Categories: Taita Taveta News

MADAI YAIBUKA RAILA ALIZINDUA MRADI HEWA TAITA

 

NA LUCY MKANYIKA

MIZOZO na madai ya ufisadi yameibuka katika mradi wa maji uliozinduliwa na kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, katika Kaunti ya Taita Taveta wiki iliyopita.

Baadhi ya viongozi wa kijamii na wakazi wametoa wito uchunguzi ufanywe ili kubaini kama serikali ya kaunti hiyo ilitumia vyema pesa zilizonuiwa kutekeleza mradi huo.

Wakati Bw Odinga alipoongoza uzinduzi huo mnamo Ijumaa iliyopita, baadhi yao walieleza wazi kutoridhishwa kwao mbele yake.

Walidai kuwa serikali ya kaunti hiyo ilipeleka malori kujaza maji kwa mapipa katika hila hiyo ilhali mradi wenyewe hausambazi maji kutoka kwa chemchemi ilivyonuiwa.

Hata hivyo, Waziri wa Maji katika Kaunti, Bi Esther Mwanyumba, amepuuza madai kuwa pesa za mradi huo zilifujwa na kwamba malori yalitumiwa kujaza maji ili kumhadaa Bw Odinga kuuzindua.

“Kuna kazi nyingi zilizofanywa hapa na wale wanaodai pesa zilifujwa wanadanganya. Hata mkandarasi alifanya kazi zaidi ya zile alizopewa kwa kandarasi hiyo,” akasema.

Kuhusu malori ya maji yaliyoonekana hapo kabla ya mradi huo kuzinduliwa, alieleza kuwa hayakunuiwa kujaza mapipa hayo ya maji ya lita milioni 2.1 zilizopo.

“Tulitumia wiki sita kujaza maji kwa matangi hayo. Maji yalipitia kwa mabomba kutoka kwa chemchemi na kisimani. Malori yaliyokuwa hapa yalikuwa yanatumiwa kunyunyiza maji barabarani na katika uwanja ambapo hafla ya uzinduzi iliandaliwa,” akaeleza.

Kulingana naye, bomba la maji la urefu wa kilomita 18 litakuwa likipeleka maji kila wakati hadi katika matangi hayo, akahakikishia wakazi wa eneo la Mwaktau kwamba changamoto za uhaba wa maji zimetatuliwa.

Alidai kuwa wakazi waliopiga kelele wakati wa uzinduzi walikuwa wamepelekwa hapo na mahasimu wa kisiasa wa gavana wa kaunti hiyo, Granton Samboja. Bw Samboja na Mbunge wa Mwatate, Bw Andrew Mwadime, wamekuwa wakizozana kuhusu afisi iliyohusika kufanikisha mradi huo wa maji wa Nangoro ambao umegharimu Sh88 milioni.

Mradi huo umenuiwa kusaidia zaidi ya wakazi 17,000 wanaoishi katika vijiji 14 vya maeneo ya Godoma na Mwaktau.

Bw Mwadime alidai gavana huyo anajizolea sifa ilhali ni yeye ndiye aliyetafuta ufadhili kutoka kwa serikali ya kitaifa.

“Hawakutaja hata mchango wangu katika kutafuta ufadhili. Mimi ndiye niliyeshinikiza serikali ya kitaifa isaidie wakazi,” akasema.

Mbunge huyo aliyesimamia eneobunge la Mwatate tangu 2013, analenga kushindania tikiti ya ODM kuwania ugavana, huku Bw Samboja pia akitarajiwa kuhamia ODM kutoka Wiper kuwania wadhifa huo kwa awamu ya pili.

Mbunge huyo aliungana na wale wanaotaka uchunguzi ufanywe kuhusu mradi huo.

“Inavyoonekana, kazi iliyofanywa hapa hailingani na kiasi cha pesa kilichotumiwa,” akadai.

Viongozi wengine walioomba wasitajwe gazetini walisema watafuatilia malalamishi hayo ya wakazi na viongozi wenzao ili wabainishe jinsi fedha zilivyotumiwa.

“Tunataka tusubiri hadi tutakapojibiwa kuhusu haya masuala yaliyoibuka ndipo tutatoa maoni yetu. Kuna mipango ya kuanzisha uchunguzi,” akasema mmoja wao.

Licha ya hayo, baadhi ya wakazi wana matumaini kwamba mradi huo utatatua uhaba wa maji ambao umewakumba kwa muda mrefu.

~ Taifa Leo

Kwaela News Network

Leave a Comment
Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

18 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago