By Carol Korir
Nchini Kenya, wabunge katika Kaunti ya Taita Taveta, wametofautiana kuhusu mswada unaoruhusu utengezaji, uuzwaji na unywaji wa pombe ya kienyeji, inayoitwa Mbagara, wakati huu pombe isiyo na viwango ikiendelea kusababisha maafa nchini humo. Wiki moja iliyopita watu 10 walipoteza maisha baada ya kunywa pombe haramu katika Kaunti ya Nakuru.
Lakini je, pombe hii ya Mbangara inatengezwa vipi ? Mwandishi wetu Carol Korir amerejea kutoka Taita Taveta na ametuandalia ripoti kadhaa kuhusu pombe hii.
Soma Pia: ‘MBOKO’, A TRADITIONAL GOURD USED TO DRINK PALM WINE HARD TO FIND
Safari ya kwenda Taita Taveta inaanzia kwenye kituo cha treni, Syokimau, jijini Nairobi. Baada ya saa tano, njiani tunawasili Wundanyi mji mdogo wa kaunti ya Taita Taveta.
Natembelea vijiji vya Masumbusunye ,Mwangeka na Wesu vionavyoongoza kwenye utengezaji wa Mbagara, nakutana na wanaume kadhaa wakinywa pombe hii.
“ Inabidi tujipange ,haki ya Mungu ,” wanasikika wakisema walevi.
Jimmy ni mgema wa Mbagara, namtembelea nyumbani kwake, anaeleza namna pombe hii inavyoandaliwa .
Soma Pia: TAITA TAVETA MCAS SEEK TO LEGALISE TRADITIONAL BREWS
“ Hapo tuko na sukari ,Pasha(mfano wa khamira) na Wishwa ambayo hutokana na mahindi. Unaanza kwa usafi,unaosha mkono na maji na sabuni ,kisha unaweka maji ya baridi kwenye ndoo ,unachanganya mpaka mseto huo uwe vizuri kisha unaacha kwa siku tatu itakuwa imekuwa tayari,”alielezea Jimmy.
Andrew Mangi, pia mgema yeye, anaanda Mbagara msituni kwa hofu ya kukamatwa na polisi.
“ Huwezi kuuza pombe eti tu hadharani,lazima uwe porini ndo angaa uuze kidogo ,maisha yamekuwa magumu kweli ,”alisikitika Andrew Mangi.
Baada ya kuwa tayari, Mbagara inauzwa Shilingi za Kenya 25 sawa na Dola za Marekani 0.23. Wanaume hawa wanaeleza ni kwanini wanaipenda pombe hii.
“ Ni nzuri kuliko hizo pombe zingine ,haswa vikali,”alisema mmoja. Akaongezea mwenzake , “ Hi ndo imenilea ,napenda sana,”alisema mteja kwa jina Basanga.
Naye mwenzake akiendelea kupata kiburudisho ,” hii ni kama kufungua akili.” Akamalizia mwenzake, “ Hapa tuko vizuri ,unatoa lock kisha unaingia shambani.”
Lakini je, ni kwanini Mbagara inauzwa na kunywewa kwa siri ? Ungana nami katika ripoti zinazofuata , kuhusu mjadala tata katika Kaunti ya Taita Taveta ya kuhalalisha pombe hii.
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
Leave a Comment