Categories: Taita Taveta News

UKISTAAJABU YA MUSA, YA WAFUASI WA SAMBOJA YATAKUMALIZA

Katika pilka pilka za kumkaribisha waziri wa wizara ya maji kutoka serikali kuu Bwana Simon Cherugui, katika kaunti ta Taita Taveta siku ya Jumatano tarehe 21/03/2018, ilipendekezwa kuwa maandalizi ya mlo yafanyiwe katika shule ya msingi ya Kighombo, ilioko kati wadi ya Rong’e.

Madhumuni ya waziri Cherugui kuzuru kaunti hii yetu ilikuwa ni kuzindua mradi wa maji katika shule ya wasichana ya Mwasere, na mradi huo ungewafaa wanafunzi na wakaazi wa rong’e kwa ujumla. Sherehe hii ilikusudiwa kufanyika tarehe 22/3/2018.

Kizazaa kilianza wakati Bi Kawuki ambaye alikuwa kama msimamizi wa maandalizi ya mapishi ambayo yalidhumuniwa kwa gavana Samboja pamoja na wageni wake, kumshurutisha mwalimu mkuu wa shule ya Kighombo Bwana Idawo kuwa atatumia darasa kuandaa maamkuli hayo, jambo ambalo Bwana Idawo hakukubaliana nalo akiashiria kwamba darasa hilo haliwezi tumika kupikia sababu lilipakwa rangi karibuni na pia kuna jiko maalum ambalo wanaweza kutumia kuandaa vyakula vyao.

Darasa kutumiwa kama jiko la kuni

Jambo hili lilimkera Bi kawuki na kusababisha kumtupia mwalimu mkuu huyo cheche za matusi huku akinukuliwa akisema,

“sisi ni watu wa county na sisi ndio wenye serikali. Tutafanya tutakalo. Na kama watu wa Samboja tumeamua kwamba tutatumia darasa kupikia chakula hicho. Unaweza hata ukafutwa kazi kwa hivyo ni vizuri ujifunze kuheshimu mamlaka na hasa gavana Samboja. Sisi team mshapa hatupendi ujinga, na kama huamini utajua sisi ni akina nani.”

Bwana Idawo naye hakusita ila kumweleza bi Kawuki kuwa, haoni shida yoyote chakula kupikiwa kwa shule yake, lakini kutumia darasa na ilihali kuna jikoni mahali maalum ambapo wanaweza kupikia vyakula vyao. Bi kawuki alioneka kutotaka kujibizana na bwana Idawo tena ila kuchukua simu yake ya rununu na kumweleza mwalimu mkuu kwamba atajua kwamba anapingana na serikali yaaani kwa lugha ya mtaani utajua hujui.

Bi Kawuki alipiga simu na baada ya dakika chache gari lenye sajili ya kaunti lilifika na ndani alikuweko Bwana Edward Mwakisima.

Kamati ya upishi

Bwana mwakisima alionekana kuwa na hamaki na kumuuliza Bwana Idawo kuwa,

“je wewe ndiye unaetukana gavana? Una akili timamu wewe?”

Hata kabla ya bwana Idawo kujieleza alipigwa mengo na kuanguka chini huku ngumi na mateke yakifwatana mfululizo.

Bwana Mwakisima alieleza kwa sauti kubwa yenye hamaki kuwa hatakubali mtu yeyote kumdhalilisha gavana Samboja na takaye jaribu ataona cha mtema kuni, huku akijigamba kwamba hakuna atakaye mfanya lolote wala kumpeleka popote.

Baada ya mwalimu kupewa kichapo cha mbwa kuingia msikitini, Bwana mwakisima alirudi kwenye gari lake na kuondoka huku mwalimu mkuu akiachwa na majeraha na kuuguza maumivu.

Kesho yake ambapo ndio sherehe kamili, siku alhamisi 22/03/2018, mheshimiwa gavana Samboja ama kwa jina la mtaani mshapa aliwasili katika kijiji cha kighombo pamoja na mgeni wake wa heshima kuzindua mradi wa maji, ila kinacho washangaza wakaaji wa kighombo ni kwamba mshapa hakulizu ngumzia juu ya mkasa huo uliofanya na mtu wake na rafiki wa karibu bwana Mwakisima.

Inawezekana kuwa habari hizo hazikumfikia Gavana Samboja? Wakaazi wa kighombo wanahisi kuwa mwalimu wao alidhalilishwa na wanaomba sheria kuchukua mkondo wake.

Upishi Darasani

Hata hivyo kufikia sasa bado Bwana Mwakisima yuko huru na anaonekana kutumia magari ya county popote aendapo.

Swali ni jee, huenda ikawa mkaaji wa kaunti ya Taita Taveta haturuhusiwi kupinga lolote linalomhusu mshapa?
Na ikiwa utapinga, basi kando na kichapo kikali yepi zaidi tunatarajia kutoka kwa mashabiki wa mshapa?

Ikiwa ubinafsi, majivuno na ubabe ndio tunaonyeshwa na wafuasi wa Samboja hata kabla ya kumaliza mwaka mmoja mamlakani, ni yapi haswa yamesali?

Tunaomba haki itendeke haraka iwekekanavyo!

Madharau yaliyoachwa baada ya upishi darasani
Kwaela News Network

Leave a Comment

View Comments

Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

18 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago