Serikali ya kaunti ya Taita Taveta imewalaumu vijana kwa kutotuma maombi ya kuitisha fedha za ustawishaji miradi yao kutoka kwa serikali, hatua ambayo imechangia pakubwa fedha hizo kurejeshwa serikali kuu kila mwisho wa mwaka wa kifedha.
Gavana Granton Samboja ameomba baraza lake la mawaziri kuweka mikakati kufufua mpango wa DaTu sawazisha , fedha ambazo zimekua zikitengwa na serikali ya kaunti hiyo kuwawezesha kina mama, vijana na walemavu huku akiomba wote waliohepa na mikopo hiyo hapo awali kufatiliwa.
“Vijana tuwache kuogopa kuwasilisha maombi ya kuitisha fedha hizi na hiyo ndio njia tutaweza kusaidika kama jamii na baadae fedha hizo hazitarudi kwa serikali kuu. Waziri Bigvai na wenzako naomba muweke mikakati ili hazina ya DaTu sawazisha irejeshwe. Wale wamekataa kurudisha pesa walizochukua naomba wafanye hivyo kwa haraka ili zisaidie wengine,” Samboja amesema.
Akiongea mjini Bura alipoongoza sherehe za kuzindua josho la Sanga, Samboja aidha ameapa kuwafurusha maafisa wa serikali yake ambao wamejitolea kuwatapeli wananchi kwa kuwatoza ada za juu za utoaji huduma za utungaji ng’ombe mimba kwa kile alichokitaja kama kulemaza maendeleo.
“Waziri Mwangoma ni jukumu letu kama serikali kuhakikisha tumetoa mafuta ya pikipiki kwa maafisa hawa kufikisha huduma za AI hadi mashinani lakini ninaapa kukabiliana na baadhi ya maafisa wako ambao wameamua kutapeli wafugaji kwa kuitisha pesa zaidi ya shilingi 200 tulizopitisha. Ni sharti tusaidie wakulima na sio kuwanyanyasa,” Amesema.
Wakati huohuo ameomba wananchi kujiandikisha kwa bima ya afya NHIF ili waepukane na gharamaza juu za matibabu na kukariri kua serikali yake iko imara kuimarisha sekta ya afya na kuongeza kwamba atazidi kushirikiana na serikali kuu kufanikisha agenda nne kuu, huduma za afya zikiwa moja wapo.
Naibu wake Bi. Majala Mlagui amewataka wananchi wanaopakana na mbuga za wanyamapori kuondoa hofu msimu huu wa upanzi baada ya idara ya KWS kuanza mpango wa kuweka ua eneo la Mwatate.
Samboja aliandamana na mawaziri kadha wakiwemo Bigvai mwailemi (michezo, vijana na utalii), Janet Mwawasi (Huduma za uma na utawala) na Claris Mnyambo wa ardhi, mazingira na mali asli pamoja na mwakilishi wodi wa eneo hilo Patel Mng’ambwa.
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
Leave a Comment