UTUMIZI MBAYA WA MAMLAKA NA OFISI: UTAWALA WA KIIMLA

 

Baada ya kujiuzulu kwa mtangazaji Javan Mwadime almaarufu Kidasi Cha Mbeo kutoka kwa kituo cha Redio cha Anguo FM, kinachomilikiwa na Gavana Granton Samboja, imebainika kuwa Ward Administrator, Bi Mercy Mwazo, ameacha jukumu la kutumikia wananchi wa Wodi ya Chawia na kuchukua nyalifa za usimamizi na utangazaji katika kituo hicho cha kibinafsi, huku akipokea mishahara kutoka kwa serikali ya Kaunti.

Huu ni utumizi mbaya wa rasilimali za umma na ofisi.

Mercy Mwazo ambaye ni kabaraka cha Gavana Samboja ameamua kushiriki kuhujumu utendakazi kwa mwananchi na vile vile kutumika katika kampuni hiyo ya kibinafsi kuendeleza utawala dhalimu wa kiimla na ubepari.

Tarehe Tisa, mwezi wa nane, tunawaomba wana DaTu tushiriane kumalize utawala huu wa mtemi Gavana.

Kumwondoa mamlakani kutasaidia kuwezesha mali ya umma kutumika kwa manufaa ya wananchi, na pia kumkomesha  mtemi kutotumia raslimali za umma kulipa mishahara ya watangazaji wa stesheni yake.

Pamoja tukomboe Taita Taveta.

more recommended stories