Categories: Taita Taveta News

UBADHIRIFU WA FEDHA ZA UMMA KATIKA OFISI YA NG-CDF YA TAVETA

Katika eneo bunge la Taveta, mwaka wa fedha wa 2024/2025 umejaa utata na maswali mengi kuhusu matumizi ya fedha za umma. Takwimu za bajeti zilizowekwa kwenye tovuti rasmi ya NG-CDF zinaonyesha wazi kuwa kuna ulaghai unaoendelea.

Kwa mfano, gharama za kuunganisha mtandao zimeongezeka kutoka Sh80,000 mwaka uliopita hadi Sh150,000 mwaka huu. Je, ni nini kimebadilika ghafla na kufanya gharama hizi kupanda mara dufu? Hii ni ishara ya wazi ya matumizi mabaya ya fedha za umma.

Pia, bajeti inaonyesha kuwa Sh120,000 zimetengwa kwa ajili ya kununua tangi la maji la lita elfu kumi. Je, bei hii iko sawa ama imeongezwa kama ile ya mashine ya kuchapisha iliyonunuliwa kwa Sh2.5 milioni? Cha kushangaza ni kuwa, hadi sasa, wahusika hawajatoa namba rasmi ya usajili ya mashine hiyo ili kuthibitisha gharama yake.

Wakaazi wa Taveta na Wakenya kwa jumla wanapaswa kuwa macho na kuhoji matumizi haya ya fedha. Kwa mfano, mbunge Bwire ametenga Sh12 milioni za kununua mabasi mawili kwa shule za Bishop Njenga na Eldoro Girls. Wazazi wa Bishop Njenga wanapaswa kuongezea Sh5.5 milioni ili kununua basi la Isuzu FTR lenye viti 51, na wazazi wa Eldoro wanapaswa kuongezea Sh4.5 milioni kwa basi la Isuzu FRR lenye viti 46.

Upekuzi wa haraka kwenye mtandao unaonyesha kuwa mabasi ya aina hizi hugharimu chini ya Sh8 milioni yakiwa mapya. Je, fedha hizi za ziada zinaenda wapi? Ni wazi kuwa kuna ulaghai mkubwa unaoendelea.

Cha kusikitisha ni kuwa, licha ya wazazi kuchanga fedha zote hizo, mabasi hayo yakifika mashuleni, wabunge ndio hupongezwa na kumiminiwa sifa, ingawa hawana mchango wowote kwenye mradi huo.

 

Ni wakati sasa kwa raia wa Taveta na Kenya kwa jumla kuwa makini zaidi na kukagua takwimu za mgao wa fedha zetu ili kuhakikisha zimetumika ipaswavyo. Hatupaswi kukaa kimya tunapoona fedha za umma zikibadhiriwa.

Mwachere Shuma

Leave a Comment
Share
Published by
Mwachere Shuma

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

18 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago