Categories: Taita Taveta News

WAJUMBE WAAPA KUTEKELEZA WAJIBU WAO WA UNYAPARA KWA MASHINE MPYA YA UCHIMBAJI MAJI TAITA TAVETA.

Hatimaye wakaaji wa kaunti ya Taita Taveta wamepata sababu ya kutabasamu baada ya serikali ya kaunti hiyo kuzindua rasmi mashine ya kuchimba maji yenye kununuliwa kwa takribani shilingi milioni 45 na inatarajiwa kusaidia pakubwa kukabiliana na changamoto ya kuwepo maji safi ya matumizi, kuongeza kapu la uzalishaji kwa kutoa maji ya unyinyizaji pamoja na kuongeza pato la kaunti hiyo.

Wakiongea wakati wa uzinduzi mashine hiyo mapema hii leo mjini Wundanyi, viongozi wa serikali hiyo wakiongozwa na gavana Granton Samboja wameomba kuwepo mikakati dhabiti kusimamia mashine hiyo ili ifikie malengo yake huku wakitoa tahadhari kwa yeyote anayelenga kuitumia kwa njia zisisofaa kua hataruhusiwa.

“Naomba wizara husika kuhakikisha gari hili linatunzwa na pia kamati husika katika bunge la kaunti zinaweka mikakati dhabiti ili kifaa hiki kiwe cha manufaa kwa mwananchi. Haitakua na faida iwapo tutazindua leo kisha baada ya siku chache liwe limeharibika kwa kukosa kuwajibikiwa. Ni wajibu wetu kama viongozi kuhakikisha raslimali za mwanachi zinatumika kwa umakini.” Gavana Samboja amesema.

Mwenyekiti wa kamati ya maji kwa bunge la kaunti Khamadi Chanzu ameitaja mashine hiyo kama mwamko mpya kwa kaunti kwani itasaidia pakubwa kufidia changamoto zinazozidi kushuhudiwa ikiwemo uhaba wa maji, chakula na kuongeza kuwa wataweka sheria kuhakikisha inatumika kuongeza fedha zinazokusanywa kama ushuru.

“Jimbo hili limekua na changamoto ya ukosefu wa mapato na mashine hii itatumika kama njia ya kutatua swala hilo. Tutabuni sheria kuhakikisha wote watakaoikodisha kibinafsi wanatozwa fedha zitakazosaidia kuongeza mapato tunayokusanya kama ushuru. Naomba wananchi wakumbatie mradi huu kikamilifu.” Mwenyekiti huyo amesema.

Hata hivyo wajumbe wa kaunti hiyo kupitia kamati ya uhasibu na uwekezaji chini ya mwenyekiti wake Anselim Mwadime wameapa kutekeleza wajibu wao wa unyapara kuhakikisha chombo hicho kinatumika kiumakini kufikia malengo hitajika.

“Baada ya kuchaguliwa tuliandaa kikao kama viongozi wa kaunti hii kuangazia maswala tunayofaa kuyapatia kipaumbele na maji ndio ilikua swala kuu. Sisi kama kamati ya uhasibu na uwekezaji tutahakikisha tunatekeleza wajibu wetu wa unyapara ili mashine hii itumike ipasavyo.” Anselim ameeleza.

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na naibu gavana Bi. Majala Mlagui, mawaziri Gasper Kabaka (Maji), Houghton Mombo (Nyumba na Miundomisingi), Bigvai Mwailemi (Vijana, michezo, utamaduni na utalii), Getrude Shuwe (Biashara, ushirika na jinsia), Claris Mnyambo (Ardhi, mazingara na maliaslli), Dkt. Davis Mwangoma (Kilimo, ufugaji, uvuvi na unyinyizaji) pamoja na wajumbe kutoka kamati za maji na ile ya uhasibu na uwekezaji kwa bunge la kaunti hiyo.

David Moto

Leave a Comment
Share
Published by
David Moto

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

18 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago