Taita Taveta County Assembly Clerk - Gadiel Maghanga
Leo alfajiri na mapema, viongozi wa bunge la kaunti ya Taita Taveta waandaa mkutano,ukiongozwa na clerk Bwana Gadiel Maghanga, akisaidiwa, bwana William Sowa na Elizabeth Ngele. Kabla mkutano haujaanza, Clerk aliamurisha sergent at arms kunyangโanya kila mtu simu na kuzifungia kwa sefu.
S๐ฐ๐๐ฅ๐ข ๐ง๐ข ๐ฃ๐, ๐ฐ๐๐ง๐๐๐ข๐๐ก๐ ๐ง๐ข๐งi?
Kwenye mkutano huo, wafanyikazi hao wameonywa vikali kwa kutoa siri za bunge na kumfikia ADMIN wa Kwaela News Network na kuzichapisha hadharani. Bwana Clerk alikasirishwa sana na swala la kuona siri za bunge za kweli zinachapishwa hadharani.
Mheshimiwa Clerk ameongea kwa ukali akisema kuwa siri zinazochapishwa Kwaela News Network hazipaswi kutoka nje ya jengo la bunge, wala kuchapishwa kwenye mtandao ili ziweze kusomwa na umma. Amewaonya wanaotoa habari hizo waache mara moja sababu wakikamatwa wataona cha mtema kuni kwa kuchukuliwa hatua kali ya kuvunja masharti na miiko ya bunge.
Kuona siri za bunge la kaunti zinachapishwa hadharani kumetingisa uongozi wa bunge la kaunti na hivyo kuwafanya kutumia njia tofauti tofauti kutaka kujua ni nani anatoa siri hizo. Kufikia sasa inaonekana bado hawana habari.
Bw. Sowa amedokeza kwamba huenda kuna wafanyi kazi fulani wanatoa siri za bunge na kuwapa MCAs, ambao hakuwataja na kufikishia ADMIN wa Kwaela News Network. Hii ni ishara kuwa hawana habari ni vipi kitoweo kimetumbukia nyongo. Isitoshe basi, Kwaela News Network inaandaa kumuangazia Bw Sowa ambaye ametajwa kwa mlolongo wa masaibu ya ufujaji wa fedha za umma, ufisadi, utepetevu na maovu mengine kadha wa kadha.
Kwenye mkutano huo, Mheshimiwa Clerk ameshindwa kujieleza vizuri hata wafanyikazi wakamshangaa, asilolijua ni kuwa watu wana habari ya maovu yote anayoyafanya chini ya maji. Kwa mfano, Bw. Clerk ameshindwa kueleza ni nini Spika wa Bunge, P.A wake na MCAs kadhaa maeenda kufanya nchini Rwanda tangu wiki jana ilhali wafanyikazi wa kawaida hawalipwi marupurupu yao, kisa hakuna pesa. Pesa za wangwana hawa za kutangatanga zinatoka wapi?
Kwenye mkutano huo wafanyikazi wote wamelishwa kiapo cha kutotoa siri za bunge na kuzifikishia ADMIN wa Kwaela News Network.
Aliyepeane kiapo hicho ni Pastor bandia anayeitwa ๐๐๐จ๐ซ๐ ๐ ๐๐ณ๐ฎ๐ง๐ ๐ฎ ambaye ni Sergeant at Arms bungeni. Duru zinasema kuwa Bwana Mzungu hakumaliza masomo ya shule ya msingi, inasemekana aliachia shule darasa la sita. Wafanyi kazi wa bunge wanashangaa imekuwaje wanaapishwa na mtu ambaye hata kuandika jina lake mwenyewe huwa anatokwa na kijasho chembamba! Mengi zaidi kuhusu Pastor huyu bandia, mwenye kipawa cha kuwatembelea wajane, tutayaweka bayana kwa toleo lijalo.
Kwa haya machache na mengi tunasema ahsante na usiondoke.
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
Leave a Comment