Mwatate united yang’ara nyumbani baada ya kuinyuka vihiga bullets mabao matano kwa bila, huku Ivan Mgoto akiifungia united mabao matatu katika mchuano wa kenya super league.
Katika dakika ya 33 Brian Kipruto ameifungia United bao la kwanza kupitia mkwaju wa penalti baada ya kuchezewa visivyo katika maeneo ya hatari na beki wa Bullets naye Ivan Tata akiongezea bao la pili katika dakika ya 36 baada ya kupiga kichwa cha kiustadi kabisa.
Katika kipindi cha pili United waliendeleza mashambulizi na juhudi zao zikazaa matunda wakati Alvin Mgoto alipoifungia bao la tatu katika dakika ya 56 na kuongezea bao lingine katika dakika ya 67.
Vihiga walionekana kulemewa kwani mashambulizi yao yalikuwa machache mno huku united wakionekana kuwa na kiu yakuongezea mabao mengine. Katika dakika ya 72 Alvin Mgoto akipachika bao la tano.
Mechi hio imechezwa katika uwanja wa Dawson Mwanyumba mjini Wundanyi katika kaunti ya Taita Taveta. Ijapo kulikuwa na rasharasha za mvua katika kipindi cha pili lakini mashabiki walionekana kufurahishwa. Mwatate United itachuana na timu ya Mara FC kisha kuchuana na Bandari Fc katika kinyang’anyiro cha kombe la Mozari.
~ ML TV
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
Leave a Comment