Mheshimiwa Naibu Gavana, Bi Christine Kilalo, Waheshimiwa Wabunge katika bunge la Taifa na bunge la Seneti, Mheshimiwa Spika wa Bunge la Kaunti ya Taita Taveta, Waheshimiwa Wabunge katika Bunge la Kaunti ya Taita Taveta,
Kamishina wa Kaunti ya Taita Taveta pamoja na Maafisa wengine wa Serikali Kuu, Mwenyekiti na wanaBodi wa Bodi ya Utumishi wa Umma, ya Kaunti ya Taita Taveta, Waheshimiwa mawaziri wa Serikali ya Kaunti ya Taita Taveta, washauri wangu, na wafanyi kazi wote wa Serikali ya Taita Taveta,
Wageni waalikwa,
Na wananchi watukufu wa Taita Taveta, Ni furaha yangu kubwa, kujumuika nanyi siku hii muhimu katika historia ya taifa letu tukufu. Leo hii tunasherehekea mwaka wa sitini tangu tulipojinyakulia Uhuru kutoka kwa minyororo ya Mkoloni.
Ikumbukwe ya kwamba, Uhuru huu hatukuupata kwa njia rahisi : Mashujaa wengi walitulipia kwa damu na Maisha yao, na wengine wengi kuteswa na kufungwa gerezani na Wabeberu. Ni wajibu wetu kuulinda Uhuru huu kwa kuwakumbuka Mashujaa hao, na kujitolea kujenga Kenya yetu tukufu kwa mioyo, na nguvu zetu zote.
Mabibi na Mabwana
Nawaombeni nianze kwa kumshukuru Mwenyezi
Mungu kwa kutuwezesha kuiona siku hii.
Pili, napenda kutoa pole zangu kwa Wahanga na
Waasiriwa wote wa janga la mafuriko, ambalo
limetokana na mvua kubwa ambayo inaendelea
hadi sasa. Serikali yangu, ikishirikiana na Serikali
Kuu, Mashirika ya wahisani, kama vile Msalaba
Mwekundu, pamoja na Wahisani wa kibinafsi,
imejitolea kuhakikisha ya kwamba waasirika wote
wamepata msaada wa kuwawezesha kurudia
maisha yao ya kawaida, haraka iwezekanavyo.
Natoa kongole zangu kwa wote wale waliojitolea kwa hali na mali, kuwasaidia ndugu zetu walioathirika.
Ningependa, vile vile, kuwashukuru Wananchi wote wa Taita Taveta kwa ushirikiano mlionipa mimi, pamoja na Serikali yangu. Naahidi kuendelea kuwatumikia kwa moyo wangu wote.
Wananchi wa Taita Taveta, Kwa kipindi hiki cha miezi kumi na sita tangu Serikali yangu kuchukua hatamu za utawala, tumefanikiwa kupata maendeleo mengi, licha ya changamoto ambazo tunaendelea kukumbana nazo.
Katika kitengo cha afya, Tumeweza kumaliza deni la takriban milioni 89, tulilolikuta, la Shirika la Madawa la KEMSA. Na Vile vile, tumelipa deni la Shirika la MEDS. Hali hii imetuwezesha kuanza tena kupata madawa na vifaa vya huduma za afya. Serikali yangu pia imeweza kuongeza vifaa
vyengine vinne vya usafishaji damu (dialysis). Kwa ushirikiano na wafadhili, tumeweza kujenga Kliniki ya kuhudumia wagojwa wa UKIMWI na Kifua Kikuu, na pia kumalizia ujenzi wa kituo cha kisasa cha kuhudumia wagojwa wa maradhi ya macho. Ujenzi wa Cancer Centre, vile vile, umekaribia kukamilika.
Serikali yangu pia, imeweza kushirikiana na
Wildlife Works katika ukarabati na uboreshaji wa
Kajire Dispensary, huko Sagala. Kwa ushirikiano na shirika la Safaricom Foundation, tumeweza kupata vifaa vya Afya ya
uzazi, katika hospitali ya Wesu na zahanati za
Ghazi na Werugha. Katika hospitali yetu kuu ya rufaa ya Moi, serikali yangu imeweza kukarabati na kuweka vifaa katika
kitengo cha shughulikia Ajali na Dharura za
kiafya.
Mabibi na Mabwana
Katika sekta ya Elimu, Napenda kusema
kwamba kwa mwaka wa fedha uliopita, kutokana
na ushirikiano mzuri kati ya Serikali yangu, na
Bunge letu la Jimbo (County Assembly), tuliweza
kupeana bursaries za kiwango cha shillingi Millioni mia moja kwa shule za upili, vyuo vikuu na vyuo vya ufundi, na kulipia scholarship kwa wanafunzi wanao funzwa na serikali yangu, na kumalizia malimbikizi ya ada zote walizokua wakidaiwa, kando na fedha tulizowekeza katika
mikopo ya elimu ya juu.
Kwa mwaka huu mpya wa kifedha, naahidi
kuwekeza millioni mia mbili katika bursaries, na
tutaendelea kusomesha wana funzi kupitia
scholarships za Kaunti. Isitoshe – naahidi kwamba
msaada huu kwa Watoto wetu utaendelea kupeanwa kwa njia ya uwazi na haki, kama vile
ilivyofanyika mwaka huu.
Wananchi wenzangu, ni wazi ya kwamba walimu ni nguzo muhimu katika sekta ya Elimu, na kwa kuweka msingi thabiti katika maisha ya baadaye ya Watoto wetu. Kwa kujali maslahi ya walimu wetu, na kama njia ya kuwashukuru kwa kazi yao
muhimu, niliamua kuwaweka walimu wote katika mpango uajiri wa kudumu, yani Permanent and Pensionable.
Napenda pia, kushukuru mashirika kama GIZ, Stanbic Foundation na wadau wengine, kupitia kwa vyuo vyetu vya fundi, kwa kuhakikisha vijana wa kaunti hii wanapata elimu bora katika maswala utandawazi, ujuzi wa kidijitali, ujuzi wa
madini, uchumi samawati, ubunifu, ujenzi, na ushonaji wa mavazi.
Kwa ushirikiano na Shirika la World Vision tumeweza kujenga na kufungua rasmi madarasa sita ya chekechea katika kaunti ndogo ya Taveta. Katika sekta ya Ujenzi na miundo-msingi, Tangu nichukue hatamu, serikali yangu imechukulia sekta hii kwa uzito sana. Tumeweza kukarabati kilomita mia tatu na hamsini za barabara katika wadi zote. Ukarabati huu ni kama vile grading, na kuweka murram katika sehemu zingine. Tumeweza pia kuhakikisha tinga zetu ziko katika hali nzuri ya kazi.
Hata hivyo, sekta hii imepata changamoto kubwa kufuatia mvua hii ya El Nino inayoendelea kunyesha. Barabara zetu nyingi zimeharibika. Maeneo mengi yamekatwa, na hayafikiki.
Tunashirikiana kwa karibu na mashirika ya serikali kuu kama KENHA, KERRA na KURA kuhakikisha kuwa barabara zote zilizoharibika zinakarabatiwa haraka iwezekanavyo. La muhimu la dharura kwa sasa, ni kusaidia pale pameharibika na hapapitikin ili shughuli za lazima ziweze kuendelea.
Wananchi wenzangu,
Katika sekta ya Kilimo na Mifugo, kwa ushirikiano na shirika la FAO, tumeweza kuinua hali ya uchumi ya wakulima wetu kwa kuwazawadi na matangi 500 ya maji, na mbuzi
2,550 aina ya Gala Goats zenye uwezo wa kunawiri katika mazingara magumu. Pia, tumeweza kuanzisha mradi wa usambazaji wa mbegu ya nyasi ya lishe za mifugo, pamoja na
kupeana vifaa vya kukata nyasi kwa wakulima wetu.
Tumeweza pia, kupeana mbegu elfu kumi za migomba na mbegu 800 za minazi zilizopasishwa kuwa za uzalishaji wa hali ya juu. Serikali yangu imepanua ekari elfu 18 katika
mashamba ya mpunga ya Buruma, huko Mboghoni, katika kaunti ndogo ya Taveta, na tayari, katika mwaka huu wa kifedha, tumepanga kuwekeza kiasi cha shilingi millioni 45 kwa ujenzi wa kiwanda cha kukoboa mpunga, na kupakia
mchele.
Wakulima wetu wa nyanda za milimani, pia hawakuwachwa nyuma. Tumeweza kuwekeza kwa vifaa vya kisasa katika mashirika ya maziwa ya Tagho na Dawida ili kuwezesha ukuaji wa kiuchumi na kutoa ajira kwa wananchi wa maeneo
ya Wundanyi/Mbale na Mwanda/Mghange mtawalia.
Katika Wadi ya Wundanyi Mbale vile vile, tumeweza kupeana mizinga zaidi ya mia tatu na thelathini ya kisasa, kwa wafugaji wa nyuki kutoka katika vijiji hamsini na tisa.
Ni matumaini yangu kwamba, juhudi zetu hizi, zitaimarisha hali ya uchumi ya wakulima wetu, na pia kutoa ajira kwa watu wetu huko mashinani.
Mabibi na Mabwana,
Katika sekta ya Maji na Mazingira, tangu munipatie hatamu za uongozi, tumeweza kujenga tenki la kuhifadhi maji huko Dembwa, miradi ambao unakaribia kukamilika, na utazunduliwa punde tu miundo-msingi na mikakati ya
usambazaji maji itakapo kamilika. Tumeweza kukarabati na kuweka mashini za kupiga maji na Kuchimba visima kadhaa katika kaunti yetu, na pia tumeweka vifaa vya kutumia nishati ya jua katika visima tofauti kama kisima cha Uthiani wadi ya Challa.
Tumemaliza kujenga mabwawa kama vile Bwawa la Mwambisi lililo Wadi ya Wusi/Kishamba, Bwawa la Lora, huko Kiteghe na Bwawa la Kiroghe katika wadi ya Kasighau. Katika sekta hii pia, tumeboresha kupanua usambazaji wa maji, kama katika mradi wa Itinyi, mradi wa kwa Hebron Wadi ya Wundanyi Mbale, na Kadhalika.
Tumeweza kupanda miche zaidi ya laki moja kaunti nzima, na ninaendelea kuwasihi wananchi wangu tushirikiane katika juhudi za kupanda na kukuza miti, ili kukabiliana na ukame, na mabadiliko ya tabia nchi.
Wananchi wenzangu,
Katika sekta ya ardhi, serikali yangu imeweza kupata wafadhili kadhaa wanao simamia zoezi linaloendelea la mpangilio wa ardhi ikizingatia mfumo wa teknologia (GIS) almaarufu kama Spatial Plan. Hili ni zoezi muhimu ambalo
linasaidia Kaunti kupanga sehemu za kufanya maendeleo, kujenga mahospitali, shule, ofisi na kadhalika.
Serikali yangu imeshirikiana na serikali kuu kutekeleza mradi wa kuimarisha mitaa ya mabanda ambapo awamu ya kwanza imekamilika katika eneo la Taveta ikiwemo BuraNdogo na
Chachewa. Katika awamu ya pili, tayari wananchi wameanza kuhusishwa kwa mpangilio huo utakaofanyika eneo la Kaloleni mjini Voi na eneo la Kariobangi na Soko ya zamani, mjini Mwatate.
Tumeweza, kama kaunti, pia kuweka mikakati ya kupandisha miji ya Taveta na Voi kuwa Manisapaa, na kwa sasa hivi majina ya watakao simamia manisapaa hizi, yamepelekwa kwa bunge letu la kaunti. Ombi langu ni kwamba, watakao pitishwa, watasimamia miji hiyo kwa uadilifu.
Katika sekta ya Fedha, Nimeweza kuweka mikakati ya kuzuia ufujaji wa mapato ya ndani kwa kuwekeza katika mfumo wa kidijitali wa usimamizi wa mapato, na nina imani katika mwaka mpya wa kifedha, mapato yetu ya kaunti
yataongezeka kwa kiwango cha kuridhisha. Ni vyema pia, niwajulishe kwamba, nilipoingia nilipata serikali ina malimbikizi ya mishahara ya wafanyikazi ya miezi mine, lakini kufukia sasa, nimeweza kulipa mishahara kwa muda unaofaa,
na tunafanya bidii kuhakikisha kwamba tunalipa malipo ya kisheria kama vile NHIF, NSSF, kwa muda unaofaa.
Nikimalizia, ningependa kueleza ghadhabu yangu, kwa kitendo cha kusikitisha kwa Coast Water Services Board cha kukatia Kaunti hii maji, kwa deni la shillingi millioni mia sita themanini na nane la tangu mwaka 2006, ilhali maji haya ya Mzima springs yanatokea katika kaunti hii hii ya Taita Taveta. Udhalimu huu, ni kati ya dhulma (HISTORICAL INJUSTICES) ambazo zimezonga tangu jadi. Tutaendelea kupambana na dhulma hizi, na zengine, kama vile haki yetu ya kugawiwa nusu ya mapato ya Tsavo East na Tsavo West, ambazo ziko kwenye ardhi yetu, kama vile ilivyoagiziwa Mheshimiwa Rais William Samoei Ruto.
Wananchi wenzangu, napenda kuwatia moyo ya kwamba mikakati tuliyoiweka tangu niingie mamlakani kama Gavana wenu, imeanza kuzaa matunda. Hivi karibuni, gurudumu la maendeleo, ambalo limeanza kusonga mbele, litashika kasi, na Jimbo letu la Taita Taveta, lililobarikiwa na utajiri
mkubwa, litarudia hadhi itakayoturidhisha sote. Mwisho kabisa, napenda kuchukua fursa hii, kutakia kila mkaazi wa Taita Taveta, KRISMASI NJEMA, na MWAKA MPYA wa MAFANIKIO.
MUNGU IBARIKI TAITA TAVETA!!!
MUNGU IBARIKI KENYA!!!
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
Leave a Comment