SHIRIKA LA HEARTBEAT MINISTRIES LAFADHILI WANAFUNZI 10 TAITA TAVETA

Mkurugenzi wa Shirika hilo lenye makao yake Mjini Bura, Oliver Mbogho ameeleza kuwa ufadhili huo unanuiwa kuboresha viwango vya elimu eneo hilo.

Ni afueni kwa zaidi ya wanafunzi 10 watakaojiunga na kidato cha kwanza kutoka familia zisizojiweza maeneo tofauti ya kaunti ya Taita Taveta baada ya kunufaika na ufadhili wa masomo kutoka shirika la Heartbeat Ministries kutoka Canada.

Mkurugenzi wa Shirika hilo lenye makao yake Mjini Bura, Oliver Mbogho ameeleza kuwa ufadhili huo unanuiwa kuboresha viwango vya elimu eneo hilo.

Aidha utasaidia kupunguza idadi ya watahiniwa ambao husalia nyumbani na kukosa kuendeleza masomo licha ya kufanya vyema katika mitihani ya kitaifa.

Wanafunzi wengine wamepata ufadhili  kutoka mashirika tofauti huku wengine wakifadhiliwa na serikali ya kaunti.

Taarifa na Fatuma Rashid.

~ Radio Kaya

 

more recommended stories