Mwatate — Taharuki imezidi kuongezeka miongoni mwa wanahisa wa Bura Ranch kufuatia maswali mazito kuhusu matumizi ya fedha za ranch na madai ya mamilioni ya pesa yanayohusishwa na Mbunge wa Mwatate, Mheshimiwa Peter Shake.
Wanahisa wa ranch hiyo, kupitia ziara yao ya hivi karibuni, waligundua kuwepo kwa kisima cha maji kinachodaiwa kuchimbwa mwaka 2014 kwa gharama ya shilingi milioni 3.8, kilichokusudiwa kuboresha shughuli za ufugaji. Hata hivyo, licha ya fedha hizo kudaiwa kulipwa, kisima hicho hakijawahi kutumika kwa zaidi ya miaka kumi, huku viongozi wa ranch wakishindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu hali hiyo.

Wasiwasi huo umeongezeka zaidi kufuatia madai kuwa Mbunge wa Mwatate, Mheshimiwa Peter Shake, anadai jumla ya shilingi milioni 55 kutoka kwa Bura Ranch, akidai kuwa fedha hizo zilitumika kutafuta cheti cha umiliki wa ardhi ya ranch. Wanahisa wanasema kuwa hadi sasa, hakuna risiti wala vielelezo vilivyowasilishwa kuthibitisha matumizi ya fedha hizo.
Taarifa zinaeleza kuwa tayari Mheshimiwa Shake amelipwa zaidi ya shilingi milioni 11, huku viongozi wa ranch wakipanga kumlipa shilingi milioni 46 zaidi mwaka huu, jambo lililozua maswali makubwa kuhusu uwajibikaji na uwazi wa matumizi ya fedha za wanahisa.
Katika tukio lingine lililozua mshangao, wanahisa walidai kushuhudia uwepo wa beacons ndani ya shamba hilo zilizoandikwa jina “Peter M”, hali iliyowafanya kuhofia kuwa huenda kuna njama ya kunyakua sehemu ya ardhi ya ranch.

Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa wanahisa uliofanyika Januari 17, 2026, Mheshimiwa Shake alizungumza kwa hasira, akisisitiza kuwa hatasamehe hata shilingi moja ya fedha anazodai kutumia kwa manufaa ya ranch. Alidai kuwa kama si juhudi zake binafsi, ranch hiyo huenda ingeshanyakuliwa kitambo.
Bila kutaja majina, mheshimiwa huyo alidai kuwa watu kutoka familia kubwa nchini walimshawishi kwa kumpa mamilioni ya pesa ili asaliti jamii yake, lakini alikataa. Alijigamba kuwa yeye ni tajiri na hawezi kushawishiwa na pesa kusaliti watu wake, akidai kuwa i gekuwa ni watu wengine – kina Mwakuzughwa – wangeiuza ranch hiyo kwa manufaa binafsi.
Hata hivyo, wanahisa wa Bura Ranch wanasema kuwa hasira na kauli kali haziwezi kuchukua nafasi ya uwajibikaji, wakisisitiza kuwa wanahitaji ufafanuzi wa wazi, wa maandishi na wenye vielelezo kuhusu matumizi ya shilingi milioni 55 zinazodaiwa kutumika kutafuta cheti cha umiliki wa ardhi.
Kwa sasa, uchunguzi unaendelea kubaini undani wa sakata hilo, huku wanahisa wakizitaka taasisi husika za uchunguzi na ujasusi kuchukua hatua za haraka na kufichua ukweli wa madai hayo bila upendeleo.
more recommended stories
TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSUREThe growing controversy surrounding the.
NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULINGAffected families in Mlambenyi, Golani and.
TAITA TAVETA: WILL DEBORAH WAKESHO SUCCEED THE LATE MARGARET KAWUKI, OR WILL POLITICAL CARTELS INTERFERE?Questions emerge over Jubilee Party’s.
CHRISTOPHER MWAMBINGU: EACC INVESTIGATES ALLEGED FORGED DEGREE USED TO SECURE DIRECTOR OF ADMINISTRATION POSITIONA third case raises further.
MWATATE MP RACE: RICHARD LUKINDO’S AMBITIONS AND THE UNANSWERED DEGREE QUESTIONThe political stakes surrounding former.
TAITA TAVETA: PRISONS OFFICER, NINE OTHERS ARRESTED IN MOTORCYCLE THEFT SYNDICATE PROBESerious questions emerge over alleged security.
ALLEGATIONS OF HARASSMENT RETURN ALONG VOI-CALTEX ROAD CORRIDORResidents, motorists, and public transport operators.
CHURU CHURU PROJECTS HAZIJENGI TAIFAKuna tofauti kubwa kati ya.
BWIRE: ACCESS TO POWER IS NOT A POLITICAL MANDATEHon. John Bwire’s declaration that.
RESIDENTS RAISE CONCERNS OVER ALLEGED MOTORIST HARASSMENT ALONG VOI-MOMBASA ROADResidents and motorists in Voi.
THE TAITA TAVETA COUNTY ASSEMBLY’S VETTING PROCESS MUST UPHOLD THE CONSTITUTION AND PUBLIC TRUSTWe, the concerned citizens of Taita.
THE STRUCTURED POVERTY IN TAITA TAVETAResidents demand answers after thousands.
Taita Taveta Workers Demand Immediate Payment of Salaries and AllowancesFrustration is mounting among employees in.
Nepotism Concerns Intensify as Family Links Dominate Senior Appointments in Taita Taveta CountyCalls for transparency and fairness in.
UNGA, POLITICS AND 2027: PS MWAMODO’S JORA VISIT SPARKS DEBATEA food distribution exercise led by.
Taita Taveta Residents Increasingly Question Leaders’ Priorities Amid Unresolved ChallengesWhat was billed as a development.

Leave a Comment