Tumeweka mkazo sana juu ya kile ambacho taifa linaweza kufanyia kila mmoja wetu – haki zetu – na kusahau kile ambacho kila mmoja wetu anapaswa kufanyia taifa letu. Yafuatayo ni mapendekezo muhimu yaliyotolewa na Jopokazi:
1. Wakenya wana haki kutoka kwa Mungu ambazo sasa ni lazima ziende sambamba na Mkataba wa Majukumu ya Wananchi ambayo yamehamasishwa na Wimbo wa Kitaifa na Maadili ya Kitaifa, na inajumuisha Ahadi ya Uzalendo kwa Taifa na Katiba ya Kenya (kwa shule, mahali pa kazi na katika hafla rasmi za kitaifa na umma).
2. Kuanzisha na kuendesha mipango ya kuendeleza na kusambaza elimu ya uraia kuhusu haki na majukumu.
3. Fundisha watoto utamaduni wa uwajibikaji kwa kubuni mipango ya utendaji na kujitolea shuleni ili kusaidia jamii na asasi zilizo karibu na shule.
4. Kuwatiisha Mawaziri wote na Makatibu Wakuu kwa taasisi za umma wanazoendesha. Ikiwa asasi za umma haziwafai, basi wao hawawafai Wakenya.
5. Kubuni mtaala wa kulea watoto na kufundisha ulezi katika asasi za kidini, vituo vya afya na katika asasi nyinginezo za kijamii, serikali na kitamaduni.
6. Kuhimiza vijana Wakenya kati ya miaka 18 hadi 26 kujitolea kwa kipindi cha miezi sita ya maisha yao kuwatumikia Wakenya kwa hiari.
Haya ndio matishio makuu kwa ufanisi wa Kenya na ustawi wa nchi yetu. Jopokazi linapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:
1. Kuelimisha Wakenya kuhusu tamaduni na mila zao tofautitofauti na kuunda mtaala wa shule unaofundisha wanafunzi kuhusu tamaduni na mila za kila jamii na dini nchini Kenya. Pia, ni sharti shule zote za sekondari za bweni za umma ziandikishe asilimia 50 ya idadi ya wanafunzi wake kutoka nje ya kaunti.
2. Ondoa mtindo wa urais wa “mshindi ndiye anayechukua kila kitu”, badala yake anzisha mfumo jumuishi wa kisiasa. Hii itabadilisha mfumo wetu wa kisiasa ili uambatane zaidi na desturi za makubaliano ya watu wetu, na kupunguza makali ya kikabila ambayo ndio msingi wa ushindani wa kisiasa anaovuruga ubora wa uchaguzi.
3. Kama njia ya kuunganisha jamii zetu zilizo mipakani, na kubadilisha mfumo wetu wa sasa wa kisiasa na kikabila, huku tukijenga uchumi uliostawi zaidi, tuharakishe mchakato wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kama hatua ya kuafikia Shirikisho la Kisiasa.
4. Hakikisha kwamba usambazaji wa rasilimali haufanywi kwa usawa pekee bali pawe hasa na hisia za usawa – Punguza migogoro kuhusiana na usambazaji wa rasilimali za kitaifa kwa kuwachukulia Wakenya wote kuwa sawa – hii inapaswa kuzingatia idadi ya watu, uwekezaji unaohitajika katika sekta za afya na kilimo, utoaji wa huduma, na upatikanaji wa rasilimali asili na fursa za kuishi
5. Baraza la washauri — Kwamba Rais kama Nembo ya Umoja wa Kitaifa anapaswa kuwa na ushauri wa kibinafsi wa watu mashuhuri, wenye uzoefu, na wenye heshima wanaohudumu katika Baraza la Washauri pasi na kulipwa mishahara.
6. Imarisha ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa ili kuiwezesha kushughulikia tatizo la ubaguzi wa kisiasa kwa kuajiri na kuteua Msajili ambaye ni huru, anayejiamini na mchapa kazi.
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
Leave a Comment