin Tairo Maseghe, kutoa taarifa rasmi na za kina kuhusu matumizi ya KSh 78 milioni zilizotengwa kwa miradi ya maendeleo katika wodi zote ishirini za Kaunti ya Taita Taveta.

Haya yameibuka kufuatia mjadala unaoendelea mitandaoni kuhusu usambazaji na utekelezaji wa miradi inayodaiwa kufadhiliwa kwa fedha hizo. Wananchi na wadau mbalimbali wameonyesha shauku ya kujua iwapo kweli fedha hizo ziligawiwa kwa usawa, na kama miradi iliyopangwa imetekelezwa kwa ufanisi.

Waziri Maseghe anahimizwa kufafanua:

  • Orodha ya miradi iliyotekelezwa kwa kila wodi.
  • Gharama halisi ya kila mradi.
  • Vigezo vilivyotumika katika ugawaji wa fedha hizo.

Aidha, Waheshimiwa MCA wanaombwa kuidhinisha hadharani kuwa miradi hiyo ipo, na kazi imefanyika kama ilivyokusudiwa.

“Ni muhimu kwa viongozi wetu kuhakikisha kuwa kuna uwazi na uwajibikaji, hasa katika matumizi ya rasilimali za umma. Ukimya wa viongozi husika unaweza kuendelea kuibua maswali na hisia kali miongoni mwa wananchi,” alisema mmoja wa wachangiaji wa hoja hiyo.

Iwapo hakutakuwa na maelezo ya wazi katika muda wa karibu, kuna mpango wa kuchapisha orodha ya madai yanayoendelea kusambaa kuhusu matumizi ya fedha hizo kwa nia ya kuhamasisha uchunguzi na usahihi wa taarifa.

Concerned Datuzen

 

more recommended stories