Kwa muda mrefu swala la Pending Bills limekuwa tatizo sugu katika kaunti ya Taita Taveta.
Takrimu zinaonyesha kuwa kufikia sasa kaunti inadaiwa mamilioni ya Pending Bills tangu mfumo wa ugatuzi uanze. Bajeti ya kaunti ya fedha ya mwaka wa 2022/2023 ya Taita Taveta ina takriban Kshs 351,546,613 ya pending bills.
Kufikia sasa haijulikani ni hela ngapi zimelipwa kupunguza madeni hayo. Isitoshe, wanakandarasi hawajui kama watalipwa fedha zao zote mwaka huu. Lakini kuna madai ya kwamba hela hizo zimeadimika kuliko maziwa ya kuku.
Tatizo hili likiambatana na tatizo la Wage Bill limeipatia serikali ya kaunti kisingizio kikubwa cha kutofanya maendeleo ya maana katika jimbo hili. Serikali hii inadai kuwa mgao wa hela unaweza kuishia kulipa madeni haya na recurent expenses.
Maswala haya na mengine yamewafanya wana DaTu na viongozi mbali mbali kutoka jimbo hili kuwa na mijadala ya kusisimua mtandaoni.
Baada ya mwana DaTu mmoja kutaka kujua inakuwaje serikali inakumbwa na madeni haya mazito ilhali kila mradi huwa umetengewa hela kwenye bajeti na kufadhiliwa ipaswavyo? Aliyekuwa Waziri wa Maji, Mheshimiwa Esther Mwanyumba, alijitokeza wazi na kuorodhesha maneno yafuatayo kama baadhi ya sababu kuu zinazosababisha ulimbikizaji wa madeni jimboni:
1. Serikali kuchelewesha procurement plan.
Mara nyingi procurement plan ambayo inatarajiwa kuwa tayari mwanzoni mwa mwaka wa fedha hucheleshwa hadi mwezi wa tisa, miezi mitatu baada ya mwaka wa fedha kuanza. Hii inazuia tendering kukamilika ndani ya miazi mitatu ya mwaka wa fedha ( Julai – Septemba), ili kuwezesha mradi kuanza kwenye wakati ufaao. Hivyo basi inakuwa vigumu mradi huo kukamilika ndani ya mwaka wa fedha. Ifikapo tarehe 30 Juni, mwaka wa serikali unafungwa kabla mradi haujakamilika na pesa inabidi irudishwe kwa CRF account na kuacha wanakandarasi wakidai.
2. Kuchelewa kwa mgao kutoka serikali kuu.
Hili limekuwa tatizo kubwa na si kwa serikali ya kaunti ya Taita Taveta pekee bali ni kwa nchi nzima. Kwa hivyo mwaka wa serikali unapofungwa tarehe 30 Juni, serikali ya kaunti italazimishwa kuanza mwaka mpya wa kifedha na madeni ya miradi ya mwaka uliopita.
3. Makadiro finyo ya gharama ya miradi.
Mara kwa mara inatokea kuwa mwanakandarasi ana makadirio ya chini ya mradi. Kutokana na inflation na mambo mengine yanayotokea mradi ukiendelea, gharama inaweza kupita matarajio ya bajeti. Hivyo basi inalazimu serikali kusukuma hela zote zilizozidi kwa mwaka unaofwata kama madeni.

4. Ufisadi haswa kwa miradi ya wafadhili mbali mbali.
Hii hutokea mara tu mwanakandarasi anapojua kuwa mradi umefadhiliwa na mtu au shirika ambalo lina uwezo. Inadaiwa kuwa maafisa wa kaunti na mwanakandarasi wanaingiwa na ulafi na kuzidisha makadirio ya gharama ya mradi. Hivyo basi bajeti iliyotengwa haitoshi na pesa zinaisha kabla mradi haujakamilika. Mwishowe mfadhili anadinda kuongezea hela na mradi unakwama.
Wakati mwingine tatizo huwa ni mambo ya rushwa. Kuna madai ya kuwa kuna baadhi ya wafanyikazi walafi wa kaunti ambao huitisha hongo ya asilimia kumi ya bajeti ya mradi, mwanakandarasi akidinda kutoa, wanazuia malipo yake mpaka mwaka wa fedha unaisha. Hivyo basi pesa hizo zitakuwa deni kwenye mwaka wa fedha unaofuata.
5. Kuchelewa kwa wanakandarasi kumaliza miradi kwa wakati uliokubalika.
Inasemekana kuwa baadhi ya wanakandarasi wanafanya kazi pole pole hadi mwaka wa fedha unaisha kabla mradi haujakamilika. Kwa hivyo inabidi gharama zinakuwa deni mwaka wa fedha unaofwata, sababu hulipwa mradi unapokamilika.
6. Matukio ya dharura.
Matukio haya yanailazimu serikali kubadilisha bajeti kwa kukata ufadhili katika idara kadhaa na hela hizo zinatumika kwa matukio hayo ya ghafla. Mfano mzuri ni janga la Corona ambapo hela za miradi zilitumika kupambana na janga hilo. Migao ya wizara kadhaa ilibidi ikatwe na pesa kuelekezwa kwa wizara ya afya kupambana na corona. Hivyo basi malipo ya miradi iliyokamilika yanasitishwa na yatahesabiwa katika mwaka wa fedha unaofwata kama madeni.
7. Mwanakandarasi kufanya kazi bila kufuata sheria.
Wakati mwingine hutokea kuwa mwanakandarasi anapewa kazi kwa maneno ya mdomo bila kuandikisha mkataba wowote. Mara nyingi mradi huo hauko kwa bajeti ya serikali na hauna stakabadhi rasmi. Kwa hivyo mwanakandarasi anamaliza kazi lakini hapati malipo kama alivyotarajia. Kwa sababu ofisi husika ya kuruhusu malipo ya fedha haiwezi kubali kutoa hela bila stakabadhi zinazohitajika ili kuepuka maswali mazito kutoka kwa serikali kuu wakati wa audit. Hivyo basi inambidi mwanakandarasi ashughulikie kupata stakabadhi na huenda atazipata kama mwaka wa fedha umeyoyoma na malipo yake yanakuwa deni kwenye mwa wa fedha unaofwata.
Kwa kiwango kikubwa, haya na matatizo mengine ndiyo yanasababisha madeni almaarufu pending bills kupanda kana nyuzi za aliyeshikwa na homa kali.
Swala kuu sasa ni vipi serikali yetu ya kaunti itajikwamua kutoka kwa matatizo haya, ili iweze kufanya maendeleo ya kuboresha maisha ya wana DaTu?
Karibu utoe maoni yako kwa comments hapo chini.
Ahsante
Mwachere Shuma

more recommended stories
TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSUREThe growing controversy surrounding the.
NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULINGAffected families in Mlambenyi, Golani and.
TAITA TAVETA: WILL DEBORAH WAKESHO SUCCEED THE LATE MARGARET KAWUKI, OR WILL POLITICAL CARTELS INTERFERE?Questions emerge over Jubilee Party’s.
CHRISTOPHER MWAMBINGU: EACC INVESTIGATES ALLEGED FORGED DEGREE USED TO SECURE DIRECTOR OF ADMINISTRATION POSITIONA third case raises further.
MWATATE MP RACE: RICHARD LUKINDO’S AMBITIONS AND THE UNANSWERED DEGREE QUESTIONThe political stakes surrounding former.
TAITA TAVETA: PRISONS OFFICER, NINE OTHERS ARRESTED IN MOTORCYCLE THEFT SYNDICATE PROBESerious questions emerge over alleged security.
ALLEGATIONS OF HARASSMENT RETURN ALONG VOI-CALTEX ROAD CORRIDORResidents, motorists, and public transport operators.
CHURU CHURU PROJECTS HAZIJENGI TAIFAKuna tofauti kubwa kati ya.
BWIRE: ACCESS TO POWER IS NOT A POLITICAL MANDATEHon. John Bwire’s declaration that.
RESIDENTS RAISE CONCERNS OVER ALLEGED MOTORIST HARASSMENT ALONG VOI-MOMBASA ROADResidents and motorists in Voi.
THE TAITA TAVETA COUNTY ASSEMBLY’S VETTING PROCESS MUST UPHOLD THE CONSTITUTION AND PUBLIC TRUSTWe, the concerned citizens of Taita.
THE STRUCTURED POVERTY IN TAITA TAVETAResidents demand answers after thousands.
Taita Taveta Workers Demand Immediate Payment of Salaries and AllowancesFrustration is mounting among employees in.
Nepotism Concerns Intensify as Family Links Dominate Senior Appointments in Taita Taveta CountyCalls for transparency and fairness in.
UNGA, POLITICS AND 2027: PS MWAMODO’S JORA VISIT SPARKS DEBATEA food distribution exercise led by.
Taita Taveta Residents Increasingly Question Leaders’ Priorities Amid Unresolved ChallengesWhat was billed as a development.

Leave a Comment