Wakazi wa Kaloleni wameshtushwa na tukio la kushangaza ambapo nyumba ya Mheshimiwa Azhar Din, Mwakilishi wa Wodi ya Kaloleni, imewekewa uzio (fence) na Shirika la Makonge, ambalo linadai kwamba ardhi anayokalia ni yao kihalali.
Picha kutoka eneo hilo zinaonesha ua hilo likiendelea kujengwa huku baadhi ya mashine na wafanyakazi wakiendeleza kazi kana kwamba ni eneo la taasisi ya serikali au shirika. Hali hii imeibua maswali mengi miongoni mwa wananchi wanaoshangaa ni vipi kiongozi aliyechaguliwa hajalindwa wala kujitetea, hadi kufikia hatua hiyo ya aibu.
Wakazi wasema: “Kama MCA ameshindwa kujitetea… sisi je?“
Wakazi wameeleza hofu yao wakisema iwapo mwakilishi wao wa wodi mwenye ushawishi bungeni ameshindwa kutetea haki yake ya kumiliki ardhi, basi wao, wananchi wa kawaida, wana nafasi gani katika vita vya ardhi vinavyoendelea?
Kauli hizi zimechochewa zaidi na mzozo unaoendelea katika maeneo kama Mkamenyi, ambako kuna taarifa za njama za kuwaondoa wakaazi katika ardhi wanayoishi kwa miongo mingi. Wananchi sasa wanahoji:
“Ikiwa Azhar Din amenyamaza kuhusu nyumba yake mwenyewe, atawezaje kuwatetea wananchi wa Mkamenyi wanaokabiliwa na hatari ya kutimuliwa?”
Wito kwa viongozi: Tuchague watetezi, si watazamaji
Wito umetolewa kwa viongozi kuamka na kuonyesha uthabiti katika kutetea haki za wananchi. Tukio hili limetajwa kuwa funzo kwa wapiga kura kuhoji uwezo wa viongozi kabla ya kuwapa mamlaka ya kisiasa.
Kwa sasa, macho yote yameelekezwa kwa Mheshimiwa Azhar Din kusikia atakavyojibu au kuchukua hatua, huku wananchi wakisubiri kwa hamu kuona kama ataweza kutatua mzozo huo na kulinda heshima ya ofisi yake na wodi anayoiwakilisha.
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
Leave a Comment