Tulikuwa wateja wa kampuni moja ijulikanayo kama RAFIKI IMARA HOLDINGS LIMITED kwa kikundi kimoja cha wakulima kijulikanacho kama TUPENDANE – MLONDO hapa Werugha, tangu mwaka wa 2023 na kutokana na ugumu wa kupata fedha na uchumi wa taifa, tukaamua kuwachana nao mwaka huu tarehe 20/2/2025 baada ya kulipa mikopo yote waliokuwa wanadai wanachama. Hivi basi tuliwapelekea barua zetu za kuondoka kwa chama pamoja na vijitabu vyao(passbooks) ofisini mwao Voi tarehe 20/2/2025 na wakavichambua kwa kina kuthibitisha hakuna mwanachama amesalia na deni lao.
Baada ya kuthibitisha kuwa hawatudai, walituahidi kuwa wataanza kurudisha AKIBA zetu ambazo ni takriban jumla ya shilingi 180,000, nazo zilikuwa zitumwe kwa kila mwanachama kupitia M-PESA baada ya miezi miwili tokea tarehe hiyo 20/2/2025 ambapo tarehe kamili ya ya kurudishiwa Akiba zetu ingekuwa kwanzia tarehe 20/4/2025. Japo hadi sasa hawajatimiza ahadi hii. Tumejaribu kuwasiliana nao kwa simu mara kadhaa ila aidha watudanganye au wakose kushika simu zetu.
Kutokana na hili tunaona kuwa baadhi ya kampuni kama hizi zinazokuja jimboni mwetu la Taita-Taveta kufanya biashara ni MATAPELI na tunaomba ofisi husika za Kaunti hii yetu wawe na utaratibu wa kuwawekea Sheria kali kampuni kama hizi kabla ya kuwapa vibali vya kufanya biashara kwetu.
Nawaomba nyie KWAELA NEWS NETWORK mliweke hadharani swala hili kwani kulingana na vile uchumi umedhoofika unaumiza ukitapeliwa ma elfu ya pesa.
Ahsante
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
Leave a Comment