Gavana Samboja akizindua George Faraji Dispensary huko Werugha
Hakuna mtu yeyote katika ulimwengu huu asiyejua umuhimu wa kutunza mazingara yetu kwa manufaa ya vizazi vijavyo – ikiwemo watoto wetu, wajukuu, vitukuu, vilembwe… na pia kwa manufaa yetu wenyewe.
Athari na majanga mengi kama vile ukame, mvua ya masika, kubadilika kwa misimu, kukauka kwa mito, kuenea kwa majangwa, kuzuka kwa magonjwa mapya yasiyo na tiba…yote yana uhusiano mkubwa na shughuli za mwanadamu zinazoharibu mazingara – shughuli kama vile kulisha mifugo na kulima mahali pasipofaa, (kama vile kwenye hifadhi za maji), kuchafua anga kwa moshi na hewa kutoka kwa viwanda, na ukataji wa miti kiholela.
Hii ndio sababu kubwa ya mababa na mababu zetu kuhakikisha kwamba, tangu jadi, waliishi na kutumia rasilmali zao bila madhara au uchafuzi wa mazingara.
AHADI YA SAMBOJA
Wakati akiomba kura ya ugavana mwaka wa 2017, mojawapo ya ahadi ambazo alitoa kwa wananchi katika manifesto yake ni kwamba (na ninamnukuu) :
“Nitahifadhi na kudumisha mazingira”.
Ahadi hii ni moja ya sababu kuu ya wapiga kura wa Taita Taveta kumpa Samboja kura zao, kwani waliamini ya kuwa mazingara yao yatasalia kuwa kwenye mikono “ya kuaminika” ya Gavana-mtarajiwa Samboja. Haikuwa vigumu kwa Samboja kuwashawishi wapiga-kura wake, kwani hotuba zake na za wahubiri wa kidini hazikuwa na tofauti kwa vile alikuwa stadi kwa kuingiza vifungu vya Biblia Takatifu na Tenzi za Rohoni katika semi zake zote. Na kweli, baada ya kura kupigwa, Bwana alimwandalia Samboja meza “mbele ya watesi wake” kwa kumpatia ushindi, akawa Gavana.
WANAKIJIJI WA SAGHASA
Wanakijiji wa Saghasa, wakiongozwa na Chifu Rashid wa Werugha, eneo analotoka Gavana Samboja, kwa miaka mingi wamehakikisha kwamba wamelinda na kudumisha mazingara yao – kama anavyohubiri Samboja na inavyo himiza serikali kuu. Wananchi hao wamekuwa mstari wa mbele kwa upanzi na utunzi wa miti, pindi tu miti hiyo inapokomaa na kukatwa kwa manufaa ya jamii nzima.
Hali hii imeelekea kuipatia Werugha na Taita kwa ujumla, mazingara mazuri yenye misitu ya kupendeza, mito na hewa safi.
MIRADI YA MAENDELEO
Kwa kawaida, kwa kuwa miti ya jamii (mtengo) hupandwa na kutunzwa na wananchi wote kwa jumla, miti hiyo inapokatwa, wananchi wa eneo hilo hupatiwa fidia ya aina fulani ili kuwatia motisha. Fidia hiyo huingia kwenye kikapu cha kijiji kizima. Hilo ndilo wakazi wa Saghasa walitarajia baada ya miti yao kukatwa na mbao zilizopatikana zikatumika kwa mradi wa VTC huko huko Saghasa.
Ukweli ni kwamba wananchi wote wa Saghasa wanafurahia mradi huo ambao una manufaa kwa watoto wao. Vilevile, hawana shida na mradi wa George Faraji Dispensary uliozinduliwa juzi, kwa kuwa utaimarisha hali yao ya kiafya – hata ingawa hawakuhusishwa kwa jina lililopewa mradi huo. George Faraji ni jina la marehemu baba wa Gavana Granton Samboja.
Lililowakera wakazi hao wa Saghasa ni kwamba miti yao ilipokatwa, hawakupewa fidia ya aina yeyote. Kikapu chao cha kijiji kikabaki kitupu. Walipolalamikia jambo hilo, Gavana Samboja alimtuma msaidizi wake, Bw. Wilfred Mwalimo, ambaye aliwaambia wanakijiji hao kwamba “masawi” yaliyobaki ndiyo wangetumia kama kuni na wasitarajie malipo yeyote. Mwakilishi wa Gavana katika wodi ya Werugha ajulikanaye kama Savalanga, aliwaghadhabisha wananchi hao zaidi kwa kuwaambia kwamba yeye ameamua jinsi mbao hizo zitatumika na hivyo ndivyo itakavyokuwa. Jambo hilo lilipomfikia Chifu Rashid, lilimuudhi na akaamua kuwa mstari wa mbele kutetea haki za wananchi wake.
SAMBOJA ABOBOKWA
Jumamosi iliyopita, tarehe 1 Agosti 2020, katika sherehe ya uzinduzi wa mradi wa George Faraji Dispensary, Gavana Samboja alishangaza wananchi wote katika sherehe hiyo kwa kutokwa na cheche za maneno ya kumshambulia Chifu Rashid mbele ya umma. Kulingana na Samboja, Rashid amekuwa “akipinga maendeleo yote Samboja anayoleta kwa manufaa ya wananchi”. Isitoshe, Samboja alaiendelea kwa kumkejeli Rashid ya kwamba “ana watoto wengi”.
Ilikuwa fedheha na aibu, hasa kwa wageni kutoka nje, pamoja na watoto, kumuona Gavana wao akifoka na kuropoka hadharani, akimlimbikizia lawana Chifu wao, ambao alichukuwa msimamo sawa na jamii yote kwa jumla. Mwananchi mmoja alisikika akisema “tulikosea kumchagua huyu mtu (Samboja) lakini chuma chake ki motoni kikingojea uchaguzi wa 2022. Kwa sasa tutamvumilia kwa hizi siku zilizobaki, ila kwa sasa tuko ‘Salama rohoni zetu!’”
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
View Comments
Samboja nivizuri viongozi kua na hekima uko na office ungeita chief huko ,kumbuka wewe ni jicho taita na chief ni jicho la serekali kuu.