WAZIRI WA ZAMANI ERICKSON KYONGO ALALAMIKIWA KWA KUACHA DENI LA SACCO, ‘GUARANTORS’ WAKIANZA KUTESEKA

 

Na Mwandishi Wetu – Kwaela News Network

Malalamiko mazito yameibuka dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Ufugaji, Uchumi Samawati na Maendeleo ya Ushirika, Bw. Erickson Kyongo Johnson, kufuatia kushindwa kulipa mkopo wa Ksh 2 milioni alioupata kutoka Qwetu DT SACCO, hali iliyopelekea mishahara ya wadhamini wake kuanza kukatwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa na mmoja wa wadhamini wanaoathirika, Bw. Kyongo alifuata udhamini wa mkopo huo rasmi akiwa bado Waziri, licha ya kufahamu wazi kuwa alikuwa karibu kujiuzulu kutoka wadhifa wake wa serikali.

Baada ya kujiuzulu, Bw. Kyongo alikamilisha taratibu zote za kuondoka kazini (clearance) na akaomba kulipwa gratuity ya miaka miwili, inayokadiriwa kuwa asilimia 31 ya mshahara wa msingi (basic salary) kwa kila mwezi. Hata hivyo, katika kipindi chote hicho, Qwetu DT SACCO haikuchukua hatua zozote za haraka kufuatilia au kulinda mkopo huo, licha ya mabadiliko ya hali ya ajira ya mdaiwa kujulikana mapema.

Kinachozua mshangao mkubwa ni kwamba ni sasa ndipo SACCO imeanza kuchukua hatua za kukata mishahara ya guarantors, ilhali suala hili liliripotiwa na kujadiliwa mapema na wahusika wote. Mwanzoni mwa mwaka huu, wakati wadhamini walipoibua wasiwasi wao, Bw. Kyongo alieleza kuwa angeuza shamba lake lililopo Taveta ili kulipa deni hilo, jambo ambalo halijatekelezwa hadi sasa.

Guarantors to face the Music

Wadhamini wanasema hatua ya Qwetu SACCO kuchelewa kuchukua hatua dhidi ya mdaiwa mkuu inaakisi mfumo dhaifu wa ufuatiliaji wa mikopo, hasa pale mdaiwa anapokuwa na cheo, ushawishi au mamlaka. Kwa hali hii, wanachama wa kawaida ndio hujikuta wakibeba mzigo wa makosa ambayo yangeweza kuzuilika kupitia usimamizi thabiti, utekelezaji wa sera bila upendeleo, na ufuatiliaji wa mapema (proactive measures).

Cha kushangaza zaidi, wadhamini wanahoji kwa nini SACCO imepuuza ukweli kwamba Bw. Kyongo ana uwezo wa kulipa deni lake binafsi, ikizingatiwa kuwa anamiliki mali mbalimbali ikiwemo magari, mashamba na assets nyingine, badala ya kuwabebesha mzigo wanachama waliomdhamini kwa imani.

Read Also: PETITION FOR RECOVERY OF PUBLIC FUNDS PAID TO FORMER CECM ERIC KYONGO.

Hali hii imeibua maswali mazito kuhusu usawa, uwajibikaji, na ulinzi wa maslahi ya wanachama wa kawaida wa SACCO, huku kukiwa na hofu kwamba endapo Qwetu SACCO haitarekebisha mifumo yake ya ufuatiliaji wa mikopo, wanachama wengi wanaweza kuendelea kuumia na hatimaye kujiondoa, jambo litakalodhoofisha uaminifu na uendelevu wa taasisi hiyo ya kifedha.

Kwa sasa, wadhamini wanaitaka Qwetu DT SACCO kuchukua hatua za haraka dhidi ya mdaiwa mkuu, badala ya kuwaadhibu wanachama wa kawaida kwa uzembe ambao ungeweza kuzuilika.

 

more recommended stories