Na Mkereketwa Mashinani

Nduru za kuaminika zimasema kuwa magaidi na wasulubu /miungu ya kaunti waliojitweka majukumu ya tume ya uwajiri katika kaunti ya Taita Taveta, wako na njama fiche ya kuwafuta au kuwasimamisha kazi watawala wodi mheshimiwa Topista Lenjo – Mbololo, Mheshimiwa Charles Mwadeghu – Marungu, mheshimiwa Stanley Makeo – Sagalla na Mheshimiwa Martin Madaraka – Kaloleni Wodi. Inasemekana kuwa tayari wameanzaa kutafuta watu watakaochukua nyadhifa zao. Baadhi ya walioombwa kujaza mapengo yatakayowachwa wazi baada ya wannene hawa kufurushwa wamezikataa nafasi hizo, wakihofiwa kufutwa kiholela endapo hawataafikia matakwa ya waajiri hawawalio na nia fiche.
Watawala wodi wa Ngolia mheshimiwa Dawson Mwanyumba na wa Kasigau mheshimiwa Pastor Mwasi pia walipangiwa njama hiyo hiyo ya kuachishwa kazi hapo awali na kusazwa kwa kuzingatia umri wao kando na misimamo yao ya kisiasa.
Vyanzo vya kutaka kufutwa kwao visivyo na misingi ni kama ifwatavyo:-
Kuwa Voi imemkataa kusimama na mfalme gavana kwa harakati zake za kutaka kuchaguliwa tena 2022 kwa awamu ya pili, kwa hiyo suluhu ikawa kuwatoa mhanga kama wana Voi kwa kutoshawishi wananchi wa sehemu hiyo kumuunga mkono na kumdhabikia mfalme kwa awamu yake ya pili.
Pili ni kuwa wamekuwa na misimamo mikali na kushurutisha idara mbali mbali kujukumika, kufanya kazi na kuwacha utepetevu kwani wananchi wanahitaji huduma kama watozwa ushuru na waajiri.
Nne, kuwa walikataa kufanya majukumu ya kisiasa kama watu binafsi na kusisitiza kusimama na majukumu yao ya kikatiba na ofisi, kama ilivyoangaziwa kwa mikataba ya kazi.

Tano, kuwa wamekuwa mistari ya mbele kupinga dhulma dhidhi ya wafanyikazi wenzao na kulalama kuhusu utenda kazi duni na ulaghai dhidi ya wandani wa mfalme wanaochuma pakubwa bila kuwajibika.
Sita, kuwa wamekuwa tishio mashinani kwa kujitolea kuhudumia wananchi kando na mazingira magumu na nyota zao kung’aa na kukusudiwa kupendekezwa kwa nyadhfa za juu zikiweno naibu gavana, washauri na hata wawakilishi wodi.
Saba, kuwa wamekua mistari ya mbele kutetea haki zao ka kimsingi na kazi ikiwemo maswala ya usafiri mashinani, gharama na marupurupu ya kazi, mshahara duni ikizingatiwa watawala wodi wa Taita Taveta ndio wanaolipwa mshahara duni zao di nchini.
Nane, kuwa wamekuwa wakikataa kutumiwa vibaya kidiasa dhidhi ya wapinzani wa mfalme na kuzingatia demokrasia na umoja wa wananchi.
Tisa, kwa kuwa mistari ya mbele, kuhusisha, kuhamasisha na kujuza wananchi maswala mbali mbali yanayohusu kaunti kama haki yao, ambapo kwa mfalme na wasulubu ni jambo la hatia na kinyume na matarajio.
Kumi, kuwa mawekuwa mistari ya mbele kukejeli dhulma zinazoendelea katika kaunti ya Taita Taveta, ambapo wafanyikazi haswa vijana wenzao wanafutwa kazi kwa njia zisizo za kisheria na kibinadamu.
Kumi na moja, kujukumisha na kushurutisha mawaziri na idara husika kufanya kazi na kutoa huduma kwa wananchi inavyostahili na kuwacha kula bata kwa gharama ya walipa ushuru.
Kumi na mbili, kutetea wafanyikazi wapewe mazingira bora na motisha ikiwemo kuajiriwa permanent kama ilivyoshurutishwa na serikali kuu kando na kucheleweshwa kwa mishahara.
Kumu na mbili, kushauri wangwana kuwacha kupora mali ya umma na kujigamba na kuweka maswala ya wananchi mbele yakiwemo afya, elimu, maji, kilimo, uzalishaji na kuwezesha wanabiashara wanaohisi kugandamizwa kama ilivyonykuliwa kwa Manifesto ya mfalme.
Kumi na tatu, kwa kuwa na misimamo tofauti ya vyama vya kisiasa kando na msimamo wa mfalme.

Masikitiko nikuwa lipo bunge la kaunti ambalo ni macho na sauti ya kaunti na wananchi ila liko kimnya wakati maovu na dhulma zinazokithiri hadharani, huku wakila mishahara na marupurupu bila kukemea uovu unaoendelea.
Kinaya Cha Uongozi Wa Mfalme Alieuchi ni kuwa wale wanaofanyia kazi kwa bidii na mazingira magumu ndo wanaoteswa, kutengwa na hata kufutwa kazi, ila wale wasiofanya lolote la maana ila kukaa maofisi wakinywa chai na kupora mali za umma ndio waliohuru na nguvu ya kusaliti wa kusulubu wengine.
Hali hii inapaswa kurekebishwa mapema sana na wana DaTu wote wanastahili haki zao. Kuanzia kwa wafanyikazi hadi kwa raia.
Tunatumahi mfalme atasoma ujumbe huu na arekebishe mambo kabla kitoweo kiingie mchanga.
Tuzidi kumuombea afya njema hasa kipindi hiki kigumu cha kisiasa.

more recommended stories
TAVEVO: THE GRAND WATER SCAM DRAINING TAITA TAVETA COUNTY DRY?Before demanding more water from.
USAWA NI SAWA: A PRINCIPLE THAT MUST TRANSCEND NATIONAL AND COUNTY POLITICSPicture a grand tapestry, woven with.
KAUNTI YA TAITA TAVETA ITAKWISHA KAMA HUU UONGOZI UTAENDELEA BAADA YA UCHAGUZI WA 2027Taita Taveta imebarikiwa kwa utajiri wa.
THE CROSSROADS OF TAITA-TAVETA: CHOOSING THE NEXT PATHFor decades, the conversation surrounding leadership.
KSh600 FOR A WHOLE DAY: HOW TAITA TAVETA’S “BODA BODA CROWD” MAY HAVE TURNED RUTO’S TOUR INTO A POLITICAL PHOTO SHOOTThere is a rather amusing —.
2027 BEGINS EARLY: THE MWANGOLO-BWIRE RIVALRY EXPOSES A GENERATIONAL DIVIDEThe political war between Principal Secretary.
THE ODM-UDA COALITION: A MARRIAGE OF CONVENIENCE, NOT CONVICTIONWhen the Orange Democratic Movement and.
LEGAL OPINION EXPOSES IRREGULAR COUNTY APPOINTMENT: QUESTIONS MOUNT FOR GOVERNOR WAKUJAA’S ADMINISTRATIONFresh questions are emerging over governance.
GOVERNORS NEED STRONG ASSEMBLIES, NOT CHEERLEADERSMy elder sister, Hon. Dorcas.
BEI YA MAFUTA, UBORA WA BARABARA NA GHARAMA HALISI YA KUENDESHA UCHUMI WA TAITA TAVETAMAONI Malalamiko ya wananchi kuhusu.
THE ART OF POLITICAL PARASITISMThere comes a point when.
Professional Analysis of the Taita Taveta FY 2025/2026 Supplementary II BudgetExecutive Summary The County Government of.
WHY MOMBASA DESERVES MZIMA WATER OVER COSTLY DESALINATION EXPERIMENTSAs Mombasa continues to grapple with.
UNDERSTANDING THE REALITY: WHY SALARY DELAYS ARE NOT GOVERNOR WAKUJAA’S FAILUREThere has been a lot of.
LET’S SET THE RECORD STRAIGHT ON TAITA TAVETA SALARIES & GOVERNOR WAKUJAAThere has been a wave of.
The Mouse, The Cat, and the Glass Jar Politics of Taita TavetaIn village folklore, they say wisdom.

Leave a Comment