WAZIRI WA ARDHI TAITA TAVETA, BI. CHRISTINE ZIGHE MWASHIGHADI, ADAIWA KUTUMIA CHETI BANDIA

 

Tuhuma nzito zimeibuka dhidi ya Mwakilishi wa Idara ya Ardhi, Mipango ya Miji na Uchimbaji Madini katika Kaunti ya Taita Taveta, Mheshimiwa Christine Zighe Mwashighadi. Inadaiwa kuwa ametumia cheti bandia cha shahada.

Ripoti zinaonesha kuwa anadai kuwa na Shahada ya Mipango ya Miradi kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN), lakini chuo hicho kimethibitisha kuwa hakijawahi kumtawaza shahada hiyo.

Hali hii inaleta maswali mazito:

  • – Je, Gavana Andrew Mwadime almaarufu Wakujaa atachukua hatua za kinidhamu?
  • – Je, serikali ya kaunti itarejesha fedha zote alizopokea kama mshahara na marupurupu akiwa kazini kwa kutumia stakabadhi bandia?
  • – Je, atafikishwa mahakamani kwa kosa la kughushi na kutoa taarifa za uongo?

Sasa lawama zinageukia Bunge la Kaunti lililoidhinisha uteuzi wake, licha ya kudaiwa kufanya vibaya katika usaili. Awali, alikataliwa kwa sababu zisizojulikana wazi, lakini baadaye akapitishwa kisiri.

Spika wa muda wa bunge hilo, anayejulikana kama Mr. Well Schooled, sasa anatuhumiwa kuidhinisha uteuzi haramu wa afisa haramu, aliye na vyeti bandia.

Je, haki itatendeka au ni mchezo wa siasa tena unaochukua mkondo?

#WanTam katika #TaitaTaveta bado ni HALI YA KAWAIDA! 

more recommended stories