Categories: Pwani News

WAHESABIWA MASAA KUWAFURUSHA NGAMIA TAITA TAVETA LA SIVYO MWANACHI ACHUKUE HATUA MIKONONI KUMALIZA KERO HILI

 

Kitengo cha usalama mjini Mwatate kaunti ya Taita Taveta kiko na siku saba kuwafurusha Ngamia wanaozidi kuwa kero kwa jamii mjini humo pamoja na mazingara kabla ya viongozi kuwashawishi wananchi kusaka mbinu mbadala kukabiliana na kero la wanyama hao.

Haya ni kwa mujibu wa gavana Granton Samboja ambaye vilevile hajaisaza wizara yake ya ufugaji, pale ameipatia siku mbili kufutilia mbali idhini za kuchungwa mifugo hao kaunti yake na kuongeza kuwa upole wa jamii yake katu haufai kuchukuliwa kama sababu ya kutoheshimiwa na sheria kukiukwa kiholela.

Akiongea kijiji cha MtoMwagodi, Mwatate alipowaongoza wajumbe na viongozi wa kisisa kaunti hiyo kuongelea maswala tata yanayokumba jamii hizo ikiwemo chuo cha Diaspora na mifugo aina ya Ngamia wanaozidi kumiminika kaunti hiyo kutoka kaunti za inje, Samboja ameomba jamii zilizoathirika kuimarisha amani huku asasi za usalama zikiendelea kusaka suluhu la kudumu.


“Naibu kamishna uko na siku saba kuhakikisha ngamia hawa wametolewa kwa mashamba ya mwananchi na iwapo mtashindwa basi nitajua mnakula na wamiliki mifugo hao. Waziri wangu Davis Mwangoma pia wewe sijakusahau, uko na siku mbili kufutilia mbali vibali vyote vya kuchunga mifugo hao kwasababu wizara yako ndio inahusika na upeanaji vibali hivyo.”

Mwishoni mwa mwezi jana, kamishna wa kaunti hiyo Bi. Rhoda Onyancha alielekeza kidole cha lawama kwa wizara ya ufugaji kaunti hiyo kwa kutobuni sheria ya kudhibiti mifugo lutoka kaunti za inje kuingizwa kwenye Ranch za kaunti hiyo hali ambayo imechangia pakubwa kuongezeka kwa maafa yatokanayo na mifugo hao.

Kwenye swala la chuo chenye utata cha Diaspora, Samboja amabaye hii leo alipata uungwaji mkono kutoka kwa wawakilishi wodi wanaopakana na ardhi inayosemekana kutwaaliwa kujengwa chuo hicho, msimamo aliokariri ni kuwa bado haungi mkono ujenzi wa chuo hicho na kuomba wananchi kujiepusha na walaghai wa ardhi.

“Diaspora University hakuna na huo ndio msimamo wa serikali. Kenya ni kubwa mnaweza tafuta mahali kwingine mkawekeza chuo hiko. Naomba wananchi mkue macho na wawekezaji wenye nia ya kuwatapeli mashamba yenu kwasababu wengi wenu ni maskwata na mnahitaji mashamba hayo na sio kuyapeana kwa kuhadaiwa.”

Ann Eghwa Florence

Leave a Comment
Share
Published by
Ann Eghwa Florence

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

18 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago