SIASA ZA CHAMA CHA ODM TAITA TAVETA COUNTY

Vijana wa ODM Taita Taveta walupokutana na Vijana wa Kaunti ya kwale

Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka ujao, siasa nchini zinazidi kupamba moto. Chama cha ODM kinapojiandaa kufanya uchaguzi mashinani, migogoro za mapema katika kaunti ya Taita Taveta zimeanza kujitokeza.

Hivi majuzi kijana anayetambulika kwa majina Gabriel Mwakio a.k.a. Mjumbe kutoka Rong’e ambaye amekuwa mwanachama sugu wa ODM katika sekta ya Vijana (OYL) aliapa kuwaunga Dorcas Mlughu mwaniaji wa kiti cha Mwakilishi Wodi ya Rong’e na Professor Moris Mbondenyi kama Mbunge Mwatate. Hatua hizo hazijapokelewa vyema na uongozi wa chama cha ODM Tawi la Mwatate Kwa sababu wawaniaji hao si wanachama wa chama cha ODM.

Katika harakati za kuandaa uchaguzi tarehe kumi na tano 15th September, 2021 Mjumbe amekumbana na masaibu kadha wa kadha. Kwanza kabisa jina lake limetolewa Kwa orodha ya wawalikishi ama deligates sababu amekuwa mwiba kwa Mwakilishi Wodi wa sasa Mheshimiwa Harris Keke. Inaonrkana kuwa Mheshimiwa Keke anajaribu kutumia mamlaka yake ya kuwa kuongozi wa wengi katika bunge la Kaunti vibaya na kuhusisha ofisi ya tawi la MWATATE katika migogoro hiyo. Hayo yote ni kwa sababu anataka kuwania nafasi ya mwakilishi wa ODM wa kaunti ya Taita Taveta, ilihali inajulikana wazi kuwa yeye ni mwandani wa Gavana ambaye ni mwanachama wa chama cha Wiper Movement. Hivyo basi inahofiwa kuwa huenda mheshimiwa Keke ilanatumiwa na Gavana kuleta mgawanyiko kwa chama cha ODM sababu pia yeye ndio Kiongozi wa wengi bungeni.

Ambao wanapigiwa upato kumrithi Kamishna Tairo Loliang’a ni Jimmy Mwamidi aliyekuwa mwaniaji wa MCA Wodi ya Wundanyi Mbale ama Seneta Jones Mwaruma. Ndugu Mwamidi alirambishwa sakafu kwenye uchaguzi mdogo wa Wundanyi Mbale na mwaniaji wa chama cha Wiper, Mheshimiwa Stephen Mcharo.

Pia watakao gombea nafasi za Vijana katika kaunti ni pamoja na Mshirafu Joseph Nyambu ambaye pia anatarajiwa kugombea kiti cha uwakilishi wa Wodi ya Mwanda Mghange na Particia Mwashighadi ambaye pia ni mwandani wa Gavana na anayetarajiwa kugombea kiti cha uwakilishi Wodi ya Bura.

Sakata ndani ya chama cha ORM katika Kaunti ya Taita Taveta inaeendelea.

more recommended stories