Muktasari wa Habari
Kuna mgogoro wa mashamba unaendelea katika sehemu ya Mgheno – Mwatate. Inadaiwa kuwa bwana mmoja Paul Olang’o, anayefanya kazi katika shirika la Community Land Action Now (CLAN) anashirikiana na baadhi ya viongozi wa Taita Taveta kufanya uhalifu wa mashamba huko Mgheno.
Katika Community Land ya Mgheno, ( ingawa bado haijapata cheti miliki cha ardhi yao), kwa mfano, bwana huyu pamoja na viongozi kadhaa wa Kaunti ya #TaitaTaveta kutoka idara ya ardhi na wa bunge la Kaunti waliingia kwenye shamba hilo na kuweka beacons bila kuhusisha wana chama wala uma, kwa madai ya kufanya Land Demarcation ili wenyewe wapate #TitleDeeds. Kikosi hicho kiliongozwa na Bwana Okina, Mchombo wakiwa na mamlaka kutoka kwa madam DCC wa Mwatate, ambaye alikuja juzi tu, hata hajamaliza mwaka, ni kama alitumwa huku kuja kutuvuruga.
Swali ni je, kulingana na wao, wenye shamba ni akina nani ikiwa wanachama na wakaazi hawakuhusishwa?
Baadae kulipangwa njama ya kupindua kamati ya wanachama wa mgeno kisirisiri ila njama hizo ziligunduliwa na uchaguzi wao ukazimwa kortini. Kesi bado inaendelea. Baadhi ya waliopendekezwa kuingizwa katika kamati kisirisiri ni pamoja na Engineer Elija Mwandoe, aliyekuwa CECM – Public Works kwenye serikali ya kwanza ya kaunti hii.
Engineer Mwandoe na kikosi chake wanatoka sehemu ya Saghalla – VOI, na bado wanataka kumiliki ardhi Mwatate.
Katika harakati zao za kutaka kupindua uongozi wa Mgheno Commuinty Committee, wamekuwa wakifanya mikutano ya siri na tumeweza kupata nukuuu za moja kati ya mikutano yao.
Kwenye nukuu za mkutano huo, ambazo zimetajwa kama STRICTLY CONFIDENTIAL – NOT FOR PUBLIC CIRCULATION, waliohudhuria ni kama ifwatavyo:-
Meeting Resolutions
Legal representatives Selected
Wana Mgheno Community Land wanalilia haki ya ardhi yao.
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
Leave a Comment