Categories: Taita Taveta News

TAITA TAVETA : SIASA ZA MASHINANI

Tetesi kuwa Gavana wa Taita Taveta Granton Samboja amekitema chama cha Wiper ambacho kilimdhamini katika uchaguzi wa 2017, zimeleta hali ya utata na kuzua tumbo joto kwenye ulingo wa kisiasa katika kaunti hiyo.

Kuhama chama

Hali hiyo imesababisha wanasiasa na wakereketwa wa kaunti hiyo kuanza mikakati ya kujipanga upya kimirengo ya kisiasa. Wanaounga mkono Gavana huyo kujiunga na ODM, wanadai kuwa alikuwepo ndani ya chama hicho kilipozinduliwa, na kuwa yeye ni baadhi ya wafadhili asili wa chama hicho katika kaunti ya Taita Taveta, hivyo basi ana haki ya kuwa mwana chama.

Kwa upande mwengine, wanaopinga kujiunga kwake wanadai kuwa kutaharibu sifa ya chama cha ODM, kwa sababu chama hicho kinatambulika kwa maadili mema na kuthamini wasomi na elimu kwa jumla. Samboja – ambaye ameandamwa na shutuma za ugushi wa stakabadhi zake za elimu alizoziwasilisha kwa IEBC na ambazo zilimwezesha kugombania kiti hicho cha ugavana – ameshtakiwa na mpiga kura mmoja katika kesi ambayo bado haijakamilika.

Njia panda

Kufuatia hayo, inasemekana mwanasiasa mashuhuri aliye pia mweka hazina wa chama cha ODM katika Kaunti ndogo ya Taita amejikuta katika njia panda. Mwanasiasa huyo alikuwa mfuasi na mtetezi sugu wa serikali ya awamu ya kwanza iliyoongozwa na mhandisi John Mtuta Mruttu.

Aliyekuwa Gavana wa Kwanza wa Taita Taveta, Mh. John Mruttu pamoja na Debora Wakesho matangani Taveta.

Hata hivyo, uchaguzi ulipokaribia Mwaka wa 2017, Mwanadada huyo alikihama kikosi cha Mhandisi John Mruttu na kujiunga na kikosi cha aliyekuwa mbunge wa kaunti ndogo ya Taita mheshimiwa Thomas Mwadeghu. Duru zinasema kwamba, mwanadada huyo alivuka sakafu alipoahidiwa kuwa endapo Mh. Mwadeghu angeshinda ugavana basi angeteuliwa kama MCA wa chama cha ODM katika bunge la kaunti.

Uteuzi huo wa MCA ulipomchenga mwanadada huyo, aliamua kuwa baridi na njaa ya “kukaa nje” kwa miaka tano ni hali ambayo hangeweza kustahimili. Yeye, pamoja na wakereketwa wengine, waliamua kujiunga na timu ya kumpigia Samboja debe – almaarufu “Olele Boys Band” – jambo ambalo liliwaudhi wafuasi wengi sugu wa ODM katika Taita Taveta.

Kwa muda sasa, wafuasi hao sugu wa ODM, wamekuwa wakilalamika kwamba ujio wa Samboja kwenye chama chao si baraka ila ni laana ambayo italetea chama hicho balaa na karaha. Isitoshe, haijulikani ni cheo gani au mamlaka gani ambayo Gavana Samboja amemiliki kwani amejiingiza “kwa kupitia mlango wa nyuma” kwa njia isiyo rasmi. Yeyote aliyethubutu kuonyesha kukereka kwake kwa jambo hilo alichukuliwa kuwa adui na kushambuliwa na kuharibiwa jina na ‘Olele Boys Band” kwenye mitandao na redio inayomilikiwa na Gavana huyo. Mhe Jason Tuja, ambaye ni mwakilishi wa Kaunti ya Werugha katika Baraza la Kaunti hiyo, ni mmoja wa viongozi wa ODM ambao inasemekana Samboja hakupoteza muda kumvuruga pindi tu alipojiingiza ndani ya chama hicho. Hivi majuzi, Tuja alitimuliwa kutoka kwa uongozi wa Bunge hilo la Kaunti – jambo ambalo mwanadada mweka-hazina, tuliyemwangazia hapo awali, alilishabikia kupindukia!

Gavana Mruttu akifariji waombolezaji

Inasemekana kwamba viongozi wengine wa ODM wameapa kuhakikisha kuwa chama chao hakitatekwa nyara na watapeli wa kisiasa. Wachanganuzi wa kisiasa wanahoji kuwa ni jambo la wazi kuwa chama hicho cha ODM tayari kimesha gawanyika na kitasambaratika baada ya muda usio mrefu.

Ghadhabu ya wapiga kura

Hivi majuzi, Samboja, ambaye hutoka Wadi ya Werugha, alighadhabisha wakina mama na wakazi wa Taita Taveta kwa jumla, kwa kumteua mwanamume anayetoka huko huko Werugha, kuwa Director wa maswala ya Kina Mama katika kaunti hiyo!

Juma lililopita Samboja alijitokeza akilalama kwamba hana hela ya kufanya maendeleo kwa sababu inamlazimu kutumia mgao wake wote kulipa madeni ya wanakandarasi wanaodai kaunti hiyo. Hali hii imekwamisha maendeleo mengi, hasa katika sekta za maji, afya na zenginezo – na kubakisha shughuli ya kulainisha mabarabara – pesa ambazo zinachangiwa na “Fuel levy” – kuwa maendeleo ya pekee ambayo yanayopigiwa debe kwa wakati huu. Hii ndio sababu ya kuona wawakilishi wa Gavana mashinani, wajulikanao kama Ward Administrators, huangazia “maendeleo” ya barabara kila kukicha!

Dukuduku zetu zinatuarifu kwamba “mwanadada-mwanasiasa” wetu tayari ashanukiwa kwamba ifikapo 2022 Samboja na timu yake “wataoshwa” katika uchaguzi mkuu, kupitia kwa ghadhabu ya wapiga kura. Inasemekana kwamba tayari ameanza kurudisha urafiki wake wa kisiasa “chini ya maji” na aliyekuwa gavana wa kwanza ili angalau asiachwe kwenye baridi endapo serikali ya Samboja itatimuliwa.

Chama cha Wiper

La kustaajisha ni kuwa, kwa upande mwengine, viongozi wa chama cha Wiper, kinyume na dhana ya kuwa wametatanishwa na kuhamia kwa Samboja kwa chama kingine, wengi wafurahia jambo hilo, ila wanaficha furaha yao kwa kumuogopa Gavana huyo. Hili linatokana na hofu yao kuwa utenda-kazi wa Samboja umekuwa na dosari chungu nzima, hivyo kwamba chama cha Wiper, pamoja na wagombezi wote wa chama hicho, wangeumizwa na “mzigo” wa kuhusishwa au kubeba jina la Samboja katika uchaguzi wa 2022.

Kiongozi mmoja, ambaye jina lake tumelilibana, alisikika hivi majuzi alipoulizwa juu ya maoni yake kuhusu uasi wa Samboja kwa chama cha Wiper, akajibu “sisi tunasema halleluya!”

 

 

Kwaela News Network

Leave a Comment

View Comments

  • Waliosema siyasa Ni maslahi Kumbe hakukosea.sisemi kitu but msimamo nikitu mhimu sana.samboja tutampa Tano ingine tena

Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

17 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago