Unapomtupa jongoo kweli unapaswa kumtupa na mti wake. Haya yanadhihirika wazi katika kaunti ya Taita Taveta, baada ya upelelezi wa kina wa sajili ya wafanyikazi wa kaunti. Usajili huu umeitishwa na Gavana Andrew Mwadime ili kufichua uozo na ufisadi unaodunisha utendakazi katika kaunti hiyo kwa kuajiriwa wafanyikazi wasiohitumu na ghushi. Licha ya kua halijakamilika, zoezi hilo limeanza kupigwa vita na baadhiya ya wafanyakazi hao kutoka idara mbalimbali.
Kwa kile kinachobainika kua kisa halisi cha mfa maji asiyeacha kutapa, licha kuomba kusamehewa ‘kupe‘ hao, wanaofyonza uchumi wa kaunti, wanaojulikana mitaani kama ‘Mayatima wa Mshapa’ wanazidi kuhujumu utendakazi katika kaunti hio. Jambo hilo limeonekana kama limesitisha na kuzuia kasi ya maendeleo tangu uchaguzi mkuu kufanyika.
Akijadili mada hio, mwakilishi wadi wa Ronge Mhe. Dorcas Mlughu aligusia swala hilo na kukashifu vikali vikwazo vinavyoibuka pasipo msingi kwenye kaunti hio. Kwa ghadhabu ya upendo, aligusia ukosefu wa maendeleo, maji, huduma bora za afya kwenye kaunti hio na kusitishwa kwa miradi ya maendeleo haswa ya barabara.
Hili likiwa limejiri wakati wakaazi na watumizi wa barabara ya Bura – Mgange – Werugha – Mbale – Msau – Mtomwagodi wakiitisha uchunguzi thabiti kwa kusitishwa kwa mradi huo wa ujenzi wa barabara ta kilomita gamsini na nne. Kulingana na mbunge wa Wundanyi, Mhe. Danson Mwashako, mradi huu ulitengewa kitita cha hela cha shilingi Bilioni 2.2 ambazo kufikia sasa, hela hizo hazijulikani ziliko. Duru zisizo aminika, zinadai kuwa huenda hela hizo zichafujwa na wangwana tajika katika serikali iliyopita.
Akihakikishia wananchi wingi wa maendeleo kama alivyoahidi kwenye manifseto yake, Gavana wa kaunti hiyo alionekana mcheshi na mchangamfu baada ya kuitia sahihi orodha ya waziri na maafisa wakuu kuhudumu katika idara mbali mbali kaunti hiyo. Maafisa hao wanakusudiwa kupigwa msasa na vikao vya bunge la kaunti ili kuweza kuhudumu katika nafasi walizopewa.
Kweli Msafiri ni aliye bandarini huku Taita meli ya Amani ,Upendo na Maendeleo imeng’oa nanga.
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
Leave a Comment