Categories: *Featured News

TANGU GAVANA WAKUJAA AWEKE BIBILIA CHINI …

 

Ni miaka mitatu sasa tangu aanze safari ya kuongoza Taita Taveta. Tumebakiwa na mwaka mmoja tu kabla ya kampeni kuanza rasmi. Katika kipindi hiki—kisiasa, kiuchumi na kijamii—wananchi wana haki kuuliza:

1. Je, ni lipi kubwa alilofanya katika kuinua maisha ya mwana DaTu wa kawaida?

Mwananchi wa kawaida bado anangoja majibu kuhusu mabadiliko yanayoguswa na mkono wake moja kwa moja:

  • Afya bora na inayopatikana kirahisi
  • Elimu iliyoimarishwa
  • Ajira kwa vijana
  • Miundombinu inayorahisisha uchumi wa kaya

Hadi sasa, wananchi wanahitaji kuona matokeo yanayojitokeza bila propaganda, bila takwimu za kipeperushi—matokeo yanayoonekana kwa macho.

2. Ni mradi upi maalum, uliozinduliwa na serikali yake, umefadhiliwa kikamilifu na kaunti na unaendelea ipasavyo?

Wananchi wanahoji: mbali na kutembelea, kuzindua upya au kufungua miradi ya serikali za nyuma, ni ipi aliyoianzisha yeye, kutoka msingi hadi utekelezaji?

Hili ndilo swali linaloendelea kuwasha mijadala mashinani.

3. Wizara ya Elimu: je, ameifanya vizuri zaidi ya waliomtangulia?

  • Katika kaunti ambapo:
  • Madarasa mengi bado yana vifaa pungufu,
  • Wazazi wengi wanahangaika na karo,
  • Walimu wa ECDE mara nyingi hukosa motisha na vifaa,

Wananchi wanasubiri kuona ikiwa utawala wa sasa umeleta mageuzi yoyote ya kutajika—sio tu matangazo, bali matokeo.

4. Hali ya Afya imeimarika vipi?

Mbali na Eye Center na Cancer Center—ambazo zinafadhiliwa na wafadhili—wananchi wanataka kufahamu:

  • Ni hospitali ipi mpya au vituo vya afya vilivyokarabatiwa au kujengwa kwa fedha za kaunti?
  • Je, vituo vya afya mashinani bado vina upungufu wa dawa?
  • Je, rasilimali watu wa afya wanahudumiwa ipasavyo?

Afya ndiyo kipimo kikuu cha utawala. Wananchi wanangoja majibu.

5. Miundombinu: barabara, madaraja, na ukarabati — nini kimeanzishwa tangu aapishwe?

Wakati uchumi wa Taita Taveta unategemea sana:

  • Usafirishaji wa mazao,
  • Utalii,
  • Na biashara ndogo ndogo,

Barabara ni uti wa mgongo. Swali bado: ni lipi jipya lililoanzishwa chini ya uongozi wake?

6. Je, alikamilisha miradi iliyokwama kama alivyoahidi wakati wa kampeni?

Ahadi yake kuu ilikuwa:

▶️ “Kwanza nitamalizia miradi iliyokwama kabla sijazindua mipya.”

Wananchi wanahoji:

  • Ni miradi ipi imekamilishwa?
  • Iliisha lini?
  • Na kwa kiwango gani imekuwa na manufaa kwa wananchi?

7. Vita dhidi ya Ufisadi: kuna hatua ya kweli iliyopigwa?

Katika kaunti yenye historia ya ufujaji wa fedha, wananchi wanatarajia hatua halisi kama:

  • Ukaguzi wa matumizi ya fedha,
  • Kuchukuliwa hatua kwa maafisa wafisadi na waliogushi vyeti kupata ajira.
  • Uwajibikaji wa wazi katika zabuni na tenda,
  • Ripoti za matumizi zinazosomwa hadharani.

Hadi sasa, wananchi wanajiuliza: kuna mabadiliko ya kweli au ni maneno matamu tu?

Je, Taita Taveta inajivunia kuwa na #Wakujaa kama Gavana — AU inavumilia kuwa na #Wakutoa?

Kwa mwaka mmoja uliosalia kabla ya kampeni kuanza, maswali haya si ya kisiasa—ni madai ya uwajibikaji kutoka kwa wananchi wanaohitaji uongozi wa matendo, sio wa kauli tu.

 

 

Kwaela News Network

Leave a Comment

View Comments

Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

16 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

5 days ago