Abandoned Cattle Dip at Masae village in Mrughua.
Mnamo siku ya Ijumaa, tarehe 28 Oktoba 2022, iliripotiwa kuwa wezi wasiojulikana walivunja milango ya nyumba za walimu wa Mrughua Primary School na kuiba vitu kadhaa vikiwemo vyakula na hela walizopata humo ndani. Walimu na wakaazi wa maeneo hayo wameghadhabika na kuingiwa na wasiwasi.
Ndani ya wiki, visa kadhaa kama hivyo vimeripotiwa vijijini humo.
Katika kijiji cha mochi – Mnamu Sub – location, inadaiwa kuwa wezi hao waliingia kwa nyumba ya mkaazi mmoja, usiku wa manane na wakala chakula kilichobakishwa na kutoweka na vyakula vingine na bidhaa kadhaa.
Kijiji cha Shale – Mnamu – Sub Location, wezi walivamia nyumba ya mkaazi wakakuta kichwa cha mbuzi 🐐 kikichemka jikoni. Walibeba sufuria hiyo moto na kichwa hicho na kwenda kujificha takribani mita 50 kutoka kwa nyumba hiyo. Wakala hichom kichwa, wakanywa supu na kuacha sufuria hapo na wakatoweka.
Kijiji cha Masae – Mrughua sub Location, wezi walivamia nyumba mbili mchana, wakati wenyewe wameenda shughuli zao, wakaiba unga wa ngano, mafuta ya kupika, popcorns, sukari, runinga na kutoweka. Baadaye, runinga iliyoibwa ilipatikana imefichwa msituni.
Wakaazi wanaomba mkono wa serikali ufanye kazi yake kwa kuwatafuta na kuwakamata washukiwa hao.
Wakaazi wa Mrughua na Mnamu Sub location wanalalamika kuwa hawajui mahali chifu wao anakoishi. Hivyo basi, nje ya masaa ya kazi hawawezi wakampata ili awasaidie katika matatizo kama haya, ambayom sana sana yanafanyika usiku wa manane. Sub-chief wa Mnamu sub – location pia hajulikani anakoishi, hivyo basi kufanya uchunguzi kuwa mgumu sababu sub – chief wa Mrughua sub – location ameachwa pekeyake kupambana na matatizo hayo nje ya masaa ya kazi.
Wanawaomba hawa watumishi wa uma, chifu Bura Location na Sub – Chief Mnamu sub location, wasonge karibu na wakaazi ili kupambana na uhalifu huu kisheria.
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
Leave a Comment