BUNGE LA KAUNTI YA TAITA TAVETA LAIDHINISHA KUKODI MASHINE YA KUCHIMBA VISIMA

Wananchi kaunti ya Taita Taveta wanaohitaji kujichimbia maji kwa kutumia mashine ya ya kaunti, sasa wanaweza kupata huduma hizo kwa ada ya chini baada ya bunge la kaunti hii kuidhinisha sera inayotoa muongozo wa kukodi, kutumia na kudhibiti shughli za mashine hiyo iliyonunuliwa na serikali ya kaunti.

Haya ni kwa mujibu wa gavana wa kaunti hii Granton Samboja anayasema kuwa sera hiyo inaitaka idara ya maji na usafi wa mazingira kusimamia mashine hiyo, kutenga fedha maalum za kusimamia shughli na huduma za mashine hiyo na kwamba wizara ya fedha na mipango ya bajeti kaunti hiyo italazimika kufungua akaunti ambapo fedha zitakazo kua zikikusanywa kama ada ya watakao kodi mashine hiyo zitaelekezwa kama ushuru.

“Tunafahamu fika kwamba maji ni bidhaa muhimu katika maisha ya kila mmoja wetu hivyo basi kitengo husika hakina budi ila kuzingatia vigezo vyote vya kisheria, kimazingira na ushirikiano wa jamii wakati wa kukodi mashine hii. Ni sharti kuwe na usawa kama inavyohitajika kikatiba.” Gavana Samboja amesema.

Kulingana na sera hiyo, idara ya maji na usafi wa mazingira itatakiwa kubuni kikosi cha maafisa maalum kitakacho wahusisha wataalam wa maji, madereva wa gari hilo, wataalam wa kuchimba maji na madereva wa mashine ya mabomba ya maji.

Wananchi watakaohitaji kupata huduma za mashine hiyo hata hivyo watalazimika kutuma maombi yao kwa ada ya shilingi 1,000.

Ameyasema haya alipozuru kijiji cha Vighombonyi, wadi ya Wumingu/Kishushe ili kukagua mradi wa ujenzi wa zahanati ya Vighombonyi ambayo imeratibiwa kufunguliwa siku chache zijazo.

Ameitaja zahanati hiyo kama itakayosaidia pakubwa wananchi wa eneo hilo na vijiji jirani na kwamba atazidi kuhakikisha ahadi alizoweka wakati wa kusaka kura zinazimia.

Amesistiza hoja ya kuwataka wananchi kuzidi kuwa makini wakati huu wa vita dhidi ya virusi vya Corona vikizidi kuendelea.

Kwasasa Samboja anakutana na viongozi wa kijiji cha Mashighi, miongoni mwa hoja wanazozungumzia ikiwa ni pamoja na kuboresha Kilimo biashara, miundo msingi, afya, elimu na mengineo.

~ Kaunti ya Taita Taveta

more recommended stories