Balozi wa Algeria hapa nchini Kenya Francis Elhamdi Salah (katikati), gavana Granton Samboja (kulia) na mshauri wa kisiasa afisi ya gavana Mwandawiro Mghanga muda mfupi baada ya kupeana vyeti vya usafiri kwa wanafunzi.
Wanafunzi kumi na sita kutoka kaunti ya Taita Taveta wanatarajiwa kuondoka nchini Kenya kuelekea taifa la Algeria kimasomo baada ya kupata ufadhili kutoka kwa ubalozi wa taifa hilo hapa nchini Kenya.
Kwenye sherehe zilizofanyika makao makuu ya ubalozi huo mjini Nairobi, balozi Francis Elhamdi Salah amedokeza kuwa 16 hao watapata udhamini kikamilifu kufanikisha kozi mbali mbali ikiwemo shahada ya uhandisi, sayansi, uchoraji na madawa.
“Hili ni kundi la kwanza kati ya wanafunzi 80 tuliochagua hapa nchini Kenya na wamepata ufadhili wote kufanikisha masomo yao katika vyuo kadha huko Algeria. Madhumuni yetu ni kuhakikisha tunawashika mkono wote wenye nia ya kujiendeleza kimasomo na tutazidi kushirikiana na serikali ya gavana Samboja ili tufanikishe agenda nyingi za maendeleo.” Balozi Salah amesema
Gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja ameapa kuboresha ushirikiano baina ya kaunti yake na taifa hilo ili kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wake.
“Tutazidi kushirikiana na mataifa ya inje ikiwemo hili la Algeria katika juhudi zetu kuhakikisha tunaleta maendeleo na kuboresha utoaji hudumu kwa wananchi. Elimu itazidi kusalia kipaumbele katika serikali yangu na tunaweka mikakati zaidi kuhakikisha raslimali za kutosha ikiwemo fedha zinatengewa wizara husika.” Samboja amehoji.
Wanafunzi hao wameapa kutilia maanani masomo yao ili kuleta maendeleo Taita Taveta punde watakapomaliza kosi zao.
“Ni jambo la kufurahia kuona leo hii mimi ni miongoni mwa wenzangu tuliobahatika kupata fursa hii. Naamini hii ni nafasi nimepata kufanikisha ndoto yangu ya usayansi ili kuzikabili changamoto zilizopo.” Agnes Msae ameeleza.
Baadhi ya wazazi walioshuhudia sherehe hiyo wameitaja hatua ya hii leo kama itakayosaidia kukabiliana na uhaba wa taaluma hizo kaunti ya Taita Taveta na kuomba washikadau wa elimu kutilia maanani masomo ya wanafunzi wao.
“Tunashukuru wote serikali ya kaunti kwa kutilia maanani maswala ya elimu. Ufadhili huu tunatumai utakua wa faida sio tu kwetu kama wazazi ila kwa kaunti yetu na taifa zima kwa ujumla kwani taaluma walizochukua ni nyeti na zenye faida kubwa.” Gadiel Kilaghai amesema.
Kumi na sita hao, miongoni mwao wakiwemo wasichana 6 ni kati ya idadi ya 80 kutoka hapa Kenya watakaofadhiliwa na na ubalozi huo.
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
Leave a Comment