Categories: Reviews

NI NANI HUYU KIONGOZI?

 

Kadiri upepo wa Uchaguzi Mkuu wa 2027 unavyokaribia, watu wa Kaunti ya Taita Taveta wanapaswa kusimama kidete na kutafakari kwa kina juu ya aina ya kiongozi tunayetaka kumpa hatamu za uongozi wa kaunti yetu pendwa.

Tumeshuhudia mara nyingi imani tulizoweka kwa makosa zikigeuka majuto; tumelia kwa sababu ya ufisadi, tumekata tamaa kwa sababu ya ahadi hewa, na tumetishwa na ulafi uliofunga maendeleo yetu minyororo.

Safari hii, tusifungwe macho na ukabila, porojo, wala zawadi za muda mfupi; tuangalie kwa macho ya hekima na mioyo ya ukweli. Tuwapime viongozi wetu kwa mizani ya uadilifu, maono, ujasiri, na moyo wa dhati wa kuhudumia watu.

Maswali haya yafuatayo si maneno matupu, bali ni kioo cha nafsi za viongozi wote wanaotamani kuongoza Taita Taveta kuelekea haki, ustawi, na mabadiliko ya kweli.

1. Ni nani huyu kiongozi jasiri, asiyeogopa miguu ya tembo wa ufisadi, anayeweza kuvunja minyororo ya upendeleo na kupinga siasa za maigizo ambazo zimekita mizizi katika Serikali ya Kaunti ya Taita Taveta?

2. Ni nani aliye tayari kupambana na ugonjwa wa ufisadi kwa moyo wa uzalendo kwa:

i) Kurejesha kila senti iliyopotea tangu enzi za serikali za kwanza, za pili na za tatu;

ii) Kuwafikisha wahalifu wote mahakamani bila kuogopa vyeo wala jina;

iii) Na kuhakikisha mali yote ya umma iliyoliwa inarudishwa kupitia mali za wahusika?

3. Ni nani atakayekuwa na ujasiri wa kufichua orodha za wafanyakazi hewa, na kuokoa fedha za wananchi zinazopotelea mifukoni mwa wachache?

4. Ni nani huyo kiongozi safi kama kioo, asiye na doa la kashfa, anayeweza kulinda ardhi zetu, mashamba, mito, na madini yetu dhidi ya wanyang’anyi wa rasilimali bila woga wala unafiki?

5. Ni nani mwenye uzoefu wa kweli wa kuendesha serikali yenye nidhamu, kasi, na uwazi, serikali inayofanya kazi kwa wananchi, si dhidi yao?

6. Ni nani mwenye upeo wa kimataifa na mitandao ya maana ya kuvutia wawekezaji watakaofufua uchumi wetu, kufungua viwanda, na kuleta ajira kwa vijana wetu?

7. Ni nani huyu anayeweza kushika bajeti ya mabilioni bila tamaa ya kujinufaisha, bali kwa moyo wa uwajibikaji na uwazi?

8. Ni nani aliyejaribiwa na kuthibitishwa katika kuboresha elimu na afya, kuhakikisha hospitali zina dawa, shule zina miundombinu bora, na watoto wanapata matumaini ya kesho njema?

9. Ni nani anayeweza kuamsha kilimo chetu na ufugaji wetu katika mashamba makubwa ya kaunti, ili tufaidi masoko ya kimataifa na kuinua uchumi wetu wa ndani?

10. Ni nani mwenye mpango wa maendeleo unaogusa kila kona; barabara, michezo, burudani, ajira za vijana, na huduma bora kwa wananchi?

11. Ni nani huyo kiongozi mwenye akili timamu, anayejituma, asiye mzushi, mwenye malengo thabiti, na anayejali zaidi matokeo kuliko maneno?

12. Ni nani aliye na nidhamu, maarifa, na maono ya kuweka mfumo imara wa kifedha na kimkakati unaoweza kuibadilisha Taita Taveta kuwa ngome ya maendeleo?

13. Ni nani huyo kiongozi msomi na mwenye weledi, anayeweza kulinda mashirika kama TAVEVO dhidi ya manyang’anyi wa mali ya umma, na kuyafanya kuwa taasisi zinazozalisha faida na kutoa huduma kwa kiwango cha juu?

14. Ni nani huyo mwenye maono ya kweli ya maendeleo endelevu, anayeelewa thamani ya kila raslimali, iwe ni mtu, ardhi, au maji, na kuitumia kwa manufaa ya wote?

15. Ni nani anayeweza kuchanganya busara ya siasa na weledi wa utawala, akitumikia kwa moyo wa unyenyekevu na upendo kwa watu wake?

16. Ni nani mwenye ujasiri wa kumtazama Rais wa Jamhuri machoni na kusema ukweli; akipongeza pale panapostahili, na kupinga bila woga sera zinazokandamiza haki za wananchi wa Taita Taveta?

17. Na hatimaye, ni nani huyu kiongozi mwenye moyo wa utu, anayeheshimu wote kwa usawa, asiyetenga wala kubagua kwa kabila, dini, jinsia, umri au hali ya maisha, bali anayewakumbatia wote kama wana na binti wa Taita Taveta?

Kabla hatujarudia makosa ya jana kwa kutoa uaminifu wetu kwa upofu, hebu tutafakari. Je, kweli mgombea huyo ana sifa zinazohitajika kuiongoza Taita Taveta yetu kuelekea Kanaani ya ahadi?

NI NANI HUYU KIONGOZI?

Kwaela News Network

Leave a Comment
Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

17 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

5 days ago