WAFANYI KAZI WA BUNGE LA KAUNTI WALISHWA KIAPO

Taita Taveta County Assembly Clerk - Gadiel Maghanga

Leo alfajiri na mapema, viongozi wa bunge la kaunti ya Taita Taveta waandaa mkutano,ukiongozwa na clerk Bwana Gadiel Maghanga, akisaidiwa, bwana William Sowa na Elizabeth Ngele. Kabla mkutano haujaanza, Clerk aliamurisha sergent at arms kunyang’anya kila mtu simu na kuzifungia kwa sefu.

S𝐰𝐚𝐥𝐢 𝐧𝐢 𝐣𝐞, 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐟𝐢𝐜𝐡𝐚 𝐧𝐢𝐧i?

Kwenye mkutano huo, wafanyikazi hao wameonywa vikali kwa kutoa siri za bunge na kumfikia ADMIN wa Kwaela News Network na kuzichapisha hadharani. Bwana Clerk alikasirishwa sana na swala la kuona siri za bunge za kweli zinachapishwa hadharani.

Mheshimiwa Clerk ameongea kwa ukali akisema kuwa siri zinazochapishwa Kwaela News Network hazipaswi kutoka nje ya jengo la bunge, wala kuchapishwa kwenye mtandao ili ziweze kusomwa na umma. Amewaonya wanaotoa habari hizo waache mara moja sababu wakikamatwa wataona cha mtema kuni kwa kuchukuliwa hatua kali ya kuvunja masharti na miiko ya bunge.

Kuona siri za bunge la kaunti zinachapishwa hadharani kumetingisa uongozi wa bunge la kaunti na hivyo kuwafanya kutumia njia tofauti tofauti kutaka kujua ni nani anatoa siri hizo. Kufikia sasa inaonekana bado hawana habari.

Bw. Sowa amedokeza kwamba huenda kuna wafanyi kazi fulani wanatoa siri za bunge na kuwapa MCAs, ambao hakuwataja na kufikishia ADMIN wa Kwaela News Network. Hii ni ishara kuwa hawana habari ni vipi kitoweo kimetumbukia nyongo. Isitoshe basi, Kwaela News Network inaandaa kumuangazia Bw Sowa ambaye ametajwa kwa mlolongo wa masaibu ya ufujaji wa fedha za umma, ufisadi, utepetevu na maovu mengine kadha wa kadha.

Kwenye mkutano huo, Mheshimiwa Clerk ameshindwa kujieleza vizuri hata wafanyikazi wakamshangaa, asilolijua ni kuwa watu wana habari ya maovu yote anayoyafanya chini ya maji. Kwa mfano, Bw. Clerk ameshindwa kueleza ni nini Spika wa Bunge, P.A wake na MCAs kadhaa maeenda kufanya nchini Rwanda tangu wiki jana ilhali wafanyikazi wa kawaida hawalipwi marupurupu yao, kisa hakuna pesa. Pesa za wangwana hawa za kutangatanga zinatoka wapi?

Kwenye mkutano huo wafanyikazi wote wamelishwa kiapo cha kutotoa siri za bunge na kuzifikishia ADMIN wa Kwaela News Network.

Aliyepeane kiapo hicho ni Pastor bandia anayeitwa 𝐆𝐞𝐨𝐫𝐠𝐞 𝐌𝐳𝐮𝐧𝐠𝐮 ambaye ni Sergeant at Arms bungeni. Duru zinasema kuwa Bwana Mzungu hakumaliza masomo ya shule ya msingi, inasemekana aliachia shule darasa la sita. Wafanyi kazi wa bunge wanashangaa imekuwaje wanaapishwa na mtu ambaye hata kuandika jina lake mwenyewe huwa anatokwa na kijasho chembamba! Mengi zaidi kuhusu Pastor huyu bandia, mwenye kipawa cha kuwatembelea wajane, tutayaweka bayana kwa toleo lijalo.

Kwa haya machache na mengi tunasema ahsante na usiondoke.

more recommended stories