Categories: Kenya Trends

BBI2: MUHTASAR I WA RIPOTI YA JOPOKAZI LA RAIS KUHUSU MAPATANO MARIDHIANO NA U MOJA WA KITAIFA

Sura ya 2 — Maadili ya Kitaifa

Tunakosa imani, maadili na matamanio ya pamoja kuhusu nini Kenya inaweza kuwa ikiwa sote tutazingatia maadili ya kitaifa ambayo hujenga na kuimarisha umoja wetu. Utaratibu huu ni fursa ya kihistoria kwetu kuanza, kwa hiari, kufafanua, kuendeleza na kuyaambata maono ya pamoja ambayo yataleta umoja Kenya na uwezo wa kukabili changamoto zake zote kuu.Hii ni kazi ya ujima, inayoanzia katika familia na jamii, ikisaidiwa na mikakati inayokumbatia tamaduni nzuri, imani na maadili ya jamii mbalimbali za Kenya na kuwezeshwa na mashirika ya kijamii, sekta ya kibinafsi, na asasi za Serikali. Itajumuishwa katika mfumo rasmi wa elimu, kuanzia chekechea na kudumu milele, asasi za dini na utamaduni, vyombo vya habari, na sekta yetu ya sanaa. Hayatakuwa maadili ya jamii moja bali ya jamii zenye sauti tofautitofauti zilizomotishwa na hamu ya kuchangia, kumiliki na kujenga taifa ambalo ni nyumbani kwetu sote. Hapa chini ni baadhi ya mapendekezo muhimu zaidi ambayo wanajopo wanaamini yatasaidia kujenga maadili thabiti ya kitaifa.

1. Kazi muhimu zaidi ya kitaifa ni kuwazia mambo makubwa na ya kudumu— Uchaguzi huja na kuenda na tawala mbalimbali, lakini Kenya itaendelea kuwepo. Tunahitaji maono kuhusu Kenya tunayotaka kuishi katika vizazi vitatu vijavyo au miaka 100. Maono yaliyofumbatwa katika michakato ambayo inaruhusu Wakenya kuyaendeleza zaidi ya chaguzi zinazokuja na kuenda.

2.Tunapaswa kujipatia historia halisi, inayobadilika, jumuishi na rasmi Rais Uhuru Kenyatta anapaswa kuagiza Historia rasmi ya Kenya inayorejelea miaka 1000 nyuma na inayotoa maelezo sahihi na halisi kuhusu makazi ya Kenya na wakazi wa sasa; historia zao, historia za uchumi na turathi za makabila yote nchini Kenya; majukumu ya wanawake kihistoria; maelezo kuhusu biashara ya kimataifa y a watumwa na ukoloni; mapambano dhidi ya wakoloni; historia ya kipindi cha baada ya ukoloni k a tika kila sehemu ya nchi; na historia ya kisasa ikiw emo ile ya maeneo ya mijini na jamii mpya nchini Kenya.

3. Ni lazima tufurahie ngozi yetu ya Kiafrika Jopokazi l inapendekeza kwamba Serikali ifanye mipango ya kuoanisha utambulisho wa kisasa wa Wakenya na tamaduni zetu tofauti za Kiafrika ili sisi Waafrika tujisikie vizuri kwenye ngozi yetu na pasiwe na mpaka kati ya hali hizi mbili, au zaidi, wakati mwingine hali k inzani

i. Imarisha Wizara ya Utamaduni na Turathi ambayo kwa sasa inaendeshwa na serikali kama shughuli tu ya pembeni

ii. Badilisha Siku ya Kufungua Zawadi inayoadhimishwa tarehe 26 Desemba iwe Siku ya Utamaduni Wa Kitaifa kwa kusherehekea utamaduni na kujifunz a kuhusu tamaduni zingine za Wakenya (hii inaweza pia kufanywa Januari 1).

iii. Kukuza heshima ya wazee.

4. Sisi sote tuna wajibu Ni sharti kila sekta kuu ya nchi itekeleze jukumu na wajibu wake kwa umakini zaidi katika kujenga maadili ya kitaifa kutokana na tamaduni tofauti za nchi, masilahi na makundi

5. Kukuza maadili wakati wote EACC inapaswa kulenga kukomesha uhalifu wa kiuchumi, na majukumu yake ya maadili yasambaziwe NCIC ambayo kuanzia sasa itabadilishwa jina na kuitwa Tume ya Maadili na ma jukumu yake yaboreshwe sambamba na mwito wa Tume hiyo, na kwamba iwe chini ya Ofisi ya Rais. Pia

i. Kufundisha watoto jinsi ya kutoa huduma na kuwajibika kwa kuanzisha Mtandao wa Kujitolea wa Kitaifa unaounganisha vijana
na fursa za kujitolea

ii. Kufundisha maadili kama somo la lazima katika mtaala wote wa masomo kutoka nasari hadi chuo kikuu

iii. Kujumuisha mafunzo ya maadili na kanuni za kitaifa kama sehemu ya utamaduni wa kila kabila na hususan kama sehemu ya mafunzo wakati wa sherehe za kuingia utu uzima

iv. Kutekeleza utaratibu wa sasa wa utekelezwaji sheria chini ya Kifungu kuhusu Uongozi na Uadilifu

6. Unganisha amali za kitamaduni na kaida za kisasa za Wakenya kama inavyoonyeshwa katika sherehe za kitamaduni za kuingia utuuzima na maadili na kanuni za Katiba, na Majukumu na Haki za uraia.

Sura ya 3 — Majukumu na Haki za Uraia

Kwaela News Network

Leave a Comment
Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

18 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago